Mnaotaka kujua ukweli kuhusu mzozo wa Israel na Palestina na yupi ni mkaidi piteni hapa

Eti lilianzishwa na westen! Wana wa Yakobo , Taifa lao lilianzishwa na magharibi! Hilo Taifa lipo kabla ya magharibi.

Wakati wanaenda uhamishoni Misiri hiyo westen ilikuwepo. Wakati wanaenda uhamishoni Babeli, westen ilikuwepo! Ilikuwepo.
Una maana gani,watu hawakusema wamagharibu ndio walilianzisha,bali wao ndio wanalisupport kuwepo pale,mana ukiambiwa taifa maana yake ni kundi la watu hata kama hawana ardhi.

Kwa hiyo issue sio utaifa wao,issue ni ardhi wanayoikalia.

Xx labda utuonyeshe ni wapi katika historia ilieleza kwamba waisrael ardhi yao ni pale.
 
Hivi huko Ulaya waliishi miaka mingapi ao Wayahudi?
 
Hivi huko Ulaya waliishi miaka mingapi ao Wayahudi?
Usipate sana shida, ipo hivi;
Wayahudi walianza kuhama na kuia Ulaya kawenye karne za 10 na 11, Walikaa Ulaya kwa miaka mingi kabla ya mwaka 1947.

Kati ya miaka ya 1800 na mwanzoni mwanzoni mwa miaka ya 1900, kulikuwa na idadi kubwa ya Wayahudi wameenea kuishi Ulaya na waliishi kwa makundi makubwa huku wakikamata nafasi nyingi muhimu kwa kila nchi waliyokuwepo. Kuanzia utafiti, jeshini biashara, uelimu na kila ujuacho. Zaidi, Wayahudi kwenye kila nchi waliyokuwepo walikuwa wakishirikiana sana.

Mwaka 1947 ni upo too vocal katika historia ya Wayahudi kuhama kutoka Ulaya kwa sababu ni mwaka ambapo mbali ya Baraza la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio la Umoja wa Mataifa 181 (Azimio la Ugawaji wa Palestina), ambalo lilisababisha kuundwa kwa taifa la Israel, pia ndiyo mwaka ambao Wayahudi walirudi Israel kwa mkupuo mkubwa zaidi ya awamu nyingine zote.

Kwa hiyo, Wayahudi walikuwa wamekaa Ulaya kwa mamia ya miaka kabla ya mwaka 1947.

kitendo cha Wayahudi kuhamishwa kutoka Ulaya na maeneo mengine na kurudishwa Israel mwaka 1947, halikua tukio la kwanza wala geni, bali ilikua ni muendelezo wa Juhudi za muda mrefu na hapa nitazitaja.

Upekee wa mwaka 1947 ni unatokana kwamba waliorudi safari ile walikua ni wengi sana pia wakaanzisha taifa lao.

Nitazitaja baadhi ya juhudi za uhamishaji wa Wayahudi zilizotokea kabla ya mwaka 1947 ambazo ni kama ifuatavyo;

Awamu ya Kwanza (1881-1903)
Awamu hii ya uhamishaji wa Wayahudi kutoka Ulaya kwenda Palestine land (ilivyojulikana wakati huo), ambayo ilikuwa sehemu ya milki ya Ottoman wakati huo (Ikumbukwe, Ottoman walipoteza kwa Uingereza). So, sababu pia ya dini, Ottoman waliwasaudia zaidi wapalestina dhidi Wayahudi.

Awamu ya Pili (1904-1914)
Katika awamu hii, idadi ya Wayahudi kuhama kutoka Ulaya kwenda Israel iliongezeka. Hiki kilikua ni kipindi cha kabla ya Vita vya Kwanza vya Dunia.

Awamu ya Tatu (1919-1923)
Baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, juhudi za kuhamisha Wayahudi ziliongezeka, na Palestina/Israel ilikuwa chini ya utawala wa Uingereza kwa uangalizi, Tanganyika na Uganda zilivyowekwa chini ya uangalizi wa Uingereza, baada ya German kupokonywa. Hili nalo liliwekwa chini ya Uingereza baada ya Ottoman kupoteza WW1.

Awamu ya Nne na ya Tano (1924-1948)
Wayahudi waliongeza juhudi zao za kuhamia Israel, na idadi yao iliongezeka kwa kiasi kikubwa.

Halafu kuna watu wa kukariri wenyewe kila wakija wanakuja na historia inayoanzia mwaka 1947. Hata huwa sizielewi akili zao, labda wanaowasimulia huwa wana wa hypnotise.
Zile habari za kuhamishiwa Uganda hapa unaziona zina fit sehemu gani ya awamu na ksababu ipi?
Watu wamejazwa porojo tu vichwani. Kwa miaka mingi nilikua nasoma hizo porojo but nazipotezea, ila sasa naona zinazidi kuwatia watu upofu.
 
Wayahudi wamekuwepo eneo hilo kwa miaka mingi ila walikuja kusambaa maeneo mengi duniani mpaka nchi nyinginezo

Wayahudi sio mara ya kwanza kufukuzwa, walifukuzwa uingereza, walifukuzwa marekani ya kipindi hiko kutokana na mishe mishe zao hasa katika masuala ya fedha

Wachache waliobaki kwenye maeneno yao ya asili huko Israel ya sasa, walipitia tabu na dhulma nyingi kutoka kwa wapalestina kutokana na uwingi wao

Ila makazi hayo ni yao na ndio maana hata majina ya miji mingi eneo hilo yana asili ya kiibrenia na sio kiarabu

Issue ni kuwa baada ya kuondoka muda mrefu waliolowea wameweka makazi ya kudumu hivyo hawataki kutoka

Huu msuguano sidhani kama utaisha
 
Hapakuwa pia na taifa linaitwa Israel kabla, Palestine ipo muda tu.
 
Kwa hiyo wazaramo wakirudi maeneo yao hapa dar tuondoke?
 
Kwa hiyo wazaramo wakirudi maeneo yao hapa dar tuondoke?
Wakitaka, na wakiwa na mkakati sahihi, wanaweza kuwaondoa "wageni" bila wageni kujua kuwa wanaondolewa. Lakini hilo litafanikiwa tu ikiwa wataweka malengo ya muda mrefu na kuwa tayari kulipa gharama yoyote itakayohitajika ili yatimie. Kwa hiyo, ni lazima wawe na hela na akili.

Cha kwanza, wahakikishe kuwa kila ardhi na nyumba itakayouzwa Dar inanuniliwa na watu wao (Wazaramo)

Cha pili, wahakikishe kuwa wanawashawishi watu wasiokuwa Wazaramo wakubali kuyauza maeneo yao Dar, ambapo wanunuzi watakuwa waneshaandaliwa, Wazaramo.

Cha tatu, wahakikishe wanakuwa na nguvu ya ushawishi ndani ya Mkoa wa Dar Es Salaam hasa kwa kuhakikisha kuwa wana watu wao katika ngazi mbalimbali za uongozi na uwakilishi kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi ngazi ya kitaifa.

Nne, wawachomeke watu wao kwenye nafasi za kimauzi katika ngazi za kitaifa. Si lazima awe Mzaramo, hata wa kabila jingine, muhimu awe anayasimamia maslahi yao. Kwamba, atakuwa "puppet' wa Wazaramo.

Wakishafanya hivyo, wanaweza wakaamua kubadilisha na jina la Dar Es Salaam, badala ya kuendelea kuitwa hivyo, pakawa UZARAMONI.

Si lazima makabila yote yaondoke, muhimu ni kwamba wao ndiyo wenye nguvu juu ya hatma ya Mkoa wao, UZARAMONI.
 
Nonsense
 
Israel ipo Muhamad hajazaliwa.Huendi kwenda nchi ya watu wakati nchi yako ya asili ipo.Turudi asili yetu,ZIONISM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…