Hivi huko Ulaya waliishi miaka mingapi ao Wayahudi?
Usipate sana shida, ipo hivi;
Wayahudi walianza kuhama na kuia Ulaya kawenye karne za 10 na 11, Walikaa Ulaya kwa miaka mingi kabla ya mwaka 1947.
Kati ya miaka ya 1800 na mwanzoni mwanzoni mwa miaka ya 1900, kulikuwa na idadi kubwa ya Wayahudi wameenea kuishi Ulaya na waliishi kwa makundi makubwa huku wakikamata nafasi nyingi muhimu kwa kila nchi waliyokuwepo. Kuanzia utafiti, jeshini biashara, uelimu na kila ujuacho. Zaidi, Wayahudi kwenye kila nchi waliyokuwepo walikuwa wakishirikiana sana.
Mwaka 1947 ni upo too vocal katika historia ya Wayahudi kuhama kutoka Ulaya kwa sababu ni mwaka ambapo mbali ya Baraza la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio la Umoja wa Mataifa 181 (Azimio la Ugawaji wa Palestina), ambalo lilisababisha kuundwa kwa taifa la Israel, pia ndiyo mwaka ambao Wayahudi walirudi Israel kwa mkupuo mkubwa zaidi ya awamu nyingine zote.
Kwa hiyo, Wayahudi walikuwa wamekaa Ulaya kwa mamia ya miaka kabla ya mwaka 1947.
kitendo cha Wayahudi kuhamishwa kutoka Ulaya na maeneo mengine na kurudishwa Israel mwaka 1947, halikua tukio la kwanza wala geni, bali ilikua ni muendelezo wa Juhudi za muda mrefu na hapa nitazitaja.
Upekee wa mwaka 1947 ni unatokana kwamba waliorudi safari ile walikua ni wengi sana pia wakaanzisha taifa lao.
Nitazitaja baadhi ya juhudi za uhamishaji wa Wayahudi zilizotokea kabla ya mwaka 1947 ambazo ni kama ifuatavyo;
Awamu ya Kwanza (1881-1903)
Awamu hii ya uhamishaji wa Wayahudi kutoka Ulaya kwenda Palestine land (ilivyojulikana wakati huo), ambayo ilikuwa sehemu ya milki ya Ottoman wakati huo (Ikumbukwe, Ottoman walipoteza kwa Uingereza). So, sababu pia ya dini, Ottoman waliwasaudia zaidi wapalestina dhidi Wayahudi.
Awamu ya Pili (1904-1914)
Katika awamu hii, idadi ya Wayahudi kuhama kutoka Ulaya kwenda Israel iliongezeka. Hiki kilikua ni kipindi cha kabla ya Vita vya Kwanza vya Dunia.
Awamu ya Tatu (1919-1923)
Baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, juhudi za kuhamisha Wayahudi ziliongezeka, na Palestina/Israel ilikuwa chini ya utawala wa Uingereza kwa uangalizi, Tanganyika na Uganda zilivyowekwa chini ya uangalizi wa Uingereza, baada ya German kupokonywa. Hili nalo liliwekwa chini ya Uingereza baada ya Ottoman kupoteza WW1.
Awamu ya Nne na ya Tano (1924-1948)
Wayahudi waliongeza juhudi zao za kuhamia Israel, na idadi yao iliongezeka kwa kiasi kikubwa.
Halafu kuna watu wa kukariri wenyewe kila wakija wanakuja na historia inayoanzia mwaka 1947. Hata huwa sizielewi akili zao, labda wanaowasimulia huwa wana wa hypnotise.
Zile habari za kuhamishiwa Uganda hapa unaziona zina fit sehemu gani ya awamu na ksababu ipi?
Watu wamejazwa porojo tu vichwani. Kwa miaka mingi nilikua nasoma hizo porojo but nazipotezea, ila sasa naona zinazidi kuwatia watu upofu.