Mnaotoa fedha kupitia NMB wakala kuweni makini

Hata mi nishawah kupata sms za crdb mara mbili nikashangaa sanaa inakuwaje
 
Boss,hakuna ktk post ya jamaa kauli inayoonyesha kutaka kuharibu biashara ya mtu hii ameitoa kama tahadhari tu na ni vitu hata mamlaka za kiserikali zinafanya mitandao ya simu inafanya hata bank zinafanya.

Kingine inawezekana system ili-shake hili tatizo likatokea maana system yenyewe nayo ni man made vizuri kama wakala mzoefu hili ungelibeba ukaenda kuwa-challenge bankers unaofanya kazi zao ili waendelee kuboresha sector hiyo ili hata wewe isije ikatokea kwako ikakuletea usumbufu.
 
Ili kuepukana na hayo, hebu fateni taratibu.

Leo umepata sms, ila kuna muda hata sms haziji. Je, ungefuatiliaje hela yako? Mpaka ukaangalie statement urudi, wakala akikubishia?

Ukienda kwa Wakala fata taratibu zinavyopaswa. Fika, naomba kutoa fedha. Omba form ya kujaza.

Jaza vizuri. Kabidhi kadi na form kwa pamoja. Akutolee hela kisha baki na copy yako.

Hii ni in case ikatokea tatizo, utakuwa na pa kuanzia. Chana karatasi endapo utajihakikishia kila kitu kipo sawa. Namaanisha baada ya kupitia statement yako ama kuiangalia kwenye internet banking.

Acheni kufanya mambo kienyeji.
 
Nami niliwapigia CRDB wakaniambia ilikuwa mtandao
 
Dah mi nahisi ntakua nimepigwa sana maana harakati zangu nyingi natolea kwa wakala siendi ATM na hivi huwa sijui balance yangu imebaki shingapi ndo hata wakinipiga sitajua .
Huo mchezo aliwahi kuchezewa jamaa mmoja mi nikadhani ni makosa ya bahati mbaya kumbe imeshakua hatari
 
Swali ?password alingiza mwenyewe
Au alimpa huyo dada nmb wakala
Password aingize???

Ova
 
hapa umeongea la maana. sasa niambie USALAMA wa hii app ya NMB kwenye play store, maana wajanja wasije weka ya kwao tukajisajili humo (maana huwa tunatakiwa kuweka namba ya ac na namba ya Siri). tujuze hapa mkuu
 
Nami napata shida hapa!! How!?
 
Kwa mtu anayefanya biashara zisizokuwa na muda maalumu ukimwambia habari za ATM hawezi kukuelewa maana ATM haiwezi kukupa zaidi ya 1mill.(nazungumzia NMB though sijauliza karibuni kama utaratibu huo ulibadilishwa ama lah)
Mi natoaga pesa ya bia tu kaka.
 
hapa umeongea la maana. sasa niambie USALAMA wa hii app ya NMB kwenye play store, maana wajanja wasije weka ya kwao tukajisajili humo (maana huwa tunatakiwa kuweka namba ya ac na namba ya Siri). tujuze hapa mkuu
Hakuna njia za ku-counter check baada ya kuweka account namba na neno la siri?
 

Mtoa fedha ameweka password mara moja tuu kiongoz ! Nafikir huenda hizi machine za nmb wakala kuna wajanja wanazichezea.
 
Mawakala mnaiba bhana
 
Duh !
Basi benki nyingi za Bongo zimeoza Kwa kukosa weledi ,wanajazana sifa za kijinga tu
Hasa hizi local banks
Pua pua pua kabisa
Maana hata crdb nao ni wapuuzi wakubwa ,kuna malalamiko mengi ya watu pesa zao kukwapuliwa humo kwenye accounts za crdb ,tena na wafanyakazi wa benki wenyewe
Unprofessionalism Kwa mtanzania ni chanda na pete
Hawa mbwa kwanini hawawezi kujifunza proffesionalism kwa benki za majirani zetu wakenya hawa mfano KCB na Equity ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…