Kampuni la Kimarekani Apple, maarufu kwa kuuza bidhaa za electronics na accessories zake, wanauza ivyo vitu bei ghali sana.
Inawezekana ikawa ni value for money, ila kuna baadhi ya vitu ni wazi wanawaibia "loyal customers" wake, sema ndio ivyo hawaoni au wanajizima data.
Tuachane na iPhone zao kua Million 3 kwenda juu, au Laptop zao za kishua. Ebu Kwa mfano checki izi products:
Mac Pro wheels $700 (Tsh Mil 1.8)
Hii sio computer, ni magurudumu manne ya kuweka kwenye CPU sijui tuiite ya Mac Pro. Hujakosea kusoma.
View attachment 3000624Haya matairi ilibidi wayagawe bure unavyonunua iyo bidhaa yao.
Mac Pro stand $1000 (Tsh Mil 2.6)
Naam. Mil 2.6 tunanunua stendi ya kuiwekea Monitor yetu ya Mac.
View attachment 3000625Hii pia ilitakiwa upewe bure. Kwann walitengeneza computer isio na stendi?
Mikanda ya saa $100 (Tsh Laki 2.6)
Achana na bei ya saa, mkanda tu huu unauzwa laki 2 na nusu na zaidi.
View attachment 3000608
Airpods Max $550 (Tsh Mil 1.4)
Utakua ushakutana na mabishoo wamevaa copy ya aya madude.
View attachment 3000627
Aisee original yake ndio ivo, Mil 1.4 cash.
Apple Pencil $130 (Tsh 340,000/=)
Hii wenzio Samsung ukinunua Tab wanakupa bure sijui kwann wao wanauza.
View attachment 3000606
Mac Pro $7000 (Tsh Mil 18)
Ukiliona kwenye picha kama kidude cha kusugulia nyanya au karoti. Ila ndio ivyo tena, bei ya gari.
View attachment 3000631
Waya type C $30 (Tsh 77,000/=)
Waya tu, wa mita 2 unauzwa hivi. Bila kichwa. Bila protector. Bila kava. Waya.
View attachment 3000614
Cover la Simu la Silicon $50 (Tsh 130,000/=)
Haya makava tunayaona kwa elfu 5 yanauzwa Kariakoo. Wao wanauza bei ya simu.
View attachment 3000609
Mac Pro Display $1500 na Stendi yake inafika hadi $2000 (Tsh Mil 3.9 hadi Mil 5.1)
Hii ni display ya kile kidude cha kusugulia nyanya. Display tu.
View attachment 3000612
Airpods Pro $250 (Tsh 650,000)
Sijawahi tumia kwahiyo sijui mziki wake ila kutoa Laki 6 kisa utu tudude hapana.
View attachment 3000621
Polishing Cloth $20 (Tsh 52,000)
Kitambaa cha kusafishia kioo cha simu au laptop au ipad kinauzwa bei ivo.
View attachment 3000638
Apple Mouse $100 (Tsh 250,000)
Hii ni mouse kama unayoijua sema ya kuchaji.
View attachment 3000648Hafu port ya kuchajia ipo chini kwahiyo ikiisha chaji hauwezi kutumia. Kha.
View attachment 3000650
Mi labda sina hela, ila kununua bidhaa ya Apple naona kabisa napigwa. Ata iPhone najua ina nguvu ina balaa ila kama wanakuibia kwenye bidhaa zingine kwann wasikuibie kwenye iPhone.
Nimejiandaa kuambiwa nitafute hela.