Mnaotumia bidhaa za Apple® Mnapigwa sana. Sijui hata mnavyotoa hela mnafikiriaga nini?

Mnaotumia bidhaa za Apple® Mnapigwa sana. Sijui hata mnavyotoa hela mnafikiriaga nini?

Kampuni la Kimarekani Apple, maarufu kwa kuuza bidhaa za electronics na accessories zake, wanauza ivyo vitu bei ghali sana.

Inawezekana ikawa ni value for money, ila kuna baadhi ya vitu ni wazi wanawaibia "loyal customers" wake, sema ndio ivyo hawaoni au wanajizima data.

Tuachane na iPhone zao kua Million 3 kwenda juu, au Laptop zao za kishua. Ebu Kwa mfano checki izi products:

Mac Pro wheels $700 (Tsh Mil 1.8)

Hii sio computer, ni magurudumu manne ya kuweka kwenye CPU sijui tuiite ya Mac Pro. Hujakosea kusoma.

Haya matairi ilibidi wayagawe bure unavyonunua iyo bidhaa yao.

Mac Pro stand $1000 (Tsh Mil 2.6)

Naam. Mil 2.6 tunanunua stendi ya kuiwekea Monitor yetu ya Mac.
Hii pia ilitakiwa upewe bure. Kwann walitengeneza computer isio na stendi?

Mikanda ya saa $100 (Tsh Laki 2.6)

Achana na bei ya saa, mkanda tu huu unauzwa laki 2 na nusu na zaidi.


Airpods Max $550 (Tsh Mil 1.4)
Utakua ushakutana na mabishoo wamevaa copy ya aya madude.

Aisee original yake ndio ivo, Mil 1.4 cash.

Apple Pencil $130 (Tsh 340,000/=)
Hii wenzio Samsung ukinunua Tab wanakupa bure sijui kwann wao wanauza.


Mac Pro $7000 (Tsh Mil 18)
Ukiliona kwenye picha kama kidude cha kusugulia nyanya au karoti. Ila ndio ivyo tena, bei ya gari.



Waya type C $30 (Tsh 77,000/=)
Waya tu, wa mita 2 unauzwa hivi. Bila kichwa. Bila protector. Bila kava. Waya.


Cover la Simu la Silicon $50 (Tsh 130,000/=)
Haya makava tunayaona kwa elfu 5 yanauzwa Kariakoo. Wao wanauza bei ya simu.



Mac Pro Display $1500 na Stendi yake inafika hadi $2000 (Tsh Mil 3.9 hadi Mil 5.1)

Hii ni display ya kile kidude cha kusugulia nyanya. Display tu.



Airpods Pro $250 (Tsh 650,000)
Sijawahi tumia kwahiyo sijui mziki wake ila kutoa Laki 6 kisa utu tudude hapana.


Polishing Cloth $20 (Tsh 52,000)
Kitambaa cha kusafishia kioo cha simu au laptop au ipad kinauzwa bei ivo.


Apple Mouse $100 (Tsh 250,000)
Hii ni mouse kama unayoijua sema ya kuchaji.Hafu port ya kuchajia ipo chini kwahiyo ikiisha chaji hauwezi kutumia. Kha.

Mi labda sina hela, ila kununua bidhaa ya Apple naona kabisa napigwa. Ata iPhone najua ina nguvu ina balaa ila kama wanakuibia kwenye bidhaa zingine kwann wasikuibie kwenye iPhone.

Nimejiandaa kuambiwa nitafute hela.
kama huna fedha wewe songa mbele wenzako watanunua.
 
Hiyo ya kusugulia nyanya na karoti ni kitu gani na inatumika kwenye nini
Kama CPU ya PC za kawaida.

images (27).jpeg
maxresdefault.jpg
 
Kwa products zao naona ni sawa tu, wakitoa kitu wametoa, materials wanayotumia ni next level, designing n.k kingine jamaa wanatoa toleo la simu moja ambayo ni flagship, mfano samsung wana simu hizi za bei nafuu mfano A series ku compete na Tecno, Infinix n.k kitu ambacho iphone hawafanyi, ukiikamata iphone mkononi au macbook unajua kabisa nimeshika kitu.

Kingine Apple bidhaa zao wana offer mambo mengi ambayo wakati mwingine unahisi huna matumizi nayo.

Last jamaa wana total control of their devices kuanzia software na hardware ni wao wana design ukiachana na infinix, oppo n.k ambapo OS wanategemea ni android, hili ni jambo linawafanya vifaa vyao viwe na best perfomance cause wana customize OS yao iendane na hardware zao, Siwezi hata kuongelea nikaeleweka lakini jamaa wanapobuni product wanaangalia kila kitu hata features za kupuuzia jamaa wanafanya deep research, hawachukilii vitu poa.

Kingine soko lao sidhani kama wanalenga zaidi nchi zetu za ulimwengu wa tatu that's why tunaona ni expensive.

Naona wapo sawa tu.
Kuongezea iphone wanatengeneza flagship phones only, hawana midrange wala low range.
Now flagship phone zina belong to watu wenye uwezo maana mle ndani wana flagship features

Tatizo la wengi wananunua as symbol of status lakin hawajui how to use those features
 
Back
Top Bottom