Mnaotumia bidhaa za Apple® Mnapigwa sana. Sijui hata mnavyotoa hela mnafikiriaga nini?

Mnaotumia bidhaa za Apple® Mnapigwa sana. Sijui hata mnavyotoa hela mnafikiriaga nini?

Samsung kuna simu wanatumia mediatek, Nokia kuna simu wanatumia SPD, ulishasikia iPhone anatumia mediatek au SPD?

Apple alikuwa anatumia intel kwenye computer zake hivi sasa ana processor zake za M series, jamaa wapo vizuri...
Kwani MediaTek ni mbaya?
 
Hiyo AirPods Max kuna jamaa anayo copy, bas anavyosumbua wenzie.
Na kaletewa kutoka Australia, bas full tafraniii.
 
Kwa products zao naona ni sawa tu, wakitoa kitu wametoa, materials wanayotumia ni next level, designing n.k kingine jamaa wanatoa toleo la simu moja ambayo ni flagship, mfano samsung wana simu hizi za bei nafuu mfano A series ku compete na Tecno, Infinix n.k kitu ambacho iphone hawafanyi, ukiikamata iphone mkononi au macbook unajua kabisa nimeshika kitu.

Kingine Apple bidhaa zao wana offer mambo mengi ambayo wakati mwingine unahisi huna matumizi nayo.

Last jamaa wana total control of their devices kuanzia software na hardware ni wao wana design ukiachana na infinix, oppo n.k ambapo OS wanategemea ni android, hili ni jambo linawafanya vifaa vyao viwe na best perfomance cause wana customize OS yao iendane na hardware zao, Siwezi hata kuongelea nikaeleweka lakini jamaa wanapobuni product wanaangalia kila kitu hata features za kupuuzia jamaa wanafanya deep research, hawachukilii vitu poa.

Kingine soko lao sidhani kama wanalenga zaidi nchi zetu za ulimwengu wa tatu that's why tunaona ni expensive.

Naona wapo sawa tu.
Cha ajabu vioo vyao wanamtegemea samsung ..?
 
Mchina aliniangusha aisee mimi mwenyewe nilikuwa na Redmi note 11 pro nilikuwa navimba mega pixel 108 AI Camera kumbe hamna kitu ila kuna vitu Redmi ipo poa sana
Sometimes uangalie hiyo Redmi ni Tsh ngapi na hiyo iPhone ni Tsh ngapi
In fact hata simu ya Xiaomi yenye Kamera kali kuliko zote (Xiaomi 14 Ultra) ina 50MP wakati midrange zake zina hadi 200MP. Kwa hiyo megapixel si kigezo cha ubora wa kamer
 
Kampuni la Kimarekani Apple, maarufu kwa kuuza bidhaa za electronics na accessories zake, wanauza ivyo vitu bei ghali sana.

Inawezekana ikawa ni value for money, ila kuna baadhi ya vitu ni wazi wanawaibia "loyal customers" wake, sema ndio ivyo hawaoni au wanajizima data.

Tuachane na iPhone zao kua Million 3 kwenda juu, au Laptop zao za kishua. Ebu Kwa mfano checki izi products:

Mac Pro wheels $700 (Tsh Mil 1.8)

Hii sio computer, ni magurudumu manne ya kuweka kwenye CPU sijui tuiite ya Mac Pro. Hujakosea kusoma.

View attachment 3000624Haya matairi ilibidi wayagawe bure unavyonunua iyo bidhaa yao.

Mac Pro stand $1000 (Tsh Mil 2.6)

Naam. Mil 2.6 tunanunua stendi ya kuiwekea Monitor yetu ya Mac.
View attachment 3000625Hii pia ilitakiwa upewe bure. Kwann walitengeneza computer isio na stendi?

Mikanda ya saa $100 (Tsh Laki 2.6)

Achana na bei ya saa, mkanda tu huu unauzwa laki 2 na nusu na zaidi.
View attachment 3000608

Airpods Max $550 (Tsh Mil 1.4)
Utakua ushakutana na mabishoo wamevaa copy ya aya madude.
View attachment 3000627
Aisee original yake ndio ivo, Mil 1.4 cash.

Apple Pencil $130 (Tsh 340,000/=)
Hii wenzio Samsung ukinunua Tab wanakupa bure sijui kwann wao wanauza.
View attachment 3000606

Mac Pro $7000 (Tsh Mil 18)
Ukiliona kwenye picha kama kidude cha kusugulia nyanya au karoti. Ila ndio ivyo tena, bei ya gari.
View attachment 3000631

Waya type C $30 (Tsh 77,000/=)
Waya tu, wa mita 2 unauzwa hivi. Bila kichwa. Bila protector. Bila kava. Waya.
View attachment 3000614

Cover la Simu la Silicon $50 (Tsh 130,000/=)
Haya makava tunayaona kwa elfu 5 yanauzwa Kariakoo. Wao wanauza bei ya simu.

View attachment 3000609

Mac Pro Display $1500 na Stendi yake inafika hadi $2000 (Tsh Mil 3.9 hadi Mil 5.1)

Hii ni display ya kile kidude cha kusugulia nyanya. Display tu.
View attachment 3000612

Airpods Pro $250 (Tsh 650,000)
Sijawahi tumia kwahiyo sijui mziki wake ila kutoa Laki 6 kisa utu tudude hapana.
View attachment 3000621

Polishing Cloth $20 (Tsh 52,000)
Kitambaa cha kusafishia kioo cha simu au laptop au ipad kinauzwa bei ivo.
View attachment 3000638

Apple Mouse $100 (Tsh 250,000)
Hii ni mouse kama unayoijua sema ya kuchaji.View attachment 3000648Hafu port ya kuchajia ipo chini kwahiyo ikiisha chaji hauwezi kutumia. Kha.View attachment 3000650

Mi labda sina hela, ila kununua bidhaa ya Apple naona kabisa napigwa. Ata iPhone najua ina nguvu ina balaa ila kama wanakuibia kwenye bidhaa zingine kwann wasikuibie kwenye iPhone.

Nimejiandaa kuambiwa nitafute hela.
Wewe siyo mtumiaji wa bidhaa za Apple lakini unaandika makala ndefu sana na kujaza picha za bidhaa hizo zaapple kwa nini? Unataka kushwashishi wengine pia wasizitumuie kusudi muwe wengi? Kama humudu kutumia bidhaa za apple waachie wanaozimudu wewe tumia zile unazozimudu, maisha yanaendelea. Umeandika bdihaa za apple kama vile unatumia bidhaa nyingine zote sipokuwa za apple tu ilihali makampuni ya eletcronics leo yapo lukuki. Kama wewe hutumii Apple, kuna wengine hawatumii Samsung, kuna wasitotumia Tecno, kuna wasiotumia Huawei, Kuna wasiotumia BLu, kuna wasiotumia Google Pixle, Kuna wasiotumia Infix, Kuna wasiotumia Xiaomi, Kuna wasiotumia Motororola, Kuna wasiotumia Micromax, kuna wasitumia brand nyingi sana za electronics; je wewe unazitumia zote hizo isipokuwa apple tu?
 
Upeo wa macho yako umefika hapo. Maskini anawaza kutokana na umaskini wake na tajiri the same.
Mimi nakunywa Cappucino kila siku hapa Masaki Koffe Kafe, kikombe Kimoja ni Tshs 12,000 bila hata kipande cha cake.
Mwenye mawazo ya kimaskini anakwambia hiyo hela unakunywa kawaha mwezi mzima sehemu za uswahilini, kupanga ni kuchagua. Kwa siku nikikaa kikao cha kawaida posho ni Tsh 400,000/- , kunywa elfu 50,000 kwa siku ni ndogo sana.
ukiwa mwongo mwongo unapaswa kua na akili sasa wewe akili huna. tuishie hapo nisije kukuvua nguo.

nb. aya ya 1 naafikiana na wewe.
 
Kampuni la Kimarekani Apple, maarufu kwa kuuza bidhaa za electronics na accessories zake, wanauza ivyo vitu bei ghali sana.

Inawezekana ikawa ni value for money, ila kuna baadhi ya vitu ni wazi wanawaibia "loyal customers" wake, sema ndio ivyo hawaoni au wanajizima data.

Tuachane na iPhone zao kua Million 3 kwenda juu, au Laptop zao za kishua. Ebu Kwa mfano checki izi products:

Mac Pro wheels $700 (Tsh Mil 1.8)

Hii sio computer, ni magurudumu manne ya kuweka kwenye CPU sijui tuiite ya Mac Pro. Hujakosea kusoma.

View attachment 3000624Haya matairi ilibidi wayagawe bure unavyonunua iyo bidhaa yao.

Mac Pro stand $1000 (Tsh Mil 2.6)

Naam. Mil 2.6 tunanunua stendi ya kuiwekea Monitor yetu ya Mac.
View attachment 3000625Hii pia ilitakiwa upewe bure. Kwann walitengeneza computer isio na stendi?

Mikanda ya saa $100 (Tsh Laki 2.6)

Achana na bei ya saa, mkanda tu huu unauzwa laki 2 na nusu na zaidi.
View attachment 3000608

Airpods Max $550 (Tsh Mil 1.4)
Utakua ushakutana na mabishoo wamevaa copy ya aya madude.
View attachment 3000627
Aisee original yake ndio ivo, Mil 1.4 cash.

Apple Pencil $130 (Tsh 340,000/=)
Hii wenzio Samsung ukinunua Tab wanakupa bure sijui kwann wao wanauza.
View attachment 3000606

Mac Pro $7000 (Tsh Mil 18)
Ukiliona kwenye picha kama kidude cha kusugulia nyanya au karoti. Ila ndio ivyo tena, bei ya gari.
View attachment 3000631

Waya type C $30 (Tsh 77,000/=)
Waya tu, wa mita 2 unauzwa hivi. Bila kichwa. Bila protector. Bila kava. Waya.
View attachment 3000614

Cover la Simu la Silicon $50 (Tsh 130,000/=)
Haya makava tunayaona kwa elfu 5 yanauzwa Kariakoo. Wao wanauza bei ya simu.

View attachment 3000609

Mac Pro Display $1500 na Stendi yake inafika hadi $2000 (Tsh Mil 3.9 hadi Mil 5.1)

Hii ni display ya kile kidude cha kusugulia nyanya. Display tu.
View attachment 3000612

Airpods Pro $250 (Tsh 650,000)
Sijawahi tumia kwahiyo sijui mziki wake ila kutoa Laki 6 kisa utu tudude hapana.
View attachment 3000621

Polishing Cloth $20 (Tsh 52,000)
Kitambaa cha kusafishia kioo cha simu au laptop au ipad kinauzwa bei ivo.
View attachment 3000638

Apple Mouse $100 (Tsh 250,000)
Hii ni mouse kama unayoijua sema ya kuchaji.View attachment 3000648Hafu port ya kuchajia ipo chini kwahiyo ikiisha chaji hauwezi kutumia. Kha.View attachment 3000650

Mi labda sina hela, ila kununua bidhaa ya Apple naona kabisa napigwa. Ata iPhone najua ina nguvu ina balaa ila kama wanakuibia kwenye bidhaa zingine kwann wasikuibie kwenye iPhone.

Nimejiandaa kuambiwa nitafute hela.
Mkuu naona labda sijui ni kwa makusudi au umeamua kufurahisha tu genge, vifaa vy Apple ni vifaa vyenye ubora sana, lakini pia kampuni nyingine nyingi zinatoa kompyuta/laptops ambazo bei zake ni sawa na hizi za Apple hapa Bongo tu kuna watu wanaunda PC za game na kuuza milioni 9 hiyo ni CPU tu bila monitor, sishangai kuona bei kubwa sababu pesa yetu ya madafu kwa sasa ipo chini sana kununua USD sasa ni 2690 , wa kulaumu ni serikali yakokwa kuifanya pesa ya madafu ishuke thamani, hata magari kuna benz, suzuki VX8 bei ha hata spare zake hazifanani mkuu. Nikuambie tu kama umetumia vifaa vya Apple basi ni sawa na mtu anayetumia VX8 au benzi umwambie aendeshe kirikuu mkuu. Kwa mtu ambaye maisha yake yanategemea data,graphics,game/videos rendering na takataka nyingine kuwa na vifaa vya apple ndio uwekezaji kwenye uzalishaji na si anasa,hiyo unayoita kikunia nyanya haina tofauti na PC wanazounda wabongo zipo hata za 10milion kulingana na uwezo wake. Ngoja na mimi nikuambie sijui umejiandaa? TAFUTA HELA, mengine yote utayaona rahisi.
 
Back
Top Bottom