Mnaotunza watoto wa ndugu nje ya ndoa, naomba ushauri

ufumawicha

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
510
Reaction score
213
Habari wanaJF!

Nina mtoto wa miaka miwili na nusu ambaye analelewa na mama yake baada ya mkubwa wangu kufariki Ila pesa ya matumizi ninatoa Mimi kwa niaba ya marehemu.

Mwanzoni tulienda vizuri lakini shemeji kabadilika ghafla. Leo hii kila pesa ninayompa ya kumtunza huyo mtoto anadai haitoshi. Amefikia hadi hatua ninampa fedha anagoma kupokea.

Naombeni ushauri sheria zinasemaje? Mtoto mmoja anatunzwaje? Shemeji na mtoto wako Tabora.
 
Anatumia mgongo wa mtoto kukudangia, dhambi kubwa sana hii.
 
Mkuu huyo si mtoto wako na hujazaa naye, akizingua mpotezee akiona hata hiyo aliyokuwa anakataa hapati atakuja kukupigia magoti .

Kwa vile mtoto hajaanza shule kata kwanza huduma ,atakuja na mawili baada ya kumnyima msaada.

1. Kuja kubebeleza ili apate hata hiyo kidgo.

2. Atatishia namleta mtoto wenu mlee ,hapo ndo poa
 
Kwa niaba ya marehemu
 
Hii ndio yenyewe
 
Jifanye kauzu, usimpe chochote atakutafuta mwenyewe.
Mwambie Mimi bajeti yangu hii hutaki basi nipe Mtoto, hao wadada hawana shukrani
Kwanza akienda ustawi jamii unaambiwa umpe 30,000-40000 tu kwa mwezi
 
Kiri huyo ni mtoto wako. Sidhani kama shemeji yako anaweza kukulazimisha kutoa matumizi labda kama umezaa naye. Kuwa mkweli upate msaada sahihi.
Wapo, nina mfano halisi wa aina ya huyo shemeji.
Kuna watu wana jeuri za kijinga af hawana adabu.
 
Ajifanye kauzu tu hata kwa miezi miwili ndo huyo shemeji yake atajua hela ilivyo ngumu kupata
 
Mkuu huyo si mtoto wako na hujazaa naye, akizingua mpotezee akiona hata hiyo aliyokuwa anakataa hapati atakuja kukupigia magoti .

Kwa vile mtoto hajaanza shule kata kwanza huduma ,atakuja na mawili baada ya kumnyima msaada.

1. Kuja kubebeleza ili apate hata hiyo kidgo.

2. Atatishia namleta mtoto wenu mlee ,hapo ndo poa
Nashukuru kwa ushauri nitaufanyia kazi
 
Wapo, nina mfano halisi wa aina ya huyo shemeji.
Kuna watu wana jeuri za kijinga af hawana adabu.
Kiri huyo ni mtoto wako. Sidhani kama shemeji yako anaweza kukulazimisha kutoa matumizi labda kama umezaa naye. Kuwa mkweli upate msaada sahihi.
Wapo kibao mzee na kuna mwanangu nae analea na kuhudumia watoto wa bro wake aliepita hivi.
Wamebaki na shemeji yake na yeye ndo main sponsor hapo.

Maisha yana mambo mengi mkuu
 
Halafu kingine niwashauri wanaume wenzangu
Hawa shemeji zetu wa urithi usijaribu kumla kimasihara,!!
Tunza Mtoto au watoto basi. Ukimla tu anaota pembe anaweza kukuvunjia hata ndoa!... Dharau, kiburi, jeuri zinaanza, anaona naye ni mke halali
 
Back
Top Bottom