Mnaotunza watoto wa ndugu nje ya ndoa, naomba ushauri

Mnaotunza watoto wa ndugu nje ya ndoa, naomba ushauri

Shemeji yako ni kiazi, ye kwa akili yake anadhani hilo ni jukumu lako wewe, wakati wewe hapo unafanya hisani tu, mpotezee kwanza ili aende akawasimulie na wenzie wenye tabia kama zake.
 
Wanawake wa Tabora wanapenda kulea vi serengeti boys.... hapo utakuta wewe unahudumia watoto wawili, chukua huyo damu yako ukae nae hapo.
 
Mtoto sio wako anadai hela haitoshi, dawa ya jeuri ni jeuri akisema ndogo mwambie uwezo wako ndio ulipoishia halafu mkaushie ikibidi wakati anaongea hayo umrekodi Kama ushahidi wa baadaye. Huyo ameshindwa kutumia bahati Mara nyingi ndugu wengi mume akishafariki mzigo wa watoto hubaki wa mjane wengine wote huingia mitini.
 
Wapo kibao mzee, na kuna mwanangu nae analea na kuhudumia watoto wa bro wake aliepita hivi.
Wamebaki na shemeji yake na yeye ndo main sponsor hapo.

Maisha yana mambo mengi mkuum
Halafu unaweza kuta mama watoto ni mzima tu na afya yake ila hataki kujishughulisha anasubiri shemeji alete matumizi na anampangia hadi kiasi cha kutoa wakati mtu anafanya tu msaada as sio watoto wake hao.

Ila mnahudumia familia zisizo zenu Mungu azidi kuwabariki.
 
Maybe wewe ni msimamizi wa mirathi ya marehemu, bibie anaona unafaidika na mali za mumewe na humsaidii, sina uhakika.
 
Halafu unaweza kuta mama watoto ni mzima tu na afya yake ila hataki kujishughulisha anasubiri shemeji alete matumizi na anampangia hadi kiasi cha kutoa wakati mtu anafanya tu msaada as sio watoto wake hao.

Ila mnahudumia familia zisizo zenu Mungu azidi kuwabariki.
What if jamaa anashikilia mali za marehemu kaka yake
 
Kama hawakufunga ndoa na jamaa alikuwa na wake wengi inawezekana
Maybe... sijui case ya mtoa mada iko vipi ila kwa ninayemfahamu ye anahudumia kwa kujitolea, hana mali yoyote ya kaka yake, anapitia changamoto kama za mtoa mada.
 
Mambo mengine yanachanganya sana, ndio maana sometimes kukaa na ndugu au kulea mtoto wa ndugu sitakagi
 
Halafu kingine niwashauri wanaume wenzangu
Hawa shemeji zetu wa urithi usijaribu kumla kimasihara,!!
Tunza Mtoto au watoto basi. Ukimla tu anaota pembe anaweza kukuvunjia hata ndoa!... Dharau, kiburi, jeuri zinaanza, anaona naye ni mke halali
Huyo dharau alianza muda mrefu!Hata kifo cha kaka,amechangia sana!Yaani kupitia matatizo ya kaka,sasa ninaamini kuwa wanaume kwa sasa wanaongoza kunyanyaswa kijinsia na wake zao!
 
Wanawake wengi baada ya kuzaa na mwanaume kabla ya ndoa wanaingiza matatizo yao kupitia watoto ndo maana wanaume wanaamua kukimbia majukumu kwa udanganyifu huo.
 
Kiri huyo ni mtoto wako. Sidhani kama shemeji yako anaweza kukulazimisha kutoa matumizi labda kama umezaa naye. Kuwa mkweli upate msaada sahihi.
Umewaza kama mimi mkuu yaani mtoto sio wako halafu alete nyodo na anajua kabisa muhusika amefariki big no.
 
Back
Top Bottom