Mnaowalea watoto wa kike bila kuwafundisha kazi za nyumbani mnawaandalia mazingira gani wakiwa wakubwa?

 
Wee hata kuniita shogare khaa!! Sijapentraa wala nini 🥺
Usijali next wkend
Napenda movie
Naanzia movie mliman city
Halafu ,masaki kuleee🤣🤣🤣
Nitakuita shoooo
 
Actually sio wa kike tu lakini watoto wote wanapaswa kufundisha kazi zote bila kujali jinsia zao [emoji108]
 
Yaani kwa maelezo yako bado unakubaliana na mleta mada kuwa mwanamke yeye ndio mwenye majukumu ya jikoni. Mwanaume kiubinadamu na kwa uhitaji unapaswa kujua kupika ili kutoa usaidizi tu.
Mkuu,

Endelea kunisoma utapata uelewa kamili wa msimamo wangu.

Huko mbele nimeeleza kwamba hata huyu muungwana anayetaka "kumsaidia" mke wake, kwa roho nzuri kabisa, bado ana kasumba ya gender roles na anaona kuingia jikoni kufanya kazi za jikoni ni kumsaidia mkewe, wakati hayo ni majukumu ya kazi za nyumbani tu watu wanasaidiana wote.

Nafikiri umenipata vibaya nilivyomnukuu huyo muungawana, nimeelezea msimamo wangu vizuri kwamba kuweka gender based roles ni kitu kibaya.
 
Ok nimekuelewa uzuri sasa.
kwa kweli ni muhimu sana watoto wa jinsi zote wajifunze majukumu ya nyumbani kama stadi za maisha.

sehemu sikupati sawa sawa ni huu msimamo wako ambao kwa tafsiri yake majukumu kama ya Usafi, upishi ni-SHARED ROLE KWA WOTE MKE NA MUME. Hiki ndio una maanisha?
 
Correct.

Ultimately, watu watajipangia wenyewe, lakini, inafaa jamii iondokane kwenye hizi kasumba za kusema kazi fulani ni za wanawake, na kazi fulani ni za wanaume.

Yani hata watu wakigawana majukumu, si lazima majukumu fulani yawe ya wanawake na majukumu fulani yawe ya wanaume, kwa sababu wanawake tofauti wana uwezo na utashi tofauti, na wanaume tofauti wana uwezo na utashi tofauti.

Nilikuwa naangalia movie mpya ya hii production company ya Obama, on Netflix (sasa hivi ni movie namba moja Netflix), hii movie inaitwa "Leave The World Behind".

Spoiler alert, kwa wasiotaka spoilers.

Familia imeenda vacation, wamekodi nyumba, wanataka ku connect Wi-Fi, mama anashindwa, anamwambia baba hapa tuna tatizo, Wi-Fi haifanyi kazi, unafikiri tunahitaji ku reboot Wi-Fi?

Kikawaida, kwenye mfumodume, baba ndiye mtu anayetakiwa kuwa na troubleshooting role.

Baba akamjibu mama kirahisi kabisa, sijui, wewe ndiye mtu wa tech katika familia hii.

Hapo unaona kuwa, katika familia ambayo baba ni mpishi professional na mama ni IT expert, kumtaka mama apike chakula na baba atatue matatizo ya router ni kutumia vipaji vyao vibaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…