Ok nimekuelewa uzuri sasa.
kwa kweli ni muhimu sana watoto wa jinsi zote wajifunze majukumu ya nyumbani kama stadi za maisha.
sehemu sikupati sawa sawa ni huu msimamo wako ambao kwa tafsiri yake majukumu kama ya Usafi, upishi ni-SHARED ROLE KWA WOTE MKE NA MUME. Hiki ndio una maanisha?
Correct.
Ultimately, watu watajipangia wenyewe, lakini, inafaa jamii iondokane kwenye hizi kasumba za kusema kazi fulani ni za wanawake, na kazi fulani ni za wanaume.
Yani hata watu wakigawana majukumu, si lazima majukumu fulani yawe ya wanawake na majukumu fulani yawe ya wanaume, kwa sababu wanawake tofauti wana uwezo na utashi tofauti, na wanaume tofauti wana uwezo na utashi tofauti.
Nilikuwa naangalia movie mpya ya hii production company ya Obama, on Netflix (sasa hivi ni movie namba moja Netflix), hii movie inaitwa "Leave The World Behind".
Spoiler alert, kwa wasiotaka spoilers.
Familia imeenda vacation, wamekodi nyumba, wanataka ku connect Wi-Fi, mama anashindwa, anamwambia baba hapa tuna tatizo, Wi-Fi haifanyi kazi, unafikiri tunahitaji ku reboot Wi-Fi?
Kikawaida, kwenye mfumodume, baba ndiye mtu anayetakiwa kuwa na troubleshooting role.
Baba akamjibu mama kirahisi kabisa, sijui, wewe ndiye mtu wa tech katika familia hii.
Hapo unaona kuwa, katika familia ambayo baba ni mpishi professional na mama ni IT expert, kumtaka mama apike chakula na baba atatue matatizo ya router ni kutumia vipaji vyao vibaya.