Mnaowalea watoto wa kike bila kuwafundisha kazi za nyumbani mnawaandalia mazingira gani wakiwa wakubwa?

Mnaowalea watoto wa kike bila kuwafundisha kazi za nyumbani mnawaandalia mazingira gani wakiwa wakubwa?

Ni siku ya leo nimekumbuka nikiwa kwenye mahusiano hapo miaka ya 2015 na binti moja mrembo, mapenzi yalinoga sana lakini baada yakuanza kuishi nae niliona mapungufu mengi sana, la kwanza kabisa alikuwa hajui kupika yani ugali sometimes unakuwa mbichi halafu hata hajishughulishi kuongeza mboga za pembeni wakati vitu vipo vya kutosha stoo, mambo ya kunishuguhulikia usafi wangu mwanaume wake kama kunifulia nguo nayo ni mpaka iwe vuta nikuvute tena jeans anafulia brush!!, Kwakweli taa nyekundu iliwaka kichwani suala la ndoa likafutika kabisa.

Kumuandaa mtoto wako wa kike kujua kuishi kwenye ndoa za kiafrika ni jukumu ambalo wazazi hasa mama hapaswi kulilazia damu,

Kuna wazazi tunawaona kwamba wakiwa na vijipesa basi wanamleta house girl amsaidie mtoto wa kike kazi ambazo inabidi azifanye yeye ili ziwe mazoea ya kumjengea uzoefu ya msingi ya kuwa mke anaeweza kuishi ndani ya ndoa za kiafrika.

Tutofautishe vitu viwili, kuna kufanya kitu kwa kuweza baada ya kujifunza na kufanya kitu kwa mazoea, unaweza ukajifunza leo hii kupika hata kupitia youtube ama goole lakini itachukua muda mrefu sana kujenga mazoea ya kupika, ila kama umeshazoeshwa tangu mtoto si kwamba tu unaweza lakini umepata uzoefu mwingi sana na tayari imeshakua ni mazoea, unapika bila kuhisi uchovu wala hujivuti, una enjoy kupika inakua sio shughuli bali hobby.

Sasa tukija kwa watoto hawa wanaolelewa kitamthilia inakuwa ngumu sana mwanaume wa kiafrika kumuoa maana sisi wanaume wa kiafrika suala la kwanza kwenye kuoa huwa "tunavuta jiko" hivyo vingine huwa ni vya ziada tu vikiwemo elimu, uzuri, n.k. na ukikosea ukifanya vinginevyo ujipange!! Jiko ndio kazi kuu ya mwanamke akiwa ndani ikifuatiwa na usafi wa mme wake kuanzia kumfulia nguo zake mpaka soksi, na majukumu mengine kama usafi wa nyumba, n.k.

Unakuta binti wazazi wake hawakumfundisha wala kumzoesha shughuli za kupika, matokeo yake huku kwenye ndoa anazidisha chumvi, wali boko, ugali mbichi, n.k. vinaanza kuwa kero, na hata kama anajua kupika anakuwa hana mazoea, anapika kwa kujivuta vuta sana, badala ya kujiongeza asubuhi amuandalie mme wake hata viazi vya kuchemsha yeye anaweka mkate tu, siku ya jumapili mmepumzika myumbani yeye wala hajishughulishi kupika anasonga ugali na mchicha wakati stoo kuna mchele wa kutosha, friji kuna nyama ya kutosha, yani anaona kupika pilau ni kazi nzito sana, Mwanaume anaanza kumuona mzigo tu.

Kufua nguo za mmewe wala hana muda anampa huse girl sababu huko kwao nae alikuwa anafuliwa ama hakuzoeshwa, ni mambo yanayotia aibu maana huu sio uafrika wetu, haijalishi hata kama mwanamke ana cheo kizito ni lazima amfulie mme wake nguo zake hizo ndio mila zetu waafrika tangu na tangu,
Upuuzi was kuwapeleka shule za Bweni kuanzia darasa la kwanza Hadi form six !unakuta hajui hata kufua vizuri na kila kitu akifanyiwa eti yeye ni kusoma tu!

Akija likizo Kuna dada wa kazi nyumbani ndio kazi inaanza akiolewa!!
 
Bado unaishi kwenye ulimwengu wa kukuna nazi na kupasha moto maji ya kuoga.

We have heaters for that, unafungua bomba hata dakika haifiki maji yashashika moto.

Ndiyo maana tangu awali nilisema hatuwezi kuelewana.

Tunaishi dunia mbili tofauti kabisa na sioni hata haja ya kuendeleza mazungumzo haya na wewe.
Mkuu huku Bado ,mume anapashiwa maji ya kuoga na kupelekewa bafuni🤣
 
Mkuu huku Bado ,mume anapasjiwa maji ya kuoga na kupelekewa bafuni🤣
Ndiyo maana nimekubali tu kuwa kuna watu mambo fulani kuelewana ni vigumu.

Unabishana vipi na mtu ambaye unaona kabisa mna tofauti kubwa sana ya upeo, kisha ana kiburi cha kutojifunza cha kiutamaduni?

Si bora nianze kumfundisha sisimizi string theory na quantum physics, labda ataweza kurukaruka ki quantum physics aelewe somo 🤣🤣🤣
 
Yuko sahihi wewe ndie unakuwa umekosea kuoa ungeenda kuoa kijijini kwenu.Umezaliwa porini unakomaa kuoa mtoto wa mjini ambaye maisha yake yote kazi zote zinafaywa na Houseboy na House girl ikiwemo kufua nguo zake

Ungeoa saizi Yako mliyekua naye huko maporini vijijini kwenu usingekuwa na haya malalamiko


Kaajiri house boy na house girl wafanye hizo kazi
Makosa Yako fua mwenyewe na yeye atafua zake.Tena kajitahidi kama unaona Hadi nguo zake anafua kakuvumilia sana kwao hajazoea Hilo.Kutoongeza kesi fua mwenyewe nguo zako.

Kosa lako Kwa kutooa huko porini kwenu
Aiseee nimecheka 🙌🤣🤣🤣
Mshauri anunue mashine ya kufulia
 
Akiolewa kinabadilika nini? Si atakuwa na dada pia...
Anatakiwa anipikie kwanza nione utamu was chakula jinsi unavosadifu utamu wa papuchi!we hujui!utam wa pishi la ke ndio utam wa ikulu!!?

Ndio maana ukija geto upike kwanza nile!halafu ndio tunakulana!
 
Anatakiwa anipikie kwanza nione utamu was chakula jinsi unavosadifu utamu wa papuchi!we hujui!utam wa pishi la ke ndio utam wa ikulu!!?

Ndio maana ukija geto upike kwanza nile!halafu ndio tunakulana!
Hao hao mnaowapata. Sisi tutakutana restaurant au tuagize chakula na sio kwamba hatujui kupika ila hatupikii mtu hadi tujisikie.
 
Hao hao mnaowapata. Sisi tutakutana restaurant au tuagize chakula na sio kwamba hatujui kupika ila hatupikii mtu hadi tujisikie.
Usijali tutakutana restaurant halafu utapika humo humo!kupika ninsehem ya package kwenye mahaba!!!Am so demanding!
 
Sawa mkuu naona wewe endelea huko nyumbani kwako uwe unamfulia mke wako nguo, uwe unampikia mke wako, uwe unapiga deki, uwe unampokeza kupika kwenye misiba yeye awe anaenda na wanaume kuchimba kaburi, pia wezi wakija liwe jukumu lake kukulinda wewe.
Bush Dokta kampatia jibu zuri sana lakini bado tu kashupaza shingo, haelewi hata kwanini asili kiuumbwaji ya Me wana nguvu (pumzi) sana kuliko Ke?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni jamii ya kiafrika na Mwanamke lazima ajue kupika na mila na desturi lazima zizingatiwe. mambo ya Gender roles na bla bla za usawa hao wenye nazo wenyewe kila siku talaka na balaa zingine kama hawana akili nzuri.
Kiujumla Kizazi chetu cha karne ya 21 kinatengeneza/kimeshatengeneza bomu linalolipuka kwa kasi sana ndiyomaana unaona Ke walioshupaza shingo kwa kiburi cha Haki Sawa sababu wana elimu ya juu, kazi nzuri kimaslahi wametokea kwenye familia zenye hadhi flani kimaisha huishia kuzalishwa tu bila ya kuolewa na hata wakiolewa ndoa huvunjika kirahisi sana.

Africa ndipo penye unafuu wa mahusiano ya kudumu katika ndoa kuliko nchi za magharibi palipoasisiwa haki Sawa na kuvuna ndoa za mikataba kila siku.

Angalia hata matokeo ya Watoto wa leo hii kuwa pasua kichwa ni tokana na ubovu wa malezi kwa kuiga life styles za western countries.

Me & Ke wanaenda kazini wote tangu asubuhi hadi jioni wanawaachia Watoto wadogo house maids, mwishowe Watoto huwapenda zaidi House maids kuliko Wazazi na hutegemea tabia nzuri ya hao housemaids la sivyo ndiyo matokeo ya hawa panya roads au Watoto kulelewa na single mothers pekee.

Cha ajabu zaidi mchango wa Ke katika familia haupo hata kwa 30% kifedha ilihali ndiyo hung'ang'ana na nyimbo za haki sawa kwa Me na Ke katika ndoa kwa kila jambo ila si inshu za fedha, kama si changa la macho hili ni nini?

Me tunapooa tunagalie historical background za Wazazi wa Wachumba/Wake zetu kabla ya kujikita katika ndoa la sivyo tutaendelea kuzaa kizazi cha balaa miaka mitano hadi 10 ijayo TZ na Africa nzima.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
mchango wa Ke katika familia haupo hata kwa 30% kifedha ilihali ndiyo hung'ang'ana na nyimbo za haki sawa kwa Me
Hapooo ndipo umegonga penyewe.

Kipato cha mwanamke huwa mara nyingi kinaishia kwao ama mambo yake binafsi, wewe ukipata kipato cha milioni na yeye apate milioni, bajeti inatumika milioni yako
 
Aiseee nimecheka 🙌🤣🤣🤣
Mshauri anunue mashine ya kufulia
Hawa wengine hata akiwa na mashine ya kufulia bado atataka nguo zifuliwe na mkewe.

Atakwambia za kufuliwa na mke zina utamu wake 🤣🤣🤣
 
Binti yangu nahakikisha anajiwrka dunia ya mbele. Namfundisha namna ya kuwa na followers wengi kwenye social media na faida zake. Hayo mambo ya ujima eti mtoto sijui ajue kupika, kufua wafundisheni watoto wenu. Sisi tunasonga mbele.
Hahahaha...chekesha mie
 
Kwahiyo mimi jukumu langu liwe la mara tatu kwa siku, wewe lako iwe ni pale ENDAPO wezi watavamia?
Na Kuna sisi familia zingine hatuvamiwi na wezi it means yeye kama baba Hana Cha kufanya
 
Wakati nipo nyumbani tulikua na house girl kipindi chote nakua but kazi za nyumbani tulikua tunafanya almost sawa Yani kuamka wote tunaamka asubuhi kasoro weekend kazi tunafanya wote kupika lazima tupike wote nlikua namkasirikia mama sana kwanini ananifanyisha kaz wakat Kuna house girl ila nlivyoanza kujitegemea nilikuja kumshukuru sana Nina experience ya kazi za nyumbani jinsi ya kupangilia nyumba yangu na kaz hazinisumbui kabisa hata nilivyoolewa naweza kusimamia nyumba vzuri
 
Huu uzi una tatizo la gender roles.

Yani, kuweka kazi ya kupika kuwa ni kazi ya watoto wa kike.

Hii ni tabia ya jamii zenye mfumodume.

Inatakiwa watoto wote wajue kazi zote.

Kujua kupika, kuosha vyombo, kufua ni life skills ambazo hata mtoto wa kiume anatakiwa kuzijua, akiwa peke yake aweze kufanya hizo kazi. Na hata akioa, aweze kusaidiana na mkewe. Kuna uzi nimeuona jana, mtu anasema anamsaidia mke wake kwa sababu anaona mke wake anachoka sana. Sasa, utamsaidiaje mkeo kupika ikiwa mwanamme hujui kupika?

Ila, jamii yetu bado iko nyuma, imefanya kupika, kufua, ni kazi ya mwanamke.

Ndiyo maana hata uzi huu una assume automatically kuwa mwanamke/ mtoto wa kike ndiye anatakiwa kujua vitu hivi, mwanamme ni mtu wa kuhudumiwa tu.

Mfumodume. Dunia fulani ya umasikini wa mawazo.

Najua kwa mfumodume wetu, inawezekana wengi hawataelewa somo.
Ni kweli lakin kwa asilimia kubwa duniani kuosha vyombo kupika ni kazi za mke mwanaume anaweza kufanya kukusaidia tu lakin sio kwamba ndo kazi zake kwasababu yeye ana hudumia familia kifedha ndo majukumu yake kwenye ndoa kila mtu akikaa kufanya majukumu yake Wala hamtasumbuana
 
Haina shida tunawasomesha kwajili ya kazi za ofisini kazi za nyumban siku hizi sio muhimu sana sababu hawaolewi
 
Huu uzi una tatizo la gender roles.

Yani, kuweka kazi ya kupika kuwa ni kazi ya watoto wa kike.

Hii ni tabia ya jamii zenye mfumodume.

Inatakiwa watoto wote wajue kazi zote.

Kujua kupika, kuosha vyombo, kufua ni life skills ambazo hata mtoto wa kiume anatakiwa kuzijua, akiwa peke yake aweze kufanya hizo kazi. Na hata akioa, aweze kusaidiana na mkewe. Kuna uzi nimeuona jana, mtu anasema anamsaidia mke wake kwa sababu anaona mke wake anachoka sana. Sasa, utamsaidiaje mkeo kupika ikiwa mwanamme hujui kupika?

Ila, jamii yetu bado iko nyuma, imefanya kupika, kufua, ni kazi ya mwanamke.

Ndiyo maana hata uzi huu una assume automatically kuwa mwanamke/ mtoto wa kike ndiye anatakiwa kujua vitu hivi, mwanamme ni mtu wa kuhudumiwa tu.

Mfumodume. Dunia fulani ya umasikini wa mawazo.

Najua kwa mfumodume wetu, inawezekana wengi hawataelewa somo.
Sasa nawe...kwa huyo gender roles ni tatizo 😀
 
Back
Top Bottom