Mnaowalea watoto wa kike bila kuwafundisha kazi za nyumbani mnawaandalia mazingira gani wakiwa wakubwa?

Mnaowalea watoto wa kike bila kuwafundisha kazi za nyumbani mnawaandalia mazingira gani wakiwa wakubwa?

Wa
Mfumo dumo uko dunia nzima na hakuna namna utaisha

Kibaya ni Mfumo Dume wenye dhamila mbovu ndio unapigwa vita

Kiranga nakuuliza swali unijibu hapa.

Tazama movie na miziki ya aina yoyote duniani........utakuta Mwanamke Character yuko Uchi ila kokote Mwanaume kavaa na kujistiri.

Huo ndio mfumo dume mbaya kupita yote.

Marekani kwenye mfumo unaodhaniwa ni Huru kwa Rika zote wana zaidi ya miaka 300 mpaka leo hakuna Rais Mwanamke.

Hata vyeo vya juu vya serikali wanawake ni wachache sana.

Sio kwamba hawana uwezo.

Tuna wanawake wengi wenye akili sana tu kuzidi Wanaume.

Tatizo ni vile mnatazama mfumo dume kama uadui na mnautumia vibaya.
Wanawake by nature are not suposed to lead....ni ubunifu tu na "maendeleo" .
 
Halafu hao watoto wasiojua kupika wazazi wao wana mahari makubwa ile mbaya.
 
Kuna gender roles za kabla ya ndoa na baada ya ndoa.

Wanaume mabachela hupika, hujifulia, hufanya usafi wa jikoni, n.k. lakini mambo haya inabidi yawe majukumu ya mwanamke baada ya ndoa, ndio maana kuna msemo maarufu wa kuoa kufananishwa na "kuvuta jiko".
Mkuu uzi ushavamiwa n wana harakati tayari wanatetea mwanamke kutokujua kupika na kufua tuna safari ndefu.
 
"Mkuu unataka Mke au mfanyakazi wa ndani", alisikika Feminist mmoja akiongea maneno hayo kwa ukali.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Ni kweli lakin kwa asilimia kubwa duniani kuosha vyombo kupika ni kazi za mke mwanaume anaweza kufanya kukusaidia tu lakin sio kwamba ndo kazi zake kwasababu yeye ana hudumia familia kifedha ndo majukumu yake kwenye ndoa kila mtu akikaa kufanya majukumu yake Wala hamtasumbuana
Ikiwa mimi ndiye niliyeanzisha JF, nikaweka sheria ya kusema wewe unaweza kuchangia uzi huu tu. Utaona uamuzi huo ni wa haki na sawa kwa sababu umeukuta tu?

Let me point ou the logical fallacies here. You can Google them to expand horinzs.

Umeandika "Kwa asilimia kubwa" = argument from populism. Asilimia kubwa haimaanishi kuwa kitu ni kizuri au cha kweli. Asilimia kubwa ya watu wanaweza kukubali kiti ambacho ni potofu na kibaya. Ukisoma historia ya sayansi utaona hili.

Habari nzima kwamba mwanamme anahudumia famulia kigedha ni construct, hakuna sababu yoyoye ya msingi ambayo iyaondoa nafasi sawa za wanawake na wanume kuhudumia familia.

Unakubali?
 
Tafuta mtu amfundishe pia huyo sio mfanyakazi wako ujue achen mfumo dume
 
Unarudi kulekule kwenye dunia ya kijima ya gender roles kwamba kazi ya kupika ni ya mwanamke.

Wakati tunaishi kwenye dunia ambayo ina wanawake wameolewa na professional chefs.
Kwani we jamaa unatafuta Nini kwenye huu uzi!
Sisi wanaume halisi tumemuelewa!

Wewe uliyelelewa na kwa misingi ya jikoni tangu ukiwa mdogo, pita pembeni!

Mfumo dume ulianzishwa na Muumbaji wa dunia hii

Mwanaume Ni mtafutaji,
Mke Ni mtunza nyumba

Wewe na wenzio munaotaka usawa wa kijinsia, tengenezeni dunia yenu, naona munapigania kutuharibia dunia yetu!

Mungu akiona ipo haja ya kuweka usawa wa kijinsia kwa wanadamu hatashindwa, utashuhudia watu wanazaliwa na jinsia zote mbili!

Ushauri wa bure kwako,
Mpe skills za majukumu ya ndani ya nyumba mwanao wa kike,
Na umwaambie kwa hakika akatumie skills hizo ipasavyo kwenye nyumba yake kwa faida ya ndoa yake
Kamwe usimfundishe mwanao wa kike kuwa hizo shughuli zinapaswa kushare na mumewe kwa ajili ya usawa wa kijinsia!
Mustakabali wa maisha ya binti yako hauyajui!

Shame on you female Man!
 
Hii ni ooen forum, huelewi hilo?

Hiyo unayemuita muumbaji huwezi kuthibitisha yupo, unatumia uongo kwamba yupo ili kutimiza haja zakonza kunyanyasa wanawake tu.

Kama unabisha, thibitisha huyo muumbaji yupo.

Umesha assume sana hapo juu, kijinga tu.
 
Hapo umeshakubali kwamba kwenye ndoa kuna gender roles na kupika ni kazi ya mwanamke kwenye ndoa.

Huo ndio mfumodume wenyewe.

Ndiyo maana nikasema kwa nfumo huu ni vigumu kunielewa.

Wewe unafuata mfumo wa kizamani, baba anafanya kazi, mama mke wa nyumbani.

Siku hizi wanawake wanasoma. Inawezekana baba na mama wote wanafanya kazi, kazi za nyumbani wakasaidiana pia.

Sasa happ ukileta mambo ya gender roles kwamba mama ni mpishi wakati mama naye ni mfanyakazi, unaweza kuwa unamuonea huyo mama.

Kwa sababu na yeye anafanya kazi ofisini kama baba na anarudi kachoka. Msingi wa mama kuwa mpishi kwa kiasi kikubwa ulitokana na mama kuwa mama wa nyumbani.

Msingi huu unatoweka kwa kasi katika dunia ambayo mama naye anafanya kazi ofisini.

Ila, naelewa inawezekana hunielewi kwa sababu ya mfumodume uliokithiri huko kwenye jamii zetu.

Kuna uzi nimeuona jana mtu anasema "anamsaidia" mkewe kazi za nyumbani kwa sababu anaona mkewe anachoka sana.

Sasa kama mkeo anafanya kazi ofisini halafu nyumbani anapika, mume hajui kupika, ikitokea kuna haja mke "asaidiwe" ( neno si sahihi, kwa sababu limefanya kazi ya kupika kuwa ya mke) mume atafanyaje hapo?

Bottom line, hizo gender roles ni za ulimwengu uliopita. Watoto wote wanatakiwa kujua kazi zote na kusaidiana, hata wakikua na kuwa ndani ya ndoa.

Ila naelewa ni somo gumu bado kwa jamii zetu.
Na hii ndo inatakiwa. Watoto wote wafundishwe kazi zote bila kujali jinsia. Japo mimi kama mama kuna wakati najisahau namfundisha sana huyu wa kike mvulana namsahau. Kwa mbaaali bado naona mfumo dume umeniathiri.
 
Huu mfumodume hatuwezi kuumaliza mara moja.

Kitu ambacho wanaume wengi hawajui ni ukweli kwamba mfumodume unawaathiri wao wenyewe pia.

Unakuwa na mtoto wa kiume, hafundishwi kupika. Siku akianza kujitegemea hawezi kujipikia mwenyewe. Anakuwa tegemezi. Kula mpaka apikiwe.

Mtu inafikia mpaka anakuwa na mwanamke kwa lazima si kwa sababu anampenda, bali kwa sababu anataka mtu wa kumpikia tu. Anataka "jiko".

Mfumodume unaathiri sana wanaume, ila ni vigumu kujua kwa sababu wengi sana wameuzoea.
 
Kumuandaa mtoto wako wa kike kujua kuishi kwenye ndoa za kiafrika ni jukumu ambalo wazazi hasa mama hapaswi kulilazia damu,
Ni utaahira kumuandaa mtoto kuwa mke ktk maisha ya leo. Yaani unamuandaa mtoto wako aje kuwa mtwana na mtumwa wa mtu (mume)? Kwamba huyo mwanaume atakuwa hana mikono na miguu?? Why mtoto wa kike??
 
Ni utaahira kumuandaa mtoto kuwa mke ktk maisha ya leo. Yaani unamuandaa mtoto wako aje kuwa mtwana na mtumwa wa mtu (mume)? Kwamba huyo mwanaume atakuwa hana mikono na miguu?? Why mtoto wa kike??
Acha ujinga
Mungu ndiye aliyemuandaa mtoto wa kike kuwa mke?
Hivi inakuwaje munastruggle kupambana na Nature?
 
Huu mfumodume hatuwezi kuumaliza mara moja.

Kitu ambacho wanaume wengi hawajui ni ukweli kwamba mfumodume unawaathiri wao wenyewe pia.

Unakuwa na mtoto wa kiume, hafundishwi kupika. Siku akianza kujitegemea hawezi kujipikia mwenyewe. Anakuwa tegemezi. Kula mpaka apikiwe.

Mtu inafikia mpaka anakuwa na mwanamke kwa lazima si kwa sababu anampenda, bali kwa sababu anataka mtu wa kumpikia tu. Anataka "jiko".

Mfumodume unaathiri sana wanaume, ila ni vigumu kujua kwa sababu wengi sana wameuzoea.
Huoni kuwa ni vema watu kuoana?
Inakurahisha Nini mwanaume asioe kisa anajua kujiandalia chakula kitamu

Kama kwa waume kutojua kupika ni sababu ya wao kuchukua binti na kuoa haraka, basi ni Jambo jema saaanaaaa!
 
Kwani wapi nimesema si vema watu kuoa au kuolewa?

Kuoa mtu anatakiwa kuoa kwa mapenzi, si kuoa kwa sababu ya kutafuta mtu wa kumpikia. Umeelewa hilo somo?
 
Kujua kupika, kuosha vyombo, kufua ni life skills ambazo hata mtoto wa kiume anatakiwa kuzijua, akiwa peke yake aweze kufanya hizo kazi. Na hata akioa, aweze kusaidiana na mkewe. Kuna uzi nimeuona jana, mtu anasema anamsaidia mke wake kwa sababu anaona mke wake anachoka sana. Sasa, utamsaidiaje mkeo kupika ikiwa mwanamme hujui kupika?

Ila, jamii yetu bado iko nyuma, imefanya kupika, kufua, ni kazi ya mwanamke.
Yaani kwa maelezo yako bado unakubaliana na mleta mada kuwa mwanamke yeye ndio mwenye majukumu ya jikoni. Mwanaume kiubinadamu na kwa uhitaji unapaswa kujua kupika ili kutoa usaidizi tu.
 
Back
Top Bottom