Killa Cam
JF-Expert Member
- Jun 12, 2022
- 2,264
- 6,679
Kuna siku nilitoka na mwana baada ya mizungugo akataka tukajaze nguvu. Aliagiza nami nikaagiza changu ila changu bei zaidi ya chake. Mwana akatoa macho nikaongeza na supu ya kuku nikamuona mwamba kama kapanic nikacheka moyoni. Niliagiza juice 2 kila moja bei yake 4,500 zile juice unatengezewa hapohapo. Mwana nikamuona hayupo happy tena hata Maongezi kakata kabisa. Alikuja waitress na receipt nikachukuwa nikalipia. Mwana alibaki kushangaa tu na uso wake hapo ukaanza kuonesha furaha. Mimi sipendi kulipiwa kula nalipia mwenyewe mara nyingi kuna marafiki wana simbulia sana baada ya kukupa ofa yao.Ukiamua kukaa na mimi mahali asee nisipangiwe cha kutumia. Uzuri mimi huwa nabeba muamala wangu incase hauko poa nalipa..na pia huwa nakuuliza kama uko njema au uko vibaya nimalize shoo...