Mnapopewa ofa muwe mnaanza kujitathimini

Mnapopewa ofa muwe mnaanza kujitathimini

Ukiamua kukaa na mimi mahali asee nisipangiwe cha kutumia. Uzuri mimi huwa nabeba muamala wangu incase hauko poa nalipa..na pia huwa nakuuliza kama uko njema au uko vibaya nimalize shoo...
Kuna siku nilitoka na mwana baada ya mizungugo akataka tukajaze nguvu. Aliagiza nami nikaagiza changu ila changu bei zaidi ya chake. Mwana akatoa macho nikaongeza na supu ya kuku nikamuona mwamba kama kapanic nikacheka moyoni. Niliagiza juice 2 kila moja bei yake 4,500 zile juice unatengezewa hapohapo. Mwana nikamuona hayupo happy tena hata Maongezi kakata kabisa. Alikuja waitress na receipt nikachukuwa nikalipia. Mwana alibaki kushangaa tu na uso wake hapo ukaanza kuonesha furaha. Mimi sipendi kulipiwa kula nalipia mwenyewe mara nyingi kuna marafiki wana simbulia sana baada ya kukupa ofa yao.
 
Sina vanguard yoyote
Nshamiliki ki rav4 cha 2008 nkampa dingi.

Kutanua ni maamuzi tu... hela unatafuta halafu huzitumii uje ufe wazigombanie.

Nikiwa na ishu muhimu natumia bolt
Ndo nataka njichange ntafute ki ist kirahisishe mishe.

Ahahaha dada una upiga mwingi
 
I can control myself ila kuna mahal hata mm nasema leo nguruwe njoo mkuki upo [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Muwe mnaangalia huyu mtu kajitutumua vipi. Hata mimi nikienda kwa mtu nafata alivyo kama hakinipa huakika ndio na jiachia.
 
Mademu wengi hawaju kabisa protocol,wao nikukomoa tu! Agiza kitu ambacho mtoa offer awe na uwezo nacho! Mimi nakula kande,wewe unaagiza biriani mandi la ngamia!

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom