Mnapotengana mnawapa mzigo mzito watoto sio tu wakiwa wadogo bali hata wakiwa watu wazima

Uwaambie watoto wawe makini Kwa uchaguzi ili kuepusha hayo unayoyasema,

Jitu linaendekeza tamaa ya pesa alafu huko mbeleni likikutwa na madhila Kwa nini lisitumikie maamuzi yake mabovu.

Jitu linahadaiwa na umbile la nje la Mwanaume au mwanamke linasahau tabia alafu unategemea nini.

Tafuta wakufanana naye mlee watoto kwenye misingi ya ndoa na uadilifu.
 
Wanaoomba riziki zikate ili yamkini mtulie ndio usiseme!

Tena mwanamke mwingine hakusemeshi lakini nyendo zako anazijua zote!

Kitendo cha kila wakati uko Simu yako roho haikutulii tayari ni kwamba uko na mahusiano mengine!

Kuna aliyekutuma uchagua nyoka ndani ya nyumba ili awe mumeo?
Si uliamua mwenyewe? Sasa acha uendelee na maombi ya kipumbavu ambayo ni Dua la kuku
 
Wazungu huwa nawakubali sababu mambo mengi huwa wanaanza kwa kufanya utafiti wa kisayansi kabla ya kuamua jambo kufanyika Kwa utaratibu fulani.

Unapoona takwimu za talaka kwao kuwa juu ni kwamba wanajua inawaepusha na mengi.

Mambo ya kuvumiliana kuishi Kwa sononi kuathiri afya nani ana yataka?!
 
Kuna aliyekutuma uchagua nyoka ndani ya nyumba ili awe mumeo?
Si uliamua mwenyewe? Sasa acha uendelee na maombi ya kipumbavu ambayo ni Dua la kuku

Mwenzio nilizani najadiliana na mtu ambae he is psychologically matured enough lakini kumbe sio [emoji15]

Sasa badala ya kujadili mada Kwa kutumia nafsi ya 3 umeanza kuni -attack personally mimi tena? [emoji15]

Huwa nikitambua hivyo basi naku-ignore !

Nilitaka kunogesha uzi / mada yako Kwa kufunguka facts za yanayoendelea kwenye jamii lakini nasikitika sababu ku-fix a fool is very difficult job!
 
Kwenye suala la mahusiano Wazungu wanapati Sifuri kabisa,
Mahusiano ya ndoa Wazungu hawana wajualo, ni washamba wa mwisho kabisa.

Kama HAO ndio Role model wako umekwisha,
Wazungu ni Wataalamu WA mambo mengine Kama Teknolojia, Elimu, n.k.

Lakini ishu za mahusiano ya ndoa Wana F kubwa tangu zamani, ndio maana ushoga, usagaji, kulala na wanyama, na mambo ya hovyo yapo kwao.

Kila jamii ina Jambo ambalo wanaliweza Kwa kiwango cha juu.
 
😀😀

Sasa wewe Kwenye huu mjadala si ndio muwakilishi wao, hivyo ninapokutaja wewe moja Kwa moja nagusa wafuasi WA mrengo wako.

Wewe ni sampo tuu Mkuu, huu ni mjadala na kila mjadala unawawakilishi,
Wewe umeamua kwenye mjadala huu kuwa mwakilishi wa kuona umuhimu wa talaka.

Na anayewasilisha hoja ni wewe Kwa niaba ya hao unaowasemea, na Mimi nakujibu wewe uliyetoa hizo hoja Kwa niaba ya hao waliopo kwenye jamii.
 
Watoto wako ni matokeo yako Kwa Asilimia kubwa.
Nyoka hawezi kuzaa Jongoo.
Mtoto wako ni mke au mme wa mtu.Hatuishi na watoto milele majumbani pale wapo chuoni kuelekea maisha yao ya mbeleni, so mzazi ndie uamua hatma ya ndoa ya mwanae kutokana na aina ya malezi ampayo.
 
Mtoto wako ni mke au mme wa mtu.Hatuishi na watoto milele majumbani pale wapo chuoni kuelekea maisha yao ya mbeleni, so mzazi ndie uamua hatma ya ndoa ya mwanae kutokana na aina ya malezi ampayo.

Naam Mkuu
 
Ndoa ndio chanzo cha familia na familia uzaa taifa. Taifa la hovyo ujengwa na familia za hovyo, ufisadi, ubinafsi, uvivu, upigaji, ukosefu wa uongozi bora, ukosefu wa utu na uzalendo chanzo ni familia. Familia bora uzaa taifa bora.
 
Uko deep sana mdau. Big up!!
 
Mzee wa fasihi huu uzi wako yafaa ujengewe mnara na pili ufundishwe kwenye taasisi zote zinashughulika na mahusiano mfano nyumba za ibada nk. Kutengana ni ubinafsi na ni karma
 
Ndoa ndio chanzo cha familia na familia uzaa taifa. Taifa la hovyo ujengwa na familia za hovyo, ufisadi, ubinafsi, uvivu, upigaji, ukosefu wa uongozi bora, ukosefu wa utu na uzalendo chanzo ni familia. Familia bora uzaa taifa bora.

Huko tuendako ndio kubovu kabisa
 
😂Kwamba midomo Hadi watu wanatamni wahame nyumba walizojenga wenyew
 
Hakuna kitu kinamuumiza shetani kama ndoa , thus ufanya makubwa Sana kuzibomoa kwa maana walengwa wakuu ni watoto Ili wakose muongozo kisha shetani achukue nafsi zao Ili awatumie kwenye ushoga, uteja, ukahaba, ukibaka, nk ambayo mwisho wake ni kifo cha mapema tena cha hasara duniani na kesho ahera. Lengo kuu la talaka ni Ili watoto waharibike, so mkilazimika kutengana muhimu Sana msiache kuwaombea watoto wenu ikiwemo kuwawekea kinga za kiroho Ili wasiuze nafsi zao kwa shetani.
 
Mtoto wako ni mke au mme wa mtu.Hatuishi na watoto milele majumbani pale wapo chuoni kuelekea maisha yao ya mbeleni, so mzazi ndie uamua hatma ya ndoa ya mwanae kutokana na aina ya malezi ampayo.
Hapa wazazi unawaonea kunawatoto ni pasua kichwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…