Mnapotengana mnawapa mzigo mzito watoto sio tu wakiwa wadogo bali hata wakiwa watu wazima

Mnapotengana mnawapa mzigo mzito watoto sio tu wakiwa wadogo bali hata wakiwa watu wazima

Imagine kuna wanawake sana wako kwenye ndoa wanamuomba Mungu awachukue wanaume wao wa ndoa [emoji24]

Yani mke anakuwa ametendwa na kuumizwa moyo na mumewe , amemuonya hasikii kwa miaka nenda rudi imekuwa ni mfumo wa maisha alochagua wa kuishi kimalaya!

Kwenye seminar za Neno la Mungu wachungaji wanakutana na mengi wakati wa canceling na maombezi,

Aliwahi sema Mchungaji Mwakasege kuwa inashangaza kuona kuna wanawake wanasema kabisa wamekuwa wakimuomba Mungu awachukue waume zao [emoji24]

Kwa hiyo nyie neng’enekeni tu huku mkijifanya vitombiii!


Uwaambie watoto wawe makini Kwa uchaguzi ili kuepusha hayo unayoyasema,

Jitu linaendekeza tamaa ya pesa alafu huko mbeleni likikutwa na madhila Kwa nini lisitumikie maamuzi yake mabovu.

Jitu linahadaiwa na umbile la nje la Mwanaume au mwanamke linasahau tabia alafu unategemea nini.

Tafuta wakufanana naye mlee watoto kwenye misingi ya ndoa na uadilifu.
 
Wanaoomba riziki zikate ili yamkini mtulie ndio usiseme!

Tena mwanamke mwingine hakusemeshi lakini nyendo zako anazijua zote!

Kitendo cha kila wakati uko Simu yako roho haikutulii tayari ni kwamba uko na mahusiano mengine!

Kuna aliyekutuma uchagua nyoka ndani ya nyumba ili awe mumeo?
Si uliamua mwenyewe? Sasa acha uendelee na maombi ya kipumbavu ambayo ni Dua la kuku
 
Wazungu huwa nawakubali sababu mambo mengi huwa wanaanza kwa kufanya utafiti wa kisayansi kabla ya kuamua jambo kufanyika Kwa utaratibu fulani.

Unapoona takwimu za talaka kwao kuwa juu ni kwamba wanajua inawaepusha na mengi.

Mambo ya kuvumiliana kuishi Kwa sononi kuathiri afya nani ana yataka?!
 
Kuna aliyekutuma uchagua nyoka ndani ya nyumba ili awe mumeo?
Si uliamua mwenyewe? Sasa acha uendelee na maombi ya kipumbavu ambayo ni Dua la kuku



Mwenzio nilizani najadiliana na mtu ambae he is psychologically matured enough lakini kumbe sio [emoji15]

Sasa badala ya kujadili mada Kwa kutumia nafsi ya 3 umeanza kuni -attack personally mimi tena? [emoji15]

Huwa nikitambua hivyo basi naku-ignore !

Nilitaka kunogesha uzi / mada yako Kwa kufunguka facts za yanayoendelea kwenye jamii lakini nasikitika sababu ku-fix a fool is very difficult job!
 
Wazungu huwa nawakubali sababu mambo mengi huwa wanaanza kwa kufanya utafiti wa kisayansi kabla ya kuamua jambo kufanyika Kwa utaratibu fulani.

Unapoona takwimu za talaka kwao kuwa juu ni kwamba wanajua inawaepusha na mengi.

Mambo ya kuvumiliana kuishi Kwa sononi kuathiri afya nani ana yataka?!

Kwenye suala la mahusiano Wazungu wanapati Sifuri kabisa,
Mahusiano ya ndoa Wazungu hawana wajualo, ni washamba wa mwisho kabisa.

Kama HAO ndio Role model wako umekwisha,
Wazungu ni Wataalamu WA mambo mengine Kama Teknolojia, Elimu, n.k.

Lakini ishu za mahusiano ya ndoa Wana F kubwa tangu zamani, ndio maana ushoga, usagaji, kulala na wanyama, na mambo ya hovyo yapo kwao.

Kila jamii ina Jambo ambalo wanaliweza Kwa kiwango cha juu.
 
Mwenzio nilizani najadiliana na mtu ambae he is psychologically matured enough lakini me kumbe sio [emoji15]

Sasa badala ya kujadili mada Kwa kutumia nafsi ya 3 umeanza kuni -attack personally tena? [emoji15]

Huwa nikitambua hivyo basi naku-ignore !

Nilitaka kunogesha uzi mada yako Kwa kufunguka facts za yanayoendelea kwenye jamii lakini nasikitika sababu ku-fix a fool is very difficult job!

😀😀

Sasa wewe Kwenye huu mjadala si ndio muwakilishi wao, hivyo ninapokutaja wewe moja Kwa moja nagusa wafuasi WA mrengo wako.

Wewe ni sampo tuu Mkuu, huu ni mjadala na kila mjadala unawawakilishi,
Wewe umeamua kwenye mjadala huu kuwa mwakilishi wa kuona umuhimu wa talaka.

Na anayewasilisha hoja ni wewe Kwa niaba ya hao unaowasemea, na Mimi nakujibu wewe uliyetoa hizo hoja Kwa niaba ya hao waliopo kwenye jamii.
 
Watoto wako ni matokeo yako Kwa Asilimia kubwa.
Nyoka hawezi kuzaa Jongoo.
Mtoto wako ni mke au mme wa mtu.Hatuishi na watoto milele majumbani pale wapo chuoni kuelekea maisha yao ya mbeleni, so mzazi ndie uamua hatma ya ndoa ya mwanae kutokana na aina ya malezi ampayo.
 
Ndoa ndio chanzo cha familia na familia uzaa taifa. Taifa la hovyo ujengwa na familia za hovyo, ufisadi, ubinafsi, uvivu, upigaji, ukosefu wa uongozi bora, ukosefu wa utu na uzalendo chanzo ni familia. Familia bora uzaa taifa bora.
 
Kwema Wakuu!

Huenda ukawa unajiuliza ni Kwa nini Taikon anapenda kujadili masuala ya familia, ndoa, na wanawake. Kwa kifupi tuu ni kuwa Msingi Mkuu wa Jamii ni Familia Bora, familia Bora ni matokeo ya ndoa iliyofuata misingi ya uadilifu. Familia Bora huleta jamii Bora, jamii Bora huzaa taifa Bora.

Sitochoka kugusia mambo haya ningalipo katika mgongo wa Dunia.

Umoja baina ya Baba na Mama huleta Umoja Kwa watoto. Kama Baba na Mama sio wamoja na kila mtu anafuata ubinafsi basi ni wazi hata familia hiyo watoto watakuwa hawana mbele wala nyuma.

Umoja ndani ya ndoa unaletwa zaidi na UPENDO WA dhati wenye msingi ya kimaadili. Upendo wa wanandoa usiofuata maadili huleta machafuko ndani ya Familia.

Taikon ninaamini zaidi katika Upendo. Ninaamini palipo na upendo wa kweli basi hapo usalama upo.

Wanaosema Ndoa haina umuhimu wengi wao ni kutokana na kukata tamaa na kuanguka katika kizazi Chao.

Watu wote wenye akili huchukulia familia Kama Jambo kubwa la maana.

Suala la Talaka haliwezi kupewa kipaombele mahali popote Kwa watu wenye Uelewa mkubwa na wenye malengo ya umilele.

Kutengana na kuachana huathiri watoto kivyovyote na Kwa miaka yote.

ATHARI KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 18
1. Watoto hukosa malezi ya Msingi kutoka Kwa wazazi wao wenyewe.

2. Watoto kuathirika kisaikolojia na kuwa na roho ya utengano tangu wakiwa wadogo.

3. Watoto kuathirika vibaya kiuchumi Kwa kukosa huduma zilizobora kutoka Kwa wazazi kutokana na Migogoro ya wazazi.

4. Watoto kuanza kujenga chuki ya ndani kabisa kutokana na kukosa malezi na Huduma kutoka Kwa wazazi.

5. Watoto kukosa roho ya kujali na kuwa Wabinafsi kulikochangiwa na ubinafsi wa wazazi wao. Sababu nyingi za utengano katika ndoa ni matokeo ya Ubinafsi uliopitiliza.

6. Watoto kukosa mwelekeo wa maisha na kukosa Sapoti ya wazazi kutokana na kutengana Kwa wazazi.

7. Watoto kukukosa Uhuru wa kimalezi Kwa kulelewa na Wazazi wa Kambo. Mtoto akilelewa na Mama au Baba WA kambo hata atendewe Mazuri yapi bado atakuwa hajiamini na hayupo huru.

ATHARI KWA WATOTO WENYE MIAKA 18-50.
1. Watoto kushindwa kugawa bajeti kuwasaidia wazazi wake waliotengana.
Amtumie pesa Baba, kisha amtumie pesa Mama. Hii inaathiri uchumi wa mtoto.
Tofauti na wazazi wakiishi pamoja inakuwa rahisi kuwahudumia Kwa pamoja.

2. Mtoto kupata wakati Mgumu, amelelewa na Baba WA Kambo mpaka Kakua na baada ya kujitegemea Baba mzazi anakuja naye anataka matumizi. Hii inawapa wakati mgumu Sana watoto, huyu ni Baba yake, Yule ni Baba mlezi. Wengi hapo hujikuta wanasaliti upande mmoja na mara nyingi upande huo unakuwa upande wa Baba Mlezi.

Vipato vya wengi ni duni hivyo uwezo wa kuhudumia Mababa wawili inakuwa ngumu.

3. Watoto kutokujali Wazazi wao.
Mtoto akishakua hasa katika Mazingira ya kulelewa na Mzazi mmoja, nguvu ya wazazi Kwa mtoto inakuwa nusunusu tofauti na Aliyelelewa na wazazi mwanzo mwisho.

Ni rahisi kuwapuuza wazazi waliotengana kuliko wanaoishi pamoja. Rahisi Sana.

Na hiyo inatokana na Karma, ubinafsi uliowatenganisha ndio ubinafsi huohuo watoto wenu watautumia kuwatenga.

4. Watoto kutowaheshimu Wazazi wao.
Mara nyingi watoto hawawaheshimu wazazi waliotengana Kwa ubinafsi, watoto lazima watajua kuwa Baba aliachana na Mama kisa mchepuko (Ubinafsi wa kutaka kutosheleza tamaa zake za kimwili), au mtoto atajua kuwa Mama alipata Hawara mwenye pesa ndio maana alimuacha Baba.

Mtoto hata kama hatasema Kwa mdomo wake lakini matendo yake yatajionyesha, unajua matendo ni matokeo ya Nafsi ya ndani kabisa.

Zingatia kuwa wazazi wanakuwa muhimu na kuonekana miungu kabla ya mtoto hajapata Mtoto, yaani mtoto wako Kabla hajazaa basi anakuchukulia Kama mungu mdogo lakini akishazaa mambo hugeuka kidogo. Hii ni kutokana na kuwa naye kawa mungu mdogo sasa huna utakalomuambua Kwa habari za Uzazi. Ila Kama ulimfundisha Maadili na ulifanya wajibu wako Kwa kiwango kikubwa pasipo kuonyesha ubinafsi kwake au Kwa Baba/Mama basi ataendelea kukuona wa Maana.

Heshima ya Wazazi IPO katika malezi sio katika Kuzaa. Kuzaa ni sifa ya Mnyama hivyo hata Panya anazaa lakini malezi ndio humtofautisha Mnyama na Binadamu.

Unapoendekeza ubinafsi katika maisha yako na kuathiri watoto wako basi lazima mambo yatakugeukia
Kumbuka watoto wako ni wewe (yaani toleo lako jipya) watoto wako ni kivuli chako kila unachokifanya nao watakufanyia.

Ni muhimu kuchagua Mwenza mnayefanana ili kuepusha utengano utakaoathiri watoto na kuja kuwarudia ninyi wenyewe.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Uko deep sana mdau. Big up!!
 
Mzee wa fasihi huu uzi wako yafaa ujengewe mnara na pili ufundishwe kwenye taasisi zote zinashughulika na mahusiano mfano nyumba za ibada nk. Kutengana ni ubinafsi na ni karma
 
Ndoa ndio chanzo cha familia na familia uzaa taifa. Taifa la hovyo ujengwa na familia za hovyo, ufisadi, ubinafsi, uvivu, upigaji, ukosefu wa uongozi bora, ukosefu wa utu na uzalendo chanzo ni familia. Familia bora uzaa taifa bora.

Huko tuendako ndio kubovu kabisa
 
Wanawake wengi ubomoa ndoa zao kwa midomo yao.
Wao ndio chanzo cha uasherati yaani mume kuchepuka, upungufu wa nguvu za kiume yaani mume akiwa ndani nguvu hamna akienda nje zipo yote chanzo ni mdomo, kauli chafu, maneno machafu yote haya wanaiga kwenye tathmilia na lengo kuu la tamthilia ni kubomoa ndoa ajenda ya siri.
😂Kwamba midomo Hadi watu wanatamni wahame nyumba walizojenga wenyew
 
Hakuna kitu kinamuumiza shetani kama ndoa , thus ufanya makubwa Sana kuzibomoa kwa maana walengwa wakuu ni watoto Ili wakose muongozo kisha shetani achukue nafsi zao Ili awatumie kwenye ushoga, uteja, ukahaba, ukibaka, nk ambayo mwisho wake ni kifo cha mapema tena cha hasara duniani na kesho ahera. Lengo kuu la talaka ni Ili watoto waharibike, so mkilazimika kutengana muhimu Sana msiache kuwaombea watoto wenu ikiwemo kuwawekea kinga za kiroho Ili wasiuze nafsi zao kwa shetani.
 
Mtoto wako ni mke au mme wa mtu.Hatuishi na watoto milele majumbani pale wapo chuoni kuelekea maisha yao ya mbeleni, so mzazi ndie uamua hatma ya ndoa ya mwanae kutokana na aina ya malezi ampayo.
Hapa wazazi unawaonea kunawatoto ni pasua kichwa
 
Back
Top Bottom