Mzazi yeyote mtoto wake sio wake yeye ni mlezi wa ndoa wa mtoto wake. Mtoto wako ni mme au mke wa mtu kile anachokiona kwako au unachokijaza kwenye makuzi yake ndio anakwenda kukipractice kwenye ndoa yake, so mzazi ndie anajenga au bomoa ndoa ya mtoto wake.
Kama mzazi ni mtaliki atashindwa vipi kumwambia mwanae achanae nae huyo si una Kazi yako mbona wapo wengi asikubabishe. Wakati mwingine sio sahihi Sana kuingia kwenye ndoa na mtu ambae wazazi au kwao kuna roho ya talaka waliotalikiana ile ni roho inafatilia labda tu mtu awe matured, yaani anaendeshwa na akili na sio roho means anaejitambua.
Mtoto umleavyo ndivyo atakavyokuwa labda tu apate Neema ya kuwa na elimu ya utambuzi kuhusu nini maana ya maisha ambayo wengi awapendi kutafuta maarifa bali uongozwa na matukio au upepo mfano kucopy toka kwenye tamthilia au marafiki wapotoshi, maana lengo kuu la tamthilia zote duniani bila kujali lugha iwe za kichina, kiswahili, english, korea, nk agenda kuu nyuma yake ni kubomoa familia iwe director anajua au ajui siri behind, shida wanawake wengi hawana uwezo wa kutofautisha kitu halisi na kisicho halisi wao ucopy na kupractice kwenye ndoa zao, then ndoa inavunjika kwa mikono yao wenyewe then wanaenda tena kumlilia Mwamposa awarejeshe ndoa zao kupitia upako.