Mnataka kumbebesha Hayati Magufuli madhambi yenu?

Mnataka kumbebesha Hayati Magufuli madhambi yenu?

Tulia ww 🌈
screenshot_2024-01-27-12-30-12-1-png.2884533

ona wanavyo rembuana macho.
Wamekusikia wenyewe
 
..Magufuli alikuwa na mahabusu wa kisiasa 400+.

..Je, sasa hivi kuna mahabusu wa kisiasa?

..katika utawala wa Magufuli hata wanasiasa wanawake walikuwa wakipokea vipigo, na kudhalilishwa. Rejea matukio la Halima Mdee, Bulaya, Matiko, Ruge, kujeruhiwa.

..Je, sasa hivi kuna mwanasiasa yeyote mwanamama aliyejeruhiwa na vyombo vya dola?

..Ukiacha kuwadhuru watu kimwili Magufuli ndiye mtawala aliyefungulia wanasiasa kesi za kihunihuni, na aliyeengua wagombea wengi, kuzidi watangulizi wake.
Changamoto ni kuwa na watumishi wa Uma na vyombo vya dola wenye akili kama za mbwa.
Tukiwalaumu Marais moja kwa moja bila watumishi wa Uma na vyombo vya dola siyo sawa hata kidogo.
Rais ni mtu kama walivyo wao na wanatakiwa wamshauri na kutekeleza maagizo yake kwa weledi.
Kwa ujumla wake, tatizo kubwa ni watumishi wa Uma na siyo viongozi wakuu wa nchi.
Kama bunge, mahakama, majeshi na taasisi nyingine za uma zikifanya kazi zake kwa weledi, hizi changamoto za kumlaumu Rais zitapungua sana.
Nira za utumwa wa fikra bado hazijaondolewa kwa watumishi wa Uma.
 
Hivi mnataka tuamini kuwa uchaguzi Tanzania miaka yote ulikuwa unafanyika vizuri, kwa Amani, na bila makadokado ya Chama tawala na wapambe wake? Kwamba kufika 2015 mambo yakaharibika? Yaani, tuamini JPM na timu yake walivuruga uchaguzi ili washinde 2015? Kabla ya hapo mambo yalikuwa powa.

Mmesahau kabisa yaliyotokea 2010?
Arumeru Mashariki
Nyamagana
Igunga
Nzega
Mbeya Mjini
Arusha Mjini
Tarime
Ubungo
Kilombero
Bumbuli

Na kuwa matokeo ya uchaguzi wa Rais yalivyodaiwa kupikwa na kundi la vijana waliofadhiliwa data center kumanipulate data za Tume?

Au mmesahau jinsi vyombo vya Habari vilivyokatazwa kutangaza matokeo ya Urais kama yalivyo majimboni...

Najibiwa...
Mwanakijiji wewe ni sukuma gang...uchaguzi wa 2015 ndio JPM aliuharibu wa 2010 was the best election ever!!

Nawajibu
Hakuna mwaka Tanzania ilishuhudia damu kumwagika kwenye uchaguzi ili kuhakikisha utawala unabakia madarakani kama 2010. That's a fact not an opinion.

Nawauliza:

Nani alimwaga damu kuelekea uchaguzi wa 2020 au siku ya uchaguzi?
Kosa moja halihalalishi jingine.
Kama nyakati zote kulikuwa na wizi wa kwenye uchaguzi hakuhalalishi wizi mkubwa wa 2020.
Busara ni kukemea vitendo vya wizi wa kura ili kujenga jamii na taifa la watu wastaarabu.
 
Mara hii umesahau habari za Mwangosi...!!! Umesahau ajali ya Hayati Filikunjombe na mtoa taarifa wa kwanza wa ajali hiyo...kabla ya maneno kuwekwa sawa ..nyumba ya vioo hiyo ..tulizana Mkuu.

..hata familia ya Mwangosi inastahili kuombwa radhi, na kufutwa machozi.

..tusifumbie macho mambo ya kikatili na kinyama yanayofanywa na serikali na viongozi wetu.
 
Tujisahihishe - Kauli maarufu ya CCM.

Tukijisahihisha 2011-2014, Inatosha 2015 tunaharibu. 2016-2019 tunaanza kuhubiri tena “tujisahihishe”. 2020 tunaharibu tena, 2021-2024 tunahubiri kujisahihisha. 2025 tunaharibu tena……. Tunaendelea na pattern ile ile.

What a joke!
 
Tujisahihishe - Kauli maarufu ya CCM.

Tukijisahihisha 2011-2014, Inatosha 2015 tunaharibu. 2016-2019 tunaanza kuhubiri tena “tujisahihishe”. 2020 tunaharibu tena, 2021-2024 tunahubiri kujisahihisha. 2025 tunaharibu tena……. Tunaendelea na pattern ile ile.

What a joke!
🤣🤣🤣🤣
 
..kama kuna madaraja ya uhalifu wa kisiasa Magufuli na genge lake wako daraja la juu kuwazidi wenzao.

..kwa mfano, shambulizi dhidi ya Tundu Lissu, unaanzaje kumtetea Magufuli kwa ushenzi wa kiwango kile?
Naam! ni kupitia uhalifu wake ninathubutu kutambua madaraja ya uhalifu ; Wadokozi, vibaka na Majambazi
JPM ni daraja la juu la Ujambazi kama alivyothibitisha 2020. Ni Jambazi tu ndani ya suti. Ni jambazi tu
 
Hivi mnataka tuamini kuwa uchaguzi Tanzania miaka yote ulikuwa unafanyika vizuri, kwa Amani, na bila makadokado ya Chama tawala na wapambe wake? Kwamba kufika 2015 mambo yakaharibika? Yaani, tuamini JPM na timu yake walivuruga uchaguzi ili washinde 2015? Kabla ya hapo mambo yalikuwa powa.

Mmesahau kabisa yaliyotokea 2010?
Arumeru Mashariki
Nyamagana
Igunga
Nzega
Mbeya Mjini
Arusha Mjini
Tarime
Ubungo
Kilombero
Bumbuli

Na kuwa matokeo ya uchaguzi wa Rais yalivyodaiwa kupikwa na kundi la vijana waliofadhiliwa data center kumanipulate data za Tume?

Au mmesahau jinsi vyombo vya Habari vilivyokatazwa kutangaza matokeo ya Urais kama yalivyo majimboni...

Najibiwa...
Mwanakijiji wewe ni sukuma gang...uchaguzi wa 2015 ndio JPM aliuharibu wa 2010 was the best election ever!!

Nawajibu
Hakuna mwaka Tanzania ilishuhudia damu kumwagika kwenye uchaguzi ili kuhakikisha utawala unabakia madarakani kama 2010. That's a fact not an opinion.

Nawauliza:

Nani alimwaga damu kuelekea uchaguzi wa 2020 au siku ya uchaguzi?
Wanccm wamezidi malalamiko kuhusu Uchaguzi ni Wazi sasa Tume huru Na Katiba Mpya iwekwe
 
Kwa jinsi mambo yalivyokuwa yanaenda 2010 wale wa 2015 ndio hao hao.
Dogo Makamba anajua kuwa aliyemfikisha hapo alipo kiuongozi ni muuaji wa uchaguzi wa 2010, mtu huyo yupo hai Ila hawezi kumsema, na badala yake anamsema mtu ambaye hayupo duniani, huo ni utoto na uhuni mwingi.

Mtu mwenye hali kama ya dogo Makamba hafai kuwa kiongozi popote pale. Ni wakati sasa wa wahuni kuwekwa kando katika uongozi.
 
Mnahangaika na Magufuri aliyelala kwa amani, ila wezi wauaji na waharibufu kwa nchi yetu wapo nasi na wanaendelea na mikakati yao.

Rais aliyepo madarakani angekuwa mwema kuliko JPM angevunja bunge mara tu baada ya mazishi ya JPM.

Na kwa kuwa hakuvunja bunge maana yake alivutiwa na uchaguzi huo wa 2020 na yeye alishirikiana na JPM, huyo mama yupo hai anakula mema ya nchi pamoja na marafiki na watu wa nyumbani kwake tu.

Huku sisi tunabetua midomo tu...... "JPM alivuruga uchaguzi wa 2020, watu walijaa hofu, biashara zilifungwa ..."
Kwa nini tunapambana na mfu? Je tunawaogopa walio hai? wanaiba na kuuza rasrimali zetu mchana kweupee na kutuacha na miundombinu isiyokubalika kimataifa....

Wabongo tumekazana na taarabu.... "JPM alikuwa dikiteta...."

Nahisi aliyeturoga wabongo hakufanya makosa, tumekuwa kituko tangu tupate uhuru hadi leo hatujawahi kuwa huru kabisa.

Magufuli wala hajibu chochote kuhusu hizo lawama na hatajibu milele na milele.

Sasa basi tutaendelea kuwa wajinga wa kumlaumu mfu ilhali walio hai tunawaita waheshimiwa japo ni kausha damu?
Huyo unayemtetea hasafishiki hata kwa Detol na Dodoki.
 
Wizi wa kura na ujambazi wake hakuna kipindi kinachozidi kingine. Tofauti ni JPM hakuwa mnafiki na kona kona. Ukisikia mtu anasema 2020 ilizidi ujue huyo hajawahi kuwa front kwenye uchaguzi na kama alishiriki hakuwa insider alisikia sikia tu vitu.
Lakini nyie wezi kila mwaka mnasemaga mnashinda kwa haki. Leo mmeumbuka sasa mnasakikiziana😂
 
Kwangu Mimi issue sio uchaguzi.

Kwangu mimi ni watu kuwa busy kupambana na Marehemu huku wameacha majukumu yao ya msingi ya ujenzi wa Taifa.

Marehemu alifanya yake, Mwenyezi Mungu kachukua kiumbe chake, tunachotaka kuona kwao ni suluhu ya matatizo lukuki yanayowakabili Watanzania na nchi Kwa ujumla.
You are not serious.....Kila mwenye akili anaanza kwanza na namna viongozi wanapatikana....So Uchaguzi ni namba One...huwezi kuchagua wavivu na wala rushwa harafu unataka kuona majukum yakifanyika.
 
A
Ahaaa!! January Makamba, mpuuzi mmoja, ambae hata mitihani ya O level ilimshinda, akaiba, akapewa uongoz wa, wizara mbalimbali na akashindwa na anaendelea kushindwa. Eti nae anatuambia, upumbavu na ujinga wake . Huyu Makamba junior hana akili ni mpumbavu na mjinga tu. Kama, mtu kama huyu anaweza kuongea ujinga na upumbavu kama huo. Huko wizara ni anaongozaje. Na kama, anaongea ukweli basi ajiuzuru mara, moja ubunge na uwaziri.Kwa kuwa ametamka kuwa aliingia kwa wizi wa uchaguzi.Aliyeleta utengano wa taifa ni mzee wake, mwenye akili mbovu kama yake. Wazuri hawafi.
Anakuwaje Mjinga na amekuwa kiongozi Kwenye chama chako?

Na amepewa Nyaraka mbali mbali za wizara na wewe uko hapa unapiga makelele tu?

Mbona hizo nafasi hujapewa wewe?
 
2020 ule haukuwa wizi, ulikuwa ujambazi. Ubaya matendo mabaya huwa yanakuwa na athari hata kwa walioyafanya. Wanaoumia na wizi au ujambazi wote uliofanyika siku za nyuma ni wahusika wa wizi au ujambazi wenyewe. Sidhani kama kuna aliyefaidika toka kipindi hicho
Imewatesa sana hadi leo. Hakuna mwenye raha
 
Back
Top Bottom