Mnahangaika na Magufuri aliyelala kwa amani, ila wezi wauaji na waharibufu kwa nchi yetu wapo nasi na wanaendelea na mikakati yao.
Rais aliyepo madarakani angekuwa mwema kuliko JPM angevunja bunge mara tu baada ya mazishi ya JPM.
Na kwa kuwa hakuvunja bunge maana yake alivutiwa na uchaguzi huo wa 2020 na yeye alishirikiana na JPM, huyo mama yupo hai anakula mema ya nchi pamoja na marafiki na watu wa nyumbani kwake tu.
Huku sisi tunabetua midomo tu...... "JPM alivuruga uchaguzi wa 2020, watu walijaa hofu, biashara zilifungwa ..."
Kwa nini tunapambana na mfu? Je tunawaogopa walio hai? wanaiba na kuuza rasrimali zetu mchana kweupee na kutuacha na miundombinu isiyokubalika kimataifa....
Wabongo tumekazana na taarabu.... "JPM alikuwa dikiteta...."
Nahisi aliyeturoga wabongo hakufanya makosa, tumekuwa kituko tangu tupate uhuru hadi leo hatujawahi kuwa huru kabisa.
Magufuli wala hajibu chochote kuhusu hizo lawama na hatajibu milele na milele.
Sasa basi tutaendelea kuwa wajinga wa kumlaumu mfu ilhali walio hai tunawaita waheshimiwa japo ni kausha damu?