Mnataka kumbebesha Hayati Magufuli madhambi yenu?

Kama ni upuuzi mnataka nini?

Basi msubiri Maridhiano ya Kitaifa na nyie mtubu dhambi zenu za kutengeneza mazingira pamoja na kujiteka na kujipiga risasi....

halafu mpewe madaraka ya kupewa, si ndio lengo la Mbowe na Lissu?

Unaona ndani Kama X-ray.

Haya ya Uchaguzi hamuyawezi. Hamchaguliki.
 

Ahsante.
 
Sawa JPM ana mabaya yake na ni kweli 2020 uchaguzi ulikua wa faulo.
Ila angalau hakukua na umwagaji damu.
TUACHENI UTANI NINYI BORA HATA 2020 kura ziliibiwa ila uhai wa watu ulibakia.
2000 UMWAGAJI DAMU ULIKUA WA KUKITHIRI NA WAPO WALIOPATA ULEMAVU WA KUDUMU,NI PUNGUANI PEKEE ATAESEMA BORA 2000 KULIKO 2020.
Umwagaji damu JPM alifanya akiwa keshaingia uongozini,ila nachomkubali Magufuli hakuwa mnafiki alikua yuko mnyoofu mwenye kuonesha uhalisia wake.
TUSIDANGANYANE KUWA MKAPA NA KIKWETE HAWAKUWA WAMWAGAJI DAMU.
TENA HAO WAWILI NDIO WAMEMWAGA DAMU SANA TUU JAPO KIKWETE ALIKUA MNAFIKI AKIFANYA MADUDU CHINI YA KAPETI.
Mie ninamuheshimu Magufuli kwa vitu vitatu japo kimoja kikuu ni yeye kuwa TRANSPARENT.
HAkuwa munafiki huyu jamaa.
Ila hawa kina Mama Kizimkazi na yule mzee wa pwani wanafiki sana wanavisha watu viremba vya ukoka.
 
Huyo unayemtetea hasafishiki hata kwa Detol na Dodoki.
Sio kama anatetewa hapana.
Miaka yote toka 1995 hamkua mkiongea ila kipindi cha JPM mmeongea na kumshushia kila aina ya lawama.
THIS IS TYPICAL HYPOCRICY.
Muwache unafiki aisee.
 
Tanzania imekuwa mahali salama sasahivi kwa mafisadi, vyeti feki, wapiga madili , wahujumu uchumi, wavivu
Kitu cha kujiuliza kwanini JPM alikua akichukiwa na majority ya wana ccm wenzake??
Hivi hili nalo limekaaje mkuu??
Maana katika viongozi wote JPM ni kiongozi pekee aliyejaribu kuenda kinyume na sera nyingi za CCM.
 
Ujibiwe Mkuu!
 
..kama kuna madaraja ya uhalifu wa kisiasa Magufuli na genge lake wako daraja la juu kuwazidi wenzao.

..kwa mfano, shambulizi dhidi ya Tundu Lissu, unaanzaje kumtetea Magufuli kwa ushenzi wa kiwango kile?
πŸ€πŸ“
 
J.K.Nyerere ana sifa; Utamtupia vinyesi, samadi na majitaka. Kitu usichoweza kuondoa kwake ni harufu ya mema yake

J.P. Magufuli anasifa hizi; Utamsafisha kwa jiki na msasa na kumvalisha darzi lilofumwa na hariri na kupuliziwa utuli mkali. Kitu usichoweza kuondoa kwake ni harufu ya uvundo wa maovu aliyofanya ukiwemo Ujambazi wa 2020.

JokaKuu
 
Huyo bwanako aliharibu Kila mahala sio tuu kwenye uchaguzi Hadi kwenye diplomasia na Uchumi
 
Mkuu watu hawa hitaji Mwendazake ajibu! Wanakumbushana ubaya uliotokea kipindi chake hadi kwenye uchaguzi wa 2020 ili usijirudie .

Mkuu wewe ndiye umejipa usemaje wake! Nakukumbusha tu harufu ya ushuzi haizuiliwi kwa mikono!
 
Kumtetea Magufuli kwenye ishu ya uchaguzi serikali za mitaa mwaka 2019 na 2020 inabidi akili zako uzifanye fyatu kidogo.

Leo tuna bunge asilimia 99.99999 ni CCM watupu kwa sababu ya uhuni uliopitiliza wa utawala wake.
πŸ‘πŸ‘πŸ€πŸ™πŸ—Ό
 
Hii haiondoi ukweli kuwa Magufuli alikuwa zaidi ya shetani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…