Mnataka kumbebesha Hayati Magufuli madhambi yenu?

Mkuu watu hawa hitaji Mwendazake ajibu! Wanakumbushana ubaya uliotokea kipindi chake hadi kwenye uchaguzi wa 2020 ili usijirudie .
Wanakumbusha kijinga kwa kuwa ni wajinga, wanajua wazi kwamba ubaya haukuanzi kwa Magufuli na wala ubaya haukukoma baada ya kifo cha Magufuli. Ubaya umekuwepo tangu enzi ya Nyerere hadi leo, na utaendelea kuwepo kwa sababu wabongo walikwisha vurugwa fahamu zao na watawala toka CCM.

Yaliyotokea zamani yatajirudia na mtakuwa chini ya himaya ile ile so ni ujinga kujifariji kwa kupeleka lawama za ubaya kwa mfu ilhali wapo walio hai na wanatenda ubaya wote huku mkiwaita 'waheshimiwa' pasipo kushughulika na hao watenda ubaya walio hai.

Kwa akili hizo za wabongo mtabaki kuwa watwana wa CCM milele yote

Mitano kwa mama ccm ni ile ile msijinyonge πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ilitokea wakati wa uchaguzi, siku ya uchaguzi? Kwenye kampeni? Nani alimwaga damu kuelekea uchaguzi wa 2020? Ndiyo hoja iliyowekwa mezani.
Umefufuka baada ya kipenzi chako kusemwa kwa maovu yake! Huenda ulinufaika na ushenzi wa Magufuli lakini akili isikutoke kuwa Magufuli alikuwa janga la Taifa la karne!
 
Wewe umejikita kwenye umwagaji damu wa 2010, uko sawa. Na hao wanaomlalamikia magu kupora uchaguzi wa 2020 nao wako sawa pia! Sijui unataka kumaanisha nini hapa!
 
Iwe funzo kwa mliobaki hai sio kukaza fuvu tu
Wanambebesha madhambi yao mfu ili waendelee kuiba wagawane kila kitu chetu kisha wasepe ughaibuni, wewe unakaza fuvu kuunga mkono malaumu yao huku ukijifariji kizwazwa kwamba........ "iwe funzo kwa hao walio hai..."

Wabongo katika uhalisia wetu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kitu cha kujiuliza kwanini JPM alikua akichukiwa na majority ya wana ccm wenzake??
Hivi hili nalo limekaaje mkuu??
Maana katika viongozi wote JPM ni kiongozi pekee aliyejaribu kuenda kinyume na sera nyingi za CCM.
Alijaribu kwenda kinyume na sera nyingi za ccm, kisha apore uchaguzi Ili ccm itawale kwa shuruti! Unaumwa ww. Angeheshimu uchaguzi kisha matokeo halali yapatikane ndio mje na hizi ngonjera zenu. Wawakilishi wote wa wananchi hivi Sasa ni yeye aliwaweka kupitia uchaguzi wa kihayawani, mbona hawawatetei wananchi kama alichofanya ni kitu Cha maana?
 
Ilitokea wakati wa uchaguzi, siku ya uchaguzi? Kwenye kampeni? Nani alimwaga damu kuelekea uchaguzi wa 2020? Ndiyo hoja iliyowekwa mezani.
Kwa hiyo alichoongea makamba sio kweli kwa vile 2020 damu hazikumwagika? Alichoongea makamba ni kweli, na ulichoandika hapa wewe nacho ni cha kweli. Mlichotofautiana na makamba ni kuwa yeye kasema ya 2020 na wewe umesema ya 2010 ila cha ajabu wewe unataka habari yako iwe sawa ila yake iwe batili. Mbona nakuonaga kama ni mtu smart sana? Imekuwaje tena?
 
Wewe ni mjinga sana
 
Kumtetea Magufuli kwenye ishu ya uchaguzi serikali za mitaa mwaka 2019 na 2020 inabidi akili zako uzifanye fyatu kidogo.

Leo tuna bunge asilimia 99.99999 ni CCM watupu kwa sababu ya uhuni uliopitiliza wa utawala wake.
Kwanini Samia asingelivunja bunge ili aanze upya sababu ni mwema na mpenda haki?

Kwanini ameendelea na bunge la JPM?

Je hapo kati ya JPM na Samia Gang nani mhalifu mkuu?
 
2025 mtauliwa live kuliko 2020 endeleeni kujidanganya

JPM hakuwa mnafiki aliwaonyesha ukweli wa CCM ilivyo
Nitauliwa na nani, umeona wapi naunga mkono kuendelea kushiriki hizi chaguzi za kishenzi? Na kwa taarifa yako hiyo 2025 kutakuwa na wapiga kura wachache mno maana watu wamepuuza uchaguzi. Lakini wapinzani hasa cdm wakishiriki watapata wawakilishi wengi. Huyu mama anaweza kuwabeba ccm, lakini sio muumini sana wa siasa za kishenzi kama dhalimu magu.
 
Kwanini Samia asingelivunja bunge ili aanze upya sababu ni mwema na mpenda haki?

Kwanini ameendelea na bunge la JPM?

Je hapo kati ya JPM na Samia Gang nani mhalifu mkuu?
Hiyo bajeti haipo, lakini kwa wanaccm wote na wapenda haki wanajua siasa za magu zilikuwa za kishenzi.
 
Mkuu unatanua magoli kabla ya mtanange wa hoja kuisha. Jikite kwenye hoja iliyopo!

Mwenzio kasema mabaya ya mtu wako, kama hukubaliani, kanusha kwa kuonyesha mazuri ya mtu wako, sio kuruka ruka kama bisi bisi hapa!

Tena usilete mambo ya baba yake mkinzani wako maana yeye hajaleta hoja hiyo akiwa pamoja na baba yake! Na wala kwenye hoja yake hajamsema mtu wako kwa kumuunganisha na mzazi wake.

Kwa hiyo simama kwenye hoja iliyopo, pinga hoja kwa hoja. Chuki zako binafsi peleka huko!
 
2025 mtauliwa live kuliko 2020 endeleeni kujidanganya

JPM hakuwa mnafiki aliwaonyesha ukweli wa CCM ilivyo
Mkuu naona ujumbe wako kama wa Kinana majuzi umewalenga zaidi wenyeviti, madiwani na wabunge, maana wajumbe wananoa visu tu, wakisubiri wafanye yao! 🀣 🀣 🀣
 
2020 haukuwa uchaguzi ule. Ulikuwa uhuni wa Hali ya juu. Acha kutetea ujinga.
 
πŸ€πŸ‘πŸ‘πŸ’
 
..kama kuna madaraja ya uhalifu wa kisiasa Magufuli na genge lake wako daraja la juu kuwazidi wenzao.

..kwa mfano, shambulizi dhidi ya Tundu Lissu, unaanzaje kumtetea Magufuli kwa ushenzi wa kiwango kile?
Mzee Mwanakijiji alikuwa na Mahaba na JPM.... Inaonekana mahaba yake bado yapo.

Ni kweli 2010 JK aliiba uchaguzi as well as 2015. Ila alichokifanya JPM 2020 ulikuwa ni ujangili.
 
Pitia kwenye maktaba yako utafute Ile picha ya Magufuli akiwa kwenye kampeni akisindikizwa na Mkurugenzi wa "Tume huru ya uchaguzi"🀧
Kisha urudi tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…