Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

2009..mie nilifuatwa na dada mmoja ..nikaenda hadi pale milenium tower...baada ya kuwasikiliza ...nusu saa tu nikaona hapa nimeingia chaka..nikatoka zangu nikaenda kumsubiri break point na bia zangu...ila kuna mama huyo daily anakuja ofcn kwangu kuleta hizo bidhaa..naye akawa ana nisomesha nijiunge nikawa na mchora mtu...hajui mie nawajua kuliko yeye..

na wanafunzi wengi wa chuo ndio watu wao..
 
mkuu LIKUD kuna vitabu vingi vinaeleza mafanikio kibiashara na network marketing etc, sasa hawa jamaa wanapeana hopes za namna hiyo.. sis watz tunapenda mafanikio ya bei rahis sana, wako weng wanatamani wawe ata mabongo fleva, ma actor out of ignorance.... to b honest i hate them 4m the begnin..... mafanikio c bei rahc! lazma ulipe gharama kubwa mkuu.
 
Jana tu wifi yangu katoka mwanza kuja kuzindua kitabu cha oriflame ,ananiambia soma utapenda kaniletea majalida kumheshimu nikaingia nayo chumbani asubuhi nikampa kwa kweli sitaki hata kusikia huo upuuzi wa flp,gnld, oriflame ,deci na nyingine nyingi tu,mimi sipendi na wala sittaki hela ya bure wala sitoi bure hela yangu,kama sikuweza kamatwa kwenye deci what the hell will convince me??never tena huwa siwasikilizagi nina mdogo wangu wa damu yuko huko walla sitaki kusikia pruduct blablabla
 
[


. Hapo kwenye dawa ya gout itabidi nikupm aisee


Now back to you super idiot LIKUD.

Graduatism sickness ni ugonjwa mbaya kuliko ukimwi. Imani ya kwamba ukiwa graduate basi unastahili kipato fulani hata kama huna kazi ni UPUMBAVU (ukimind nipeleke mahakamani).

Namna yako ya kusema kwamba kwa graduate laki sita ni fedha za kuzipata kwa siku, ni sawa na kusema kuwa maafisa wote wa serikali kwa level ya TGS D ni mataahira kwa kuwa wamekubali kufanya kazi kwa mshahara wa shilingi 349,270 kwa mwezi ambayo ni karibu nusu ya hiyo laki sita.

Unapozungumzia mafanikio, basi ni suala la ulipokuwepo awali na ulipofika. Huyo anayejisifia kuwa amefika Nairobi ni haki yake. Sijui ni nini cha kushangaza hapo kwa mama Tupele aliyekuwa anauza vitumbue kwenye mavumbi pale vingunguti akiinuka kiasi cha kuwa na biashara inayomfanya asafiri hadi Nairobi.

Hauna haja ya kuwatukana watu kwa kuwa umekosa courage ya kufanya wanachofanya. Wewe kaa na makaratasi yako ya degree lakini wenzako wana namna yao pia ya kutafuta mafanikio. Network Marketing haijaanza Tanzania, imetokea huko kwa waliokufundisha DEGREE badala ya JANDO NA UNYAGO, na inaendelea si kwamba imesimama.

Pale Arusha yuko mama mmoja alikuwa fundi cherehani, sasa tunavyoongea ni MILIONEA sababu ya FLP. Mimi Mwana Mtoka Pabaya ni member wa FLP na nilitambulishwa huko na member wa JF. Hata sasa membership yangu ni hai LAKINI mimi sikuwa na courage ya kuendelea na biashara hiyo, ila ninafaidika kwa punguzo la bei kwa products za FLP kama member.

Kushindwa kwangu kufanikiwa kwenye Network Marketing hakunifanyi niwatukane. Like any other business it take a lot of efforts and enthusiasm to cross the berriers; I AM NOT COURAGEOUS na nimeshindwa, lkn sisemi kuwa ni mbaya.

La kama unafikiri ni utapeli basi hiyo ni level yako ya ujinga inakuongoza. Mimi sina cha kutolea ushuhuda kiuchumi lakini kitabibu ninacho. Wakati nikijaribu jaribu kufanya hiyo biashara, nilimuuzia jirani yangu dozi ya gout, amepona na yeye amekuwa member na anafanya biashara hiyo huko kwao Kilimanjaro. Ajabu ni kwamba, yeye amefanikiwa kibiashara kwa kuwa kila aliyemuona na magongo sababu ya gout alitaka kujua ameponaje, kwa hiyo soko lake limekuwa kubwa kwa ajili hiyo.

Ningefurahi kama ungechukua calculator ukazidisha 600,000 kwa siku 365 na kutuandikia jawabu hapa ubaoni. Nafikiri utawasaidia GRADUATES kutambua level yao ya mapato kwa mwaka.
 
Last edited by a moderator:
hahaha,watu mnaongea kwa uchungu kweli maskini....i dont know abt other network marketing companies manake sijazistudy, but flp ni genuine company na inalipa kodi TRA kama kampuni nyingine yoyote, marketing plan ya forever iko wazi sana mtu yoyote anaweza kuisoma akafanya business na akafanikiwa.
wengi wanaojiunga flp thinking kuna hela za bure ama ni rahisi kufanya business ndio wanaokua disappointed sana.
lkn ni biashara nzuri sana kama umeelewa vizuri jinsi inavyofanyika. kwa kifupi flp sio utapeli, hizo supplements zimesaidia watu sana na wengine kipato kimeongezeka sana.
kwa wale mnaodhani ni utapeli,definitely network marketing is NOT for you. #no hard feelings#
 
Yani wewe ndo fal.a kweli...Nyani haoni kundule...Hiyo "silly" ni kiswahili cha wapi..? Nilitegemea uwe mfano....

Cc to LIKUD

Nawewe hiyo
cc to likud ni lugha gani?? Nyani haoni??
 
Last edited by a moderator:
Acha wivu mbona mixing yake iko powa tu.....Mjitu mingine bana .....tabu kwelkweli kama ww hutaki wenzio ndio Burudaaaaaani......
Mkuu nikupe ushauri wa bure! Acha ulimbukeni! Ukiamua kutumia kiswahili andika kiswahili na ukiamua kutumia kiingereza andika kiingereza. Hii changanya uliyofanya inaharibu ladha nzima ya ulichoandika na inaonyesha ulimbukeni wa hali ya juu!
 
Kuna mdada alinifuata alikua gnld mwaka 2010,akanipeleka sinza mori katika semina,nikasikiliza,ila nikaona sitaweza hii kazi,mwaka jana nikakutana na mshikaji mmoja yeye yupo Living forever,naye akaongea mengi sana,ilikua mlimani city,nikauliza changamoto zake,nikaona sitaweza,nikakutana tena na yule dada aliekuwa gnld,sasa hivi kahamia Living Forever,ananishawishi tena,nikamuuliza kwanini amehama gnld,akajb mambo ayakuwa mazuri,nikamuuliza je kipindi kile unGefanikiwa kuniungisha si ingekula kwangu,akacheka cheka tu,nikawajibu mi siwezi kuifanya iyo kazi,sasa wiki hii shemeji yenu kakutana nao,ameshawishia imemuingia,ni memwambia aje dar,nimpeleke semina za living forever,kama sehemu tatu,alafu akae chini afanye uamuzi,sema wengi wanaotoa ushuhuda wanapenda kuponda taaluma zingine,hiki si kitu kizuri
 
Capitalism.jpg
 
inasemekana ukiwa member wa FLP na ukiwa na chain ndefu ndivyo unavyopata pesa nyingi ila pia kuna kipindi utatakiwa kutoa kafala je kuna ukweli wowote hapa?
 
Mimi walinikokota mpaka New Arusha........nilitukana mpaka basi......ubaya hawakwambii unaenda kusikiliza forever living.....wanakuelezaeleza tu bla bla mpaka ufike ndio unagundua......

Mie nina hasira nao sana hawa jamaa ! nilikuwa na mgonjwa wangu wa Cancer na nika wa nimeacha akiba ya laki 3 nyumbani. Basi jirani yangu akamleta huyo mtu GNLD, huku na huku wakaondoka na ile laki 3 !
Aiseeh......! nilim'mind mgonjwa kwa siku tatu hatuongei !
Huku na huku kuna mjinga mmoja akawapa number yangu, wakanishawishi nifike bila kuwajuwa ni akina nani. Kwakuwa field yangu ni mambo ya sales, nikahisi labda nitajifunza kitu. Daah ! nilipofika.......watu wengi na miongoni mwao wanawake ni wengi ! mahali popote penye wanawake wengi basi ujinga ni mwingi.
Nilimwanga mitusi kwa hasira yaani mpaka walijuta !
 
Back
Top Bottom