Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Swali langu kwao ambalo hawajawahi kunijibu ni kuwa kwa kuwa wanasema bidhaa zao zinatokana na mimea, mbegu na vitu asilia, kwa nini wasifanye kampeni ya kutumia mazao asilia badala ya kutengeneza "products"? Kweli mimi wamekula laki moja yangu ya kiingilio, lakini baada ya kutafakari kwa kina nimesema hakuna biashara ya aina hiyo zaidi ya utapeli kama wa DECI. Wamehangaika kuniita kwenye training mara mikutano, lakini nimeona ni upuuzi.
 
Yani wewe ndo fal.a kweli...Nyani haoni kundule...Hiyo "silly" ni kiswahili cha wapi..? Nilitegemea uwe mfano....

Cc to LIKUD

Hahaha na wewe umerudia kwa walewale sasa hiyo "pum.bavu" mbona na wewe umeirudia kwa kiingereza?
 
Last edited by a moderator:
Jumatano ya wiki iliyo pita , nikiwa maeneo ya Mlimani City, nilikutana na mdada mmoja niliyekuwa nimepotezana naye for like 2 years..Aliomba namba zangu za simu kisha akaniuliza kama nitakuwa na nafasi jumapili ya wiki hiyo around saa saba mchana. I told her what is the problem? akaniambia kuna meeting muhimu sana ambayo angependa kuona na mimi nikishiriki. Nikamwambia hakuna shida. Siku hiyo akaniomba tukutane maeneo ya mwenge, nikamdrive hadi pale ITV kwenye ukumbi wa mikutano wa GNLD. She told me it was a GNLD meeting. She is a member, she has invited me to listen to what they are doing and may be if interested nijiunge nao pia. Nilitaka kurudi hapo hapo but nikasema ngoja niende kuwasikia wana kitu gani kipya ambacho sijawahi kukisikia mahali., ( I knew about this cra.p ) since 2001 and i know what they are actually doing ).

WAKATI WA KUTOA USHUHUDA

Baada ya introduction na kabobo kutoka kwa aliyekuwa msemaji mkuu wa hiyo meeting, ikafikia zamu ya watu mbalimbali ambao ni memba wa GNLD kutoa shuhuda zao. Huyo msichana alikuwa miongoni mwa walio toa ushuhuda.

I WAS SO SO DISAPOINTED WITH THEM.

She said, nimejiunga GNLD tangu mwaka 2009 and blah blah, Now ninaingiza PESA NYINGI SANA KWA MWEZI!
Ninaingiza shilingi LAKI SITA KWA MWEZI! ( Hivi kweli Graduate wa Chuo Kikuu anaweza kuwa na mawazo mgando kiasi hiki! Shilingi laki sita kwa mwezi ni pesa ambayo mtu anaweza kuongea na kujisifu mbele ya watu? Hii ni hela unayo takiwa kuingiza kwa siku moja bana acheni ujinga nyie.

Others were talking like, NIMEFIKA HADI NAIROBI MIMI! HUWEZI KUAMINI! UKINIONA UNANICHUKULIA POA, ILA NIMEFIKA HADI NAIROBI KWA KAZI HII HII?

( Seriously kweli! kufika Nairobi nalo ni jambo la kujisifu mbele ya kadamnasi ! )

Wengi wao wanaongea kuhusu laki nne kwa mwezi na utoto utoto kama huo..

BRAINWASHERS
: Wakati wa shuhuda kuna jamaa huwa wanasimama na kuongea utoto mwingi like u know nilikuwa meneja wa T.R.A mkoa but nimeacha baada ya kuona GNLD inanilipa.. Mwingine akasema " Nilikuwa muhasibu BARICK, nalipwa MILIONI NNE kwa mwezi, ila nimeacha kazi baada ya kuona GNLD ndio mpango. Plus utoto utoto mwingine kama huo..

Mwisho wa siku i told her, please be serious even for a second, how dare you bring me to a place like this. What do u take me for? or what kind of a fool do u think i am? do u confuse me with a looser or something ? Do i look like someone who is joking about his life? U shall not tell me about this cra.p again...

Kiukweli niliona amenidhalilisha sana, i say..

These people, are realy dont know what is going on in their lives na wanahitaji kukombolewa. Kuwa describe hawa watu wa GNLD na FOREVER LIVING PRODUCTS in a single word, they are " LOOSERS".

Inasikitisha kusikia haya. Networking marketing, watu wamekuwa wapofu sana kiasa cha kushindwa kuona jinsi ambavyo wanapoteza mda na kuwapotezea watu muda kwa vitu visivyo na tija. Anakufuata mtu akidhani una level nae sawa ya ufikiri, kwa kweli si jambo la kuomba likukute. They will come in many forms, atleast dubbed them nicely....LOOSERS
 
Yote yaliyosemwa na wakuu hapo juu ni kweli kabisa, mimi yaliwahi kunikuta, rafiki yangu tuliyepoteana kwa muda mrefu siku moja tulikutana maeneo ya Bamaga canteen ya mzalendo.

Kama kawaida ya marafiki kuulizana habari za maisha na maendeleo huwa ni kawaida. Basi jamaa akaanza kunishawishi kwa kuniambia kuna mafanikio zaidi ya haya niliyonayo pindi tu nikijiunga na kampani yao ya Forever Living ambayo anataka kuni-nitambulisha kwa wahusika.

Nilikaribishwa siku ya jumanne jengo la Millenium Tower ghorofa ile ile ya Mzalendo pub, nilichokikuta huko ni mbwembwe zile zile za ushuhuda pamoja na video za watu waliofanikiwa na kuwa mabilionea wa kutisha lakini mwisho wa siku wakaniomba nijiunge na kundi lao.

Na ili niweze kutambullika wka uongozi wa juu lazima nitoe kiingilio cha shs. 500,000/= ili niweze kupata product zangu ambazo nitaziuza kwa muda wangu baada ya saa za kazi. Hata hivyo nilishtuka nikaingia mitini pamoja na jitihada za rafiki yangu kunishawishi ziligonga mwamba baada ya mimi kuona usumbufu na kubadili laini yangu ya simu.

Leo hii ninapoandika hivi jamaa kachoka ile mbaya maana hata nikimpita njiani naogopa kumsalimia asije nisumbua tena. Ila nimesikia kwa watu kwamba jamaa yangu alishindwa kuendelea na Forever Living sasa hivi yupo na kampuni moja mpya inaitwa GREEN...
 
Hahaha na wewe umerudia kwa walewale sasa hiyo "pum.bavu" mbona na wewe umeirudia kwa kiingereza?

Sikiliza wewe kichwa maji...Mimi sijajifunga na matumizi ya lugha umenielewa.... Sasa huyo -------- mwenzako yeye anajifanya kwamba lugha moja ndo inayotakiwa wakati hata yeye ana-mix....
 
Acheni kudharau kazi za watu kwani nyie mnafanya kazi gani zaidi ya kuonyesha madharau humu kama hutaki kitu kaa kimya maana kinaweza kuwa kina tija kwa mwingine sio lazima upende kila kitu kwenye hii dunia kuna watu wanafaidika sana tu.
 
hii ni kudanganya wazi wazi na kutumika vibaya ili kuingiza watanzania wenzako kwenye matatizo...uache kazi BOT au BARICK tena mhasibu, ukauze lotion au juice na food supplements. haniingii akilini :coffee: Sitaki kusikia kabisa hawo wanaojiita sijui forever. :A S thumbs_down:
 
Acheni kudharau kazi za watu kwani nyie mnafanya kazi gani zaidi ya kuonyesha madharau humu kama hutaki kitu kaa kimya maana kinaweza kuwa kina tija kwa mwingine sio lazima upende kila kitu kwenye hii dunia kuna watu wanafaidika sana tu.

wao ndio wana dharau, unajua kumfuata mtu mzima na heshima zake na kumueleza upu.thread kama huo ni dharau ya hali ya juu sana!
 
Wakuu hii biashara ya hawa jamaa ni sawa zile zinazoitwa pyramid schemes ambazo zimepigwa marufuku nchi nyingi, na sasa kwa kuzihalalisha wamezipa majina ya kutumia kama business networking. Mfumo wake ni ule ule wa pyramid kunakuwa na ncha na base pana. Mtu ambaye yuko kwenye ncha kupata faida kutokana na watu chini yake aliowaingiza kwenye biashara na manunuzi yao ya bidhaa. Kadiri base inavyopanuka ndio mapato yake huongezeka. Products za FLP ni supplements tu na si za tiba ni wizi na udanganyifu tu unaofanyika na bei zake ni za kinyonyaji. Kwanza hazitambuliki na WHO. WHO huratibu madawa ya tiba mbali mbali na kuhakikisha zinapatikana kwa bei zisizonyonya watu. Kwa pande wa FLP miongoni mwa wanzilishi wa hiyo biashara tz ni dada mmoja aishie UK ambaye ni shemeji na aliyewahi kuwa waziri mkuu mmoja wa tz, kwa nafasi ya shemeji yake aliweza kufanya biashara nzuri kwa vigogo wengi wenye fedha akaweza kuongeza watu wengi akanufaika na kuendelea kunufaika kwa kuwa na base kubwa kwenye hiyo pyramid
 
Hahahaha nimecheka sana na baadhi ya comment za members, ila hawa jamaa uwa wanaongea sana
 
Kuna DECI ambayo imekuwepo humu nchini mda mrefu tu (Forever Living Products).., ipo disguised as a Multi level marketing sijui nini.., eti una nunua dawa kwa shillingi laki saba then unaenda kuziuza sijui.., alafu eti ukimshawishi mwenzako kwenda kukunua hayo madawa eti ile pesa yake mnagawana.

Yaani dawa ambazo kiu halisia zina-gharimu elfu 20 we una-nunua kwa laki saba..!!!, then huyo unae-mleta na yeye akiweza kupata maboya wenzake wa kwenda kununua basi ile pesa yao mnagawana nyie up-liners wale and the pyramid goes on and on! huu si wizi kabisa..! kwanini hawapigwi mnyororo hawa.., kwanza hata sijui kama wana-mashine za EFD hawa!


how-mlm-pyramid-scheme-works.png
 
Toka niisikie hii kitu, imewabeba wengi lakini sijasikia wakilalamika kufirisika labda kama wanafanya siri.

Maana hawa jamaa kwa mbwembwe...wanataka mpaka mashuka yawe ya forever living.

Siwatofautishi sana na alovera maana nayo dah....wana mpaka malapa ya alovera kwendea bafuni eti wadudu wasichanganyike na sabuni.
 
Du iyo issue walinisomesha lkn nikachomoa kabisa

Kwa kweli hata mimi nilichomoa tena nilimchomolea rafiki yangu wa karibu kiaina kwani sababu ya kumheshimu nilimpa lugha ya kumdanganya ili asinielewe vby. Lakini kiukweli ile ni DECI nyingine hapa nchini
 
Kuna DECI ambayo imekuwepo humu nchini mda mrefu tu (Forever Living Products).., ipo disguised as a Multi level marketing sijui nini.., eti una nunua dawa kwa shillingi laki saba then unaenda kuziuza sijui.., alafu eti ukimshawishi mwenzako kwenda kukunua hayo madawa eti ile pesa yake mnagawana.., yaan dawa ambazo kiu halisia zina-gharimu elfu 20 we una-nunua kwa laki saba..!!!, then huyo unae-mleta na yeye akiweza kupata maboya wenzake wa kwenda kununua basi ile pesa yao mnagawana nyie up-liners wale and the pyramid goes on and on..! huu si wizi wa ki-mbwa kabisa..! kwanini hawapigwi mnyororo hawa.., kwanza hata sijui kama wana-mashine za EFD hawa..!!!

jamani msitukane vitu msivyojua. kama walikushauri ukakataa ni uamuzi wako lakini usiwatukane kuwa ni wizi wa ki-mbwa. najua watu wengi wanaouza hizi products na wanapata hela nzuri sana huwezi amini. wananunua na kuuza hizi products,wengine hadi wana maduka. jaribu kuuliza upate ukweli.
 
Back
Top Bottom