Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Ukiwaambia kuwa hao ni matapeli mnakosana kabisa. Elimu hii iende na kwa wengine. Niwe mkweli hawa watu hii biashara si ya kuwashirikisha watu wanaotaka kufanya ujasiriamali wenye maendeleo ya kweli sio hii biashara.


Mkuu nimeshuhudia mwenyewe cjui nan atakuja kunishawishi nikubaliane nae, alafu ukiwasikia kwny marketing zao wanaelezea positive lakn upande wa negative hawaugusi, ukiwasikiliza utajiona baada ya mwezi utakuwa tajiri! Illusions!!!
 
Hasa kwenye inbox zangu every weekend and then ni huu utumbo wa FLP……kwa nini vijana na wenye nguvu msifanye kazi zinazoonekana na mapato mkalipa serikalini??!!!, Mara kiyosaki sjui nani na nani ya nn!!!
 
niliwatafutaga kitambo wakanambia tukutane millenium tower, baada ya kuongea nao nikagundua ni "wizi mtupu" nikaachana nao, mi mwenyewe born town utaanzaaje kuniibia
 
Mkuu nimeshuhudia mwenyewe cjui nan atakuja kunishawishi nikubaliane nae, alafu ukiwasikia kwny marketing zao wanaelezea positive lakn upande wa negative hawaugusi, ukiwasikiliza utajiona baada ya mwezi utakuwa tajiri! Illusions!!!

halafu maswali ya kujiuliza ni haya....
1. Anayekwambia utafanikiwa mbona huwa wote wamechoka balaa.....
2. Halafu wanatoa njia za mafanikio ambazo hazitekelezeki kwani utakuta wanasema ukiongeza watu wewe utakuwa juu na utapata gawio kubwa.... Sasa utapateje gawio bila kuuza product...
3. Product zenyewe bei ni kubwa sana.... Mtu wa kawaida hawezi kumudu hata kidogo. Sasa katika mazingira ya Kitanzania biashara gani itakuwa bila ya kuwa na wateja wanao mudu bei za product husika.

Kwamfano hao wanao jiita GNLD ndio hawafai hata bure wamewaingiza watu mikenge hadi kufikia ndoa kuvunjika kutokana na utapeli wao. Unakuta mwanamke anadanganywa na yeye anakwenda kumshawishi mumewe wanapoteza mitaji ya biashara mwisho wa yote ni ugomvi usioisha. Wala sishauri mtu kuingia huku... Kama mtu anapenda kufanya biashara afanye ile inayofanana na mazingira ya kitanzania.
 
Yaan kweli umeshindwa kutumia hata 0.0001% ya ubongo wako kweli..??! Em' wauze iphone5 au nyanya au hata vitunguu tu uone kama mi nitaongea kitu.., tatizo mnauza rubbish ambayo gharama yake si zaidi ya 20k kwa shs. laki saba...!! hio kusema mnuza dawa sijui nini ni ujanja wa kuficha sura halisi ya hii pyramid scheme ili serikali wasiweze kuwafungia..! mbwa kabisa..!!

sijasema kuwa mimi nauza.

 
yaani wakikuzia kwa laki saba hizo product huuzi hata lakimoja mwishowe unakaa nazo hizo product hadI kupiga nazo picha.....jamaaa wezi sana

Nimecheka lakini inaumiza sana.... Kuna jamaa yangu alijitutumua kwa ushawishi wa mchumba wake akakopa pesa kwa mama yake mzazi na kununua mzigo wa milioni moja na laki nane. Hadi sasa amebaki na mzigo mzima ndani na mahusiano hayapo tena wenye nguvu wamemchukua mchumba wake. Ana product za kushafishia magari na hana hata gari maskini wa Mungu. Amebaki na kumbukumbu ya kutapeliwa na kunyang'anywa mchumba.
 
Dah hii thread imenigusa aisee hawa watu sitaki hata kuwasikia.wana uongo mwingiii na ujanja ujanja tuu.yan saivi ndo wamezidi kuongezeka kila mtu foreva foreva.sitaki hata kuwasikia
 
Biashara inahitaji kupambana nawajua wadau wa 4ever living wanapiga hela sana kuna m1 ana nyumba ya ghorofa na anapush ndinga ya 0 km biashara nzuri hii ukijituma! iendelee.
Sikatai kama unaweza kupiga hela.., ninachopinga ni hao wapuuzi kununua magari ya 0km kwa jasho la wauza maandazi.., mambo ya ki-mbwa sana haya..!
 
Yaan hata mi nishasomeshwaa sana kuhusu hawaa watu ila mwenye nayo yupo Marekan anaitwa Morgan ana jina refu nimelisahau,ila hua siwaelewii kabisaaa
 
mkuu ata mim kuna rafiki yng wa karibu sana anani convince nijiunge na GNLD ila mim mpk dakika hii hatujaafikiana bado,ni zaidi ya mwezi sasa tangu aanze kuniletea hizo swagga ila mim namkwepa mpk leo hii.hawa members wanatusumbua sana sisi tusiokuwa wadau.

Mwogope huyo kama ukoma, atakuingiza ambapo utajuta
 
Aisee wezii kbsaaaa, kuna rafik yangu alinishawishi saaaana ila dah, sikumwelewa,,et niwe na kianzio cha Laki 7, mmh niliishia kuguna tuu, Laki tu kwangu Ishuu, naishi huku mbagala, nani atanunua dawa ya mswaki 25,000?
 
niliwatafutaga kitambo wakanambia tukutane millenium tower, baada ya kuongea nao nikagundua ni "wizi mtupu" nikaachana nao, mi mwenyewe born town utaanzaaje kuniibia

Hata mimi waliniita hapohapo. Cjui ndo mizimu yao ya kudanyia watu ipo
 
Aisee wezii kbsaaaa, kuna rafik yangu alinishawishi saaaana ila dah, sikumwelewa,,et niwe na kianzio cha Laki 7, mmh niliishia kuguna tuu, Laki tu kwangu Ishuu, naishi huku mbagala, nani atanunua dawa ya mswaki 25,000?

Utamuuzia nani na whitedent zimejaa kibao za buku jero..
 
Hii Biashara imekaa ki-umachinga. Unazunguka na Begi Mgongoni lenye Madawa kama Mganga wa Kienyeji.

Kwa Maisha ya Kiafrica bado sana kujihusisha Biashara za MLM kama hizi.

Na mara nyingi Mwisho wake huwa "Ku-Give Up" na kubakia na Madawa nyumbani yasokuwa a tija kama Mtoa Mada aliyetangulia kuwa unabakia na car-Shampoo wakati hata hiyo Gari yenyewe huna. Lol.
 
Toka niisikie hii kitu, imewabeba wengi lakini sijasikia wakilalamika kufirisika labda kama wanafanya siri.

Maana hawa jamaa kwa mbwembwe...wanataka mpaka mashuka yawe ya forever living.

Siwatofautishi sana na alovera maana nayo dah....wana mpaka malapa ya alovera kwendea bafuni eti wadudu wasichanganyike na sabuni.

Mkuu kwa iyo ishu ya ndala umeniacha hoi
 
Aisee nije nisikie mtu ananishawishi niingie kwenye hii DECI namba mbili naanza na huyo huyo kumkata mabanzi, haiwezekani mtu utoe laki saba kijingajinga ni bora uanzishe biashara ya vitumbua na siyo kwenye hii kamari
 
Kinachoshangaza kwa nini serikali ipo kimya kwenye hili na nina uhakika wanaijua mechanism yake?
 
Kinachoshangaza kwa nini serikali ipo kimya kwenye hili na nina uhakika wanaijua mechanism yake?

wakuu kwanza poleni....
serikali haijakaa kimya kwa kifupi two to three week from today mtaona kazi ya serikali kwa sababu kuwapiga marufuku kunatakiwa kushirikisha wizara kadhaa.

tulipongeze jeshi la polisi kwa sababu ni siku nyingi tu wamekuwa wakitaka kupiga marufuku biashara hii haramu ya consumer fraud lakini changamoto ni mambo ya protokali za kisheria.

ushauri usijiunge, kama ndugu yako au rafiki yako yupo huko auze bidhaa fasta vinginevyo itakula kwake muda si mrefu
 
Back
Top Bottom