Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

2009..mie nilifuatwa na dada mmoja ..nikaenda hadi pale milenium tower...baada ya kuwasikiliza ...nusu saa tu nikaona hapa nimeingia chaka..nikatoka zangu nikaenda kumsubiri break point na bia zangu...ila kuna mama huyo daily anakuja ofcn kwangu kuleta hizo bidhaa..naye akawa ana nisomesha nijiunge nikawa na mchora mtu...hajui mie nawajua kuliko yeye..

na wanafunzi wengi wa chuo ndio watu wao..
 
mkuu LIKUD kuna vitabu vingi vinaeleza mafanikio kibiashara na network marketing etc, sasa hawa jamaa wanapeana hopes za namna hiyo.. sis watz tunapenda mafanikio ya bei rahis sana, wako weng wanatamani wawe ata mabongo fleva, ma actor out of ignorance.... to b honest i hate them 4m the begnin..... mafanikio c bei rahc! lazma ulipe gharama kubwa mkuu.
 
Jana tu wifi yangu katoka mwanza kuja kuzindua kitabu cha oriflame ,ananiambia soma utapenda kaniletea majalida kumheshimu nikaingia nayo chumbani asubuhi nikampa kwa kweli sitaki hata kusikia huo upuuzi wa flp,gnld, oriflame ,deci na nyingine nyingi tu,mimi sipendi na wala sittaki hela ya bure wala sitoi bure hela yangu,kama sikuweza kamatwa kwenye deci what the hell will convince me??never tena huwa siwasikilizagi nina mdogo wangu wa damu yuko huko walla sitaki kusikia pruduct blablabla
 
[


. Hapo kwenye dawa ya gout itabidi nikupm aisee


 
Last edited by a moderator:
hahaha,watu mnaongea kwa uchungu kweli maskini....i dont know abt other network marketing companies manake sijazistudy, but flp ni genuine company na inalipa kodi TRA kama kampuni nyingine yoyote, marketing plan ya forever iko wazi sana mtu yoyote anaweza kuisoma akafanya business na akafanikiwa.
wengi wanaojiunga flp thinking kuna hela za bure ama ni rahisi kufanya business ndio wanaokua disappointed sana.
lkn ni biashara nzuri sana kama umeelewa vizuri jinsi inavyofanyika. kwa kifupi flp sio utapeli, hizo supplements zimesaidia watu sana na wengine kipato kimeongezeka sana.
kwa wale mnaodhani ni utapeli,definitely network marketing is NOT for you. #no hard feelings#
 
Yani wewe ndo fal.a kweli...Nyani haoni kundule...Hiyo "silly" ni kiswahili cha wapi..? Nilitegemea uwe mfano....

Cc to LIKUD

Nawewe hiyo
cc to likud ni lugha gani?? Nyani haoni??
 
Last edited by a moderator:
Acha wivu mbona mixing yake iko powa tu.....Mjitu mingine bana .....tabu kwelkweli kama ww hutaki wenzio ndio Burudaaaaaani......
Mkuu nikupe ushauri wa bure! Acha ulimbukeni! Ukiamua kutumia kiswahili andika kiswahili na ukiamua kutumia kiingereza andika kiingereza. Hii changanya uliyofanya inaharibu ladha nzima ya ulichoandika na inaonyesha ulimbukeni wa hali ya juu!
 
Kuna mdada alinifuata alikua gnld mwaka 2010,akanipeleka sinza mori katika semina,nikasikiliza,ila nikaona sitaweza hii kazi,mwaka jana nikakutana na mshikaji mmoja yeye yupo Living forever,naye akaongea mengi sana,ilikua mlimani city,nikauliza changamoto zake,nikaona sitaweza,nikakutana tena na yule dada aliekuwa gnld,sasa hivi kahamia Living Forever,ananishawishi tena,nikamuuliza kwanini amehama gnld,akajb mambo ayakuwa mazuri,nikamuuliza je kipindi kile unGefanikiwa kuniungisha si ingekula kwangu,akacheka cheka tu,nikawajibu mi siwezi kuifanya iyo kazi,sasa wiki hii shemeji yenu kakutana nao,ameshawishia imemuingia,ni memwambia aje dar,nimpeleke semina za living forever,kama sehemu tatu,alafu akae chini afanye uamuzi,sema wengi wanaotoa ushuhuda wanapenda kuponda taaluma zingine,hiki si kitu kizuri
 
inasemekana ukiwa member wa FLP na ukiwa na chain ndefu ndivyo unavyopata pesa nyingi ila pia kuna kipindi utatakiwa kutoa kafala je kuna ukweli wowote hapa?
 
Mimi walinikokota mpaka New Arusha........nilitukana mpaka basi......ubaya hawakwambii unaenda kusikiliza forever living.....wanakuelezaeleza tu bla bla mpaka ufike ndio unagundua......

Mie nina hasira nao sana hawa jamaa ! nilikuwa na mgonjwa wangu wa Cancer na nika wa nimeacha akiba ya laki 3 nyumbani. Basi jirani yangu akamleta huyo mtu GNLD, huku na huku wakaondoka na ile laki 3 !
Aiseeh......! nilim'mind mgonjwa kwa siku tatu hatuongei !
Huku na huku kuna mjinga mmoja akawapa number yangu, wakanishawishi nifike bila kuwajuwa ni akina nani. Kwakuwa field yangu ni mambo ya sales, nikahisi labda nitajifunza kitu. Daah ! nilipofika.......watu wengi na miongoni mwao wanawake ni wengi ! mahali popote penye wanawake wengi basi ujinga ni mwingi.
Nilimwanga mitusi kwa hasira yaani mpaka walijuta !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…