Ukiwaambia kuwa hao ni matapeli mnakosana kabisa. Elimu hii iende na kwa wengine. Niwe mkweli hawa watu hii biashara si ya kuwashirikisha watu wanaotaka kufanya ujasiriamali wenye maendeleo ya kweli sio hii biashara.
Mkuu nimeshuhudia mwenyewe cjui nan atakuja kunishawishi nikubaliane nae, alafu ukiwasikia kwny marketing zao wanaelezea positive lakn upande wa negative hawaugusi, ukiwasikiliza utajiona baada ya mwezi utakuwa tajiri! Illusions!!!
Yaan kweli umeshindwa kutumia hata 0.0001% ya ubongo wako kweli..??! Em' wauze iphone5 au nyanya au hata vitunguu tu uone kama mi nitaongea kitu.., tatizo mnauza rubbish ambayo gharama yake si zaidi ya 20k kwa shs. laki saba...!! hio kusema mnuza dawa sijui nini ni ujanja wa kuficha sura halisi ya hii pyramid scheme ili serikali wasiweze kuwafungia..! mbwa kabisa..!!
yaani wakikuzia kwa laki saba hizo product huuzi hata lakimoja mwishowe unakaa nazo hizo product hadI kupiga nazo picha.....jamaaa wezi sana
Sikatai kama unaweza kupiga hela.., ninachopinga ni hao wapuuzi kununua magari ya 0km kwa jasho la wauza maandazi.., mambo ya ki-mbwa sana haya..!Biashara inahitaji kupambana nawajua wadau wa 4ever living wanapiga hela sana kuna m1 ana nyumba ya ghorofa na anapush ndinga ya 0 km biashara nzuri hii ukijituma! iendelee.
mkuu ata mim kuna rafiki yng wa karibu sana anani convince nijiunge na GNLD ila mim mpk dakika hii hatujaafikiana bado,ni zaidi ya mwezi sasa tangu aanze kuniletea hizo swagga ila mim namkwepa mpk leo hii.hawa members wanatusumbua sana sisi tusiokuwa wadau.
niliwatafutaga kitambo wakanambia tukutane millenium tower, baada ya kuongea nao nikagundua ni "wizi mtupu" nikaachana nao, mi mwenyewe born town utaanzaaje kuniibia
Aisee wezii kbsaaaa, kuna rafik yangu alinishawishi saaaana ila dah, sikumwelewa,,et niwe na kianzio cha Laki 7, mmh niliishia kuguna tuu, Laki tu kwangu Ishuu, naishi huku mbagala, nani atanunua dawa ya mswaki 25,000?
Toka niisikie hii kitu, imewabeba wengi lakini sijasikia wakilalamika kufirisika labda kama wanafanya siri.
Maana hawa jamaa kwa mbwembwe...wanataka mpaka mashuka yawe ya forever living.
Siwatofautishi sana na alovera maana nayo dah....wana mpaka malapa ya alovera kwendea bafuni eti wadudu wasichanganyike na sabuni.
Kinachoshangaza kwa nini serikali ipo kimya kwenye hili na nina uhakika wanaijua mechanism yake?
Kinachoshangaza kwa nini serikali ipo kimya kwenye hili na nina uhakika wanaijua mechanism yake?