Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Mkuu Laki si pesa jaribu kunipa uelewa wako kuhusu hawa Forever

Ni hivi ukisha jiunga kuna mjanja atalipwa laki mbili kwa kujiunga kwako ndo maana wanakufata fata sana na baada ya wewe kujiunga ukifanikiwa kumshawishi boya mwengine akajiunga unapewa laki mbili. kila utakaemshawishi akajiunga utapewa laki mbili yaani ni jitihada zako tu za kusaka mbululazz ili wajiunge nawe uzidi kupata laki mbili mbili huku ukiuuza Bidhaa uchwara zenye nembo ya f living
 
Aiseeee!! hivi kumbe huyu Dada ananidharau kiasi hiki😡? ngoja aje tawawekea mguu wake nimeuvunja hapa!
 
Aiseeee!! hivi kumbe huyu Dada ananidharau kiasi hiki😡? ngoja aje tawawekea mguu wake nimeuvunja hapa!

Sio dharau ni bizness kwani wee laki mbili unaona ndogo?? Pia ukijiunga wewe pia unakuwa sehemu ya soko kwasababu huwezi uza Bidhaa usizotumia hivyo kampuni itanufaika kwa wewe kuwa consumer pia kama utafanikiwa kushawishi watu watano wakajiunga utapata 1 million, bado waona ndogo?
 
Cheki Hapa wanavyojibaragua
 
Attachments

  • 1432814250283.jpg
    1432814250283.jpg
    72.5 KB · Views: 390
Sio dharau ni bizness kwani wee laki mbili unaona ndogo?? Pia ukijiunga wewe pia unakuwa sehemu ya soko kwasababu huwezi uza Bidhaa usizotumia hivyo kampuni itanufaika kwa wewe kuwa consumer pia kama utafanikiwa kushawishi watu watano wakajiunga utapata 1 million, bado waona ndogo?

Duuu!! yaani alikuwa tayari hata kunitoa..........ili tu nijiunge kwa alivyovuga ananijali😱
 
Kwa wale wote wanaohitaji biashara ya haraka haraka na bila mtandao wala nini, ni bidhaa ambayo kila mtu anaihitaji kwa wakati mmoja au mwingine, ni bei rahisi na ni bidhaa nzuri ambayo imewasaidia wengi. Ni bidhaa moja inyotatuwa matatizo mengi sana kwenye ngozi.

Unanunuwa kwa bei ya jumla unauza rejareja na faida unabaki nayo mwenyewe. Hakuna longo longo, hakuna mtandao, hakuna kushindwa.

Pitia hapa kwa maelezo zaidi:

https://www.jamiiforums.com/matanga...ural-unaolainisha-ngozi-sasa-unapatikana.html

https://www.jamiiforums.com/jf-doct...na-zaidi-aunt-zainabs-natural-super-clay.html
 
Achana na forever living. Jiunge na trevo product. Wana product moja ambayo wanauza na rahisi kuuzika tofauti na foreve ambayo Ina products Nyingi na kuwachanganya customers. Trevo imemsaidia wengi niliowapa product hii. More details kuhusu trevo check www.trevocorporation.com/coach/Abella na simu 0767632212

Unasoma makala unakutana na msamiati unaenda kwenye kamusi katika maelezo ya msamiati huo unakutana na msamiati mwingine.
 
Wadau mwenzenu nimekuwa nafuatwa na watu wa Forever Living tena kwa mialiko mithili ya kadi za harusi. Kwa muda sasa naletewa vipeperushi na baada ya kuona siitikii wito imefikia hatua wanatumwa mabinti kuniletea hiyo mialiko. Tatizo kubwa ambalo limenifanya kuwa mzito kuitikia huu wito ni Uzi uliowahi kuletwa hapa jamiiforum ambapo wachangiaji wengi walionyesha wasiwasi na hii kampuni. Juzi nililetewa na Dada mmoja kitabu cha watu mbalimbali waliojiunga Forever na kupata mafanikio makubwa hadi akili ikawa kama nimepigwa ganzi na hadi sasa huenda nikajiunga lakini kabla ya kujipeleka huko naomba ushauri kwa mara ya mwisho.

Wameandika hao watu wamekumbana na mafanikio baada ya muda gani?
 
Fanya utafiti kabla ya kufanya maamuzi. Ingia kwa mitandao na uliza watu wanaofanya na kufanikiwa ndipo utapata majibu. what if ukaamua kuacha kuiacha wakati pengine ingekufaa au kama isingekufaa. ushauri wa bure ni kwamba fanya utafiti mwenyewe na fanya maamuzi mwenyewe.Tatizo kubwa wengi hawawezi kufanya tafiti wenyewe na kufanya maamuzi wenyewe. Na wengi hufanya maamuzi kwa kufuata mawazo ya wengine yaani opioni za wengine na siyo facts. Huyo anayekwambia uache kampuni hii na ingia hii naye pengine anakupotosha ushari sahihi angekwambia kuna kanuni za kuchangua makampuni wa mitandao kama unataka kuifanya biashara hii. ingia kwa mtandao andika how to choose networking marketing companies utapata vigezo hapo na usifuate opinion za watu bali facts. Maandiko yanasema watu wangu wanapotea kwa kukosa maaalifa. na wewe usiwe mmoja wao. Pia nashauri tafuta washauri wa biashara watakupa ushauri huru. waweza nipigia kwa 0689 41 74 72 nitakupa maelezo zaidi. maaana wengi hapa ndani inaonekana kushauri wasiyo yajua.
 
Forever Living ipo nchi nyingi ila iyo ya kujiunga na kulipa laki mbili ndio naisikia leo (chezea bongo ) kwengine kujiunga ni bure ila mtu anakua anapata seeds.

Aiseeee!! hivi kumbe huyu Dada ananidharau kiasi hiki😡? ngoja aje tawawekea mguu wake nimeuvunja hapa!
 
Habarini wadau.

Ninaelimishwa Sana na mada zijadiliwazo humu ndani. Leo natamani kuelimishwa kuhusu membership za kampuni za gnld, forever living na nyinginezo Kama hizi.

Ni Mara ya tatu sasa wanakuja kwangu na ushawishi mkubwa kwamba kampuni hizi zitanipa faida kubwa yaani nitatoka kimaisha.

Sina wasiwasi na products zao nna wasiwasi na mafanikio makubwa wayapatao wanachama kwa kadri uongezavyo watu. Wasiwasi wangu sasa ni huu; hakuna uhusiano wa kampuni hizi na free mason? Mbona hatusikii zikijitangaza kwenye vyombo vya habari?

Kama kuna faida kubwa kuwa huko mbona basi watu wasiache ajira zao na biashara zao na kujiunga na kampuni hizo? Msaada jamani. Pesa naipenda ila zina mipaka yake
 
Waliofanikiwa zaidi wameacha ajira zao na wengine bado wanaendelea. Kuna mwengine anaona hela anayoingiza forever ni zaidi ya mshahara wake ameona bora aache ajira yake nakujikita na busness. Hela ipo lakin u have to work hard especially katika ku recruit watu, hiyo team yako lazima ifanye kazi coz isipo fanya kazi jihesabu huna chako. Ukiwa na team inayojituma hayo mafanikio makubwa utayaona. Ni busness nzuri lakini ni lazima uwe committed, sisi wengine commitment ilitushinda.
 
Ndio tatizo la watanzania, wewe umefundishwaaaaaa....halafu unakuja kuomba ushauri huku kwa wati wasioijua. Kwanini maswali haya hujawauliza waliokuwa wanakuelimisha?. Halafu unapouliza Freemanson, wewe mwenyewe kwanza unawajua Freemanson ni akina nani?. Kufanikiwa au kutokufanikiwa kwa mtu inategemea akili na fikra zake mwenyewe. Badilisha kwanza mtazamo wako halafu utajua biashara hii ni kweli ama siyo kweli. Lakini pia biashara ya FOREVER ama nyingine yeyote hulazimishwi..ni wewe mwenyewe kuikubali ama kuikataa. Usipoteze muda wako mwingi kuuliza humu ndugu. Kama huwezi acha, si lazima ufanye biashara hii ama nyingine yeyote.
 
Back
Top Bottom