Naona kuna watu wengi humu wanaongea wasichokijua Ngoja nijaribu kujibu baadhi ya comments nilizoziona humu kwa kadri ya uelewa wangu.
1.Nimeona watu wanapoteza hela
Hii ni biashara kama nyingine Ni kweli kuna watu wanapoteza hela hata mimi nimeona watu wanapoteza pesa kwenye biashara ya duka, daladala, taxi n.k nimeshuhudia baa kubwa na nzuri Kinondoni na hata sinza lakini hazina wateja.
2.Ni utapeli
Kwa kampuni halali iliyosajiliwa huwa hamna utapeli. Jambo la muhimu unapofanya biashara yoyote mtandaoni chunguza kama hiyo kampuni iko regulated yaani kuwe kuna taasisi zinaisimamia. Iwe unafanya biashara ya forex, unanunua mzigo online, iwe betting n.k. kwa mfano Alliance ana Leseni ya Tanzania na nchi mbalimbali ambazo anafanya biashara, pia yuko regulated na MLMIA, Phillipines chamber of commerce, DSAP, SGS, FDA HSA na kadhalika. Epuka kampuni ambayo haiko regulated.
3.Wanajifanya wana hela
Ni kweli wako ambao wanaona ili wakushawishi kuwa hii biashara inalipa basi waigize kuwa wao wenyewe ni mambo safi. Huku ni kutojiamini sio lazima mimi niwe tajiri ndipo na wewe uamini kuwa utafaidika naweza kukuonyesha njia (na hasa pale ambapo na mimi ndio naanza) wewe ukafanikiwa na mimi nikakwama. Naweza kuwa na kitambi lakini nikakufundisha kutengeneza six packs.
3.Ni biashara ngumu
Well kama zilivyo biashara nyingine lazima uweke juhudi. Kama una mawazo kwamba hii ni pesa ya bure bure huwezi kufanikiwa na bahati mbaya baadhi ya waelimishaji wanapotosha kwa kukuambia ni rahisi tu wewe tafuta watu wawili hao wawili walete wawili na hao pia wataleta wawili basi mtandao wako utakuwa mkubwa. Nikuambie ukweli hao mamilionea wana mtandao mkubwa sana wanatumia websites, facebook insta na kila mitandao kutangaza biashara. Wanafanya semina mkoa kwa mkoa na nchi kwa nchi ili kutangaza biashara. Mimi nafamihana kwa ukaribu na mmoja kati ya members waliofanikiwa Alliance yeye akaunti yake ana watu hadi Rwanda Kenya Uganda n.k ukiwa na wanafunzi mkoani ukaandaa semina anafunga safari anakuja kuwafundisha.
4.Wananufaika waanzailishi
Hiyo naamini ina ukweli kiasi ukiwa juu una nafasi zaidi ya kukuta wanaojiunga chini wanakuwa wanakunufaisha, hata hivyo bado swala la juhudi binafsi linahusika yaani sio tu ujiunge halafu uwe dormant halafu utegemee matunda. Hii ndio imenifanya hata mimi nichague Alliance japo nilikuwa nawajua Forever GNLD Trevo n.k Alliance kwa bongo bado ni ya motomoto.
Mwisho Kwenye maisha usiangalie waliofeli angalia waliofaulu. Aliyefail hawezi kuwa role modal wako na iko wazi siku zote kuwa wanaofeli ni wengi kuliko wanaofaulu. Masikini ni wengi kuliko matajiri, wanaothubutu ni wachache kuliko wanaoogopa na kupiga porojo. Be yourself!