Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Enos Salema
Enos+Salema.jpg

Jamaa namkubali sana nilipiga nae kazi vodacom jamaa mshiko anao maana kanunua gari Discovery4 mpya pale posta na pia ana ghorofa moja na yupo around 30yrs....FLP Daima.
atakuwa alikuwa anauza bwimbwi...
 
Wajinga ndio wanaoliwa...
Kuna mwalimu na mentor wangu nilikuwa namheshimu sana, but alipoanza hii biashara nikamwambia no... nikaona anaendeleza ushawishi tena kupitia kwa mke wangu, ilibidi ni mbwatukie.
Bidhaa za elfu 2 wanauza laki 3, ili tu wakajenge maghorofa... Upuuzi mtupu...
 
SORry lkn! mbona wengi wao ni wahaya lkn? maana walikuja hapa arusha last month GOLDEN rose nikaambulia wine ya alvera bt nikawa mgumu mpaka leo wananitongoza

Hawa watu ni waongo. Kila kitu wanaweka rangi ya kijani alafu wanadanganya kina aloe vera... Aloe vera my foot
 
kiukweli hawa jamaa siwaelewi nawasikia tu, mtu anayewajua vizuri anisaidie
 
Mimi naweza kukwambia kua ni coy ambayo inahitaji sana watu kwaajili ya kusambaza bidhaa na kuwaelimisha watu wajiunge.
Ni biashara nzuri kama ukiamua kuifanya ,
inaitaji kujiamini pia huwa wanatoasemina kuwezesha members wao. ila japo wengine wanaiponda sana.
kama unataka kuingia tafuta kwanza network yako(watu wako ambao utawaingiza) ili upate faida.
 
Kuna nyingine inaitwa Ori-Flames......Upuuzi mtupu..Wapo wengi hata JF ngoja waje..

Dah usinikumbushe hawa watu mkuu, niliwahi kuingia mkenge nikaenda kununua product zao pale Mkapa tower, zilichonifanya sitaki hata kuwasikia.
 
Niko kwenye seminar ya forever living, maoni yenu wadau
 

Attachments

  • 1404833445040.jpg
    1404833445040.jpg
    67 KB · Views: 610
Kunywa hizo dawa ili uishi milele huo ndio ushauri wangu
 
Pyramid scheme... Upatu, aka deci, aka mchezo aka chezo

wajinga ndio waliwao
 
Ukijiunga jiandae kukimbiwa na ndugu na rafik mana kila ukikutana nao itakuwa kuwashawish wajiunge
 
Ni vema kuwa na watu wanaojadili fedha nyingi kukutia moyo kuwa inawezekana ukiweka bidii, kuliko kutumia muda mrefu na watu waliokata tamaa. Haya mambo yanambukiza ndugu yangu.
 
kuna mtu mmoja anaitwa robert hapo, achana nao mi nawajua hao
 
Ukitoka njoo na Ubungo Plaza, kwenye mkutano wa GNLD..
Kesho kutwa tutakua Millenium Towers kwenye mkutano wa Oriflame.....KARIBU
 
Back
Top Bottom