Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

uko unaweza kushangaa unang'ang'aniwa na warembo kama wote wanataka uwabless. usipokaa sawa unaweza kukojoa adi ubongo
Na kwa tabia yangu lazima niwabless. Basi ukikuta ninatype vitu vya hovyo hovyo humu ujue nimemwaga ubongo wote na kwamba kichwa kimebaki kama kopo tupu.
 
Kuna Paul misalaba wa namanyire nkasi

Golgota magabe wa shinyanga

hao huwa wakosekani ktk kipindi Cha ddw matangazon ya mchana kutoa kero au kupanda katka jukwa la manufa
Golgota magabe na filbert kyauke 🤣🤣🤣😂
 
Hao wa zamani walikuwa watu wazima na maisha yao safi tu mfano huyo Muhiri Obare wa Igoma,Mwanza.
 
Miaka imesonga sana, maisha yamebadilika Kwa kiasi kikubwa.Tofauti na sasa ambapo ukiwa na simu janja au tarakirishi unapata taarifa zote zilizotokea na zilizovunjika 'breaking news', Zamani redio ilikuwa chombo muhimu ktk kupata taarifa na burudani.

Leo nimewakumbuka wale watuma salamu maarufu enzi zile,ingawa hata sasa wapo baadhi ya watu ambao ni maarufu ktk vipindi mbalimbali ukisikiliza redio km Clouds mfano kuna heri dereva babaji, shangwe dereva babaji, Daudi wakota n.k

Enzi hizo ukisikiliza kipindi cha mirindimo asilia na Malima Nderema au salamu Kwa wagonjwa, kuna majina maarufu huwezi kuacha kuyasikia wakati wa kutuma salamu.

Kuna huyu jamaa wa kuitwa Wajadi fundi Wajadi binadamu mashaka, yeye kila siku yupo safarini kuelekea mahuta shimoni, fundi Khamisi full migebuka wa mwandiga fashion sokoni Kigoma.

Lawena Msonda Baba mzazi kutoka chunya Mbeya.

Ally Mrangi Gigiri Mresa yeye mar kila siku yupo safarini kuelekea mabibo Dar es Salaam.

Zakaria Ndemfoo, Issa Mzee wa urembo kutoka Moshi. Lupa tingatinga "mdau asiyechuja" ndiyo ilikuwa slogan yake bila kumsahau Chesko Mzee wa matunda kutoka Africa Sana.

Kuna mdau akiitwa Limonga Justine Limonga na kuna huyu mama Abuu wa majani mapana. Kuna jamaa aliitwa Fikiri Dario Gakala wa GGM Geita na Filbert Kyenshambi kutoka Muleba-Nshambi, wapo wengi sn na tulikuwa tunaenjoy sana Enzi hizo

Unawakumbuka baadhi? Unazikumbuka kauli mbiu zao maarufu zilizotamba?
Lawena Msonda natamani kumjua,amesumbua sana mpaka sasa.
 
Back
Top Bottom