MNEC Mlao amkaanga Tundu Lissu, asema ni mpotoshaji

sasa kamkaangaje hapo kwa mfano
 
Hao n'gombe wanaokoywa au wanagawiwa bure
 
Hata kama sisi ni wapinzani tuongee facts na sio kukwepesha maana tukizani kuidanganya jamii chama kilicho madarakani imevuruga ili kuzoa kukubalika hiyo haifai, sio yote rais wetu kaharibu ana mazuri yake, wananchi wana uelewa na elimu tosha nyakati hizi mtu anajua hapa unamdanganya au hapa upo sahihi
 

..Ccm kweli wameishiwa.

..hizo ndio hoja zao kuhusu Katiba Mpya?

..vipi kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi Ccm wana mapendekezo gani?
 
Sasa huo ndio upotoshaji ....
Tunaangalia ratio ya kupanda kwa bei hizo. Maharage kuwa 3000 kwa quality ni sawa na bei ya nyama iliyopanda pia hadi 9000. Maharage inapaswa kuwa chini na siyo ghali kiasi hiki. Naona bado hakuna ambaye anaweza kuchambua pointi za Lissu au Mbowe.
Tupe caption tuone huo mkutano wake mkubwa wa hadhara.
 
Hamna mnaloweza kulifanya labda wizi.
 
Kwahiyo mnajivunia kilo ya maarage kuwa elfu nne?

..hata mimi nawashangaa Ccm.

..wao wanatetea mfumuko wa bei na bidhaa muhimu kama nyama na maharage kuuzwa kwa bei inayoumiza Watz walio wengi.

..Kinachojidhihirisha na kwamba Ccm kimekuwa chama cha mabwanyenye na wanyonyaji, na sio chama cha wanyonge na watu wa kawaida.

..Ukisikiliza hoja zao na kutizama mienendo yao hutashindwa kubaini hilo.
 
Kwa hyo CCM wanakataa kwamba nchi hii hakuna mfumuko wa Bei ?

Ufike wakat CCM iwe na huruma na wananchi wake kila mtu anaona Hali ilivyo mtaani


Tanzania n ya 3 kwa kuwa na mifugo mingi Africa lakn Bei ya nyama n kaa la Moto kwa Sasa SS wengne tunashindia vichwa vya mbuz na utumbo tukitaman nyama kwan nyama n ghali

Unga wa ugal upo juu maharage yapo juu lkn CCM wanakataa kwamba Bei ya vyakula IPO sawa

Rais wetu alipandisha Bei ya vitu kwa mdomo wake lkn hakuna aliyempinga au kumkosoa eti kisa rais hakosolewi
 
Hawa Chadema malaghai sana, yaani yaliambiwa kilo ya nyama na maharage ni 9000, yakashangilia, halafu linaelekea nyumbani, linatoa 3000 kununua kilo ya maharage.
basi toa hiyo afutatu ununue kilo ya nyama
 
Wenye akili ndogo wataelewa wapi haya mkuu? Hawa waNEC wa kubebwa ndo utegemee watoe ufafanuzi kama huu wa kwako? Hapa eti kamkaanga Lissu.
[emoji3][emoji3][emoji3],hapo eti ndio kamkaanga Lissu,yaani hawa ni Chawa tu tofauti ni majina tu,sijui MNEC mara DC ni machawa tu
 
Huyo MNEC ni mtupu kichwani.Lissu ameongea kisaikolojia zaidi.hakumainisha kama anavyotafsiri yeye.ujumbe wa Lissu ni kwamba bei ya nyama na maharage hazitofautiani sana pia akimainisha hali ya maisha imepanda sana na inaendelea kupanda.uwezo wa pesa yetu kununua vitu ni mdogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…