MNEC Mlao amkaanga Tundu Lissu, asema ni mpotoshaji

Kwa hiyo kasikiliza hotuba nzima ya TAL akaona hoja ni maharage kufananishwa na nyama hadi akaandaa na hotuba ya maharage na nyama kuwa na utofauti wa bei? Hivi kweli hawa chawa ndivyo waliyokubaliana kukomaa na vitu vya kitoto namna hii?
Tobia Mhusika mkuu, toboa, wapashe hao majizi
 
MNEC MLAO AMKAANGA TUNDU LISSU, ASEMA NI MPOTOSHAJI.

Alhamisi, Jan 26, 2023.
Misungwi, Mwanza.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Cde Ramadhani Mwinshehe Mlao (MNEC) amewasili Jijini Mwanza akitokea mkoani Shinyanga ambako amekuwa na muendelezo wa ziara Kanda ya ziwa kuelekea katika maadhimisho ya miaka 46 ya CCM na kupokelewa na wanachama wa chama cha mapinduzi katika ofisi za CCM mkoa wa Mwanza.

Katika ziara ameweza kufika wilayani Misungwi ambapo kupitia mkutano mkubwa wa Hadhara MNEC Mlao amempongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Kazi anayoendelea kufanya kuhakikisha watanzania wanapata maendeleo lakini pia amekemea vikali wanasiasa wanaopotoshaji na wanaosema uongo juu ya kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia ambapo amesema;

"Yupo mtu mmoja jana kafanya mkutano wa hadhara pale Dar es Salaam na waziwazi amewadanganya watanzania kuwa bei ya kilo ya Nyama na Maharage ni sawa Tanzania kitu ambacho ni uongo sote tunajua bei ya nyama kilo ni Tsh 8000-9000 huku Maharage bei ni Tsh 3500-4000 hapo tunaona utofauti mkubwa hivyo mtu huyu anapaswa kupuuzwa kwa upotoshaji huo"

Aidha MNEC Mlao ameweza kushiriki katika zoezi la upandaji miti katika Hospital mpya ya wilaya ya Misungwi sambamba na kupandisha Bendera katika Shina namba tano kata ya Misungwi na kuzungumza na mwenyekiti wa shina Ndgu Juma Malangu ambapo amemshukuru sana MNEC Mlao kwa kuthamini na kutambua kazi kubwa ya chama inayofanywa kwenye mashina ya CCM.

Pia MNEC Mlao amesisitiza wanachama wa chama cha mapinduzi kuelekea maadhimisho ya miaka 46 ya CCM kuendelea kukijenga chama katika maeneo yao yote na kuwajuza kuwa uimara wa CCM utatokana na namna ambavyo tutaendelea kufanyakazi za chama kwa kujitolea vyema kuhakikisha idadi ya wanachama inazidi kukuwa sambamba nakufuatilia vyema utekelezaji wa ilani.

#MimiNiNyinyi

Imetolewa na:

JOSHUA KANDUMILA.

KATIBU WA UVCCM MKOA WA MWANZA.

View attachment 2496588
View attachment 2496589

Mnec hujui hesabu.
Tukueleweshe mahesabu yalivyo
1. Kilo ya nyama ni Tsh 10,000 ambapo ilikuwa 7,000 awali Tofauti yake ni 3,000
2. Maharagwe yalikuwa 1,500 sasa ni 4,500 kwa kilo . Tofauti yake ni Tsh 3,000

Sasa kwa mahesabu hayo bei ya nyama na maharagwe ni SAWA
 
Angalia dakika ya 1:22 huyu mzee anamsikiliza MNEC kimoyo moyo atakuwa kampa tusi la nguoni kabisa yaani

kilo ya nyama.PNG
 
Nyie ndio mliovuruga. Tuna ng'ombe wengi, hivyo bei ya nyama ilitakiwa iwe kilo 1 ni tsh.4000. Hamjamsoma Lisu vizuri, hapo mnaingia kwenye 18 alioitaka ili abutue mpita vizuri. Sasa hiyo iliyotakiwa kuwa bei ya nyama ndio bei ya maharage mpo apo. Hii bei ya tsh.9000 mpaka 10,000 siyo bei halali, bali ni ulanguzi. Nayo mnataka kusingizia vita ya Ukraine na Urusi? Wakati mifugo tunayo
Huyo ng'ombe wa kuuza nyama yake kilo elfu 4 labda Zanzibar
 
MNEC MLAO AMKAANGA TUNDU LISSU, ASEMA NI MPOTOSHAJI.

Alhamisi, Jan 26, 2023.
Misungwi, Mwanza.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Cde Ramadhani Mwinshehe Mlao (MNEC) amewasili Jijini Mwanza akitokea mkoani Shinyanga ambako amekuwa na muendelezo wa ziara Kanda ya ziwa kuelekea katika maadhimisho ya miaka 46 ya CCM na kupokelewa na wanachama wa chama cha mapinduzi katika ofisi za CCM mkoa wa Mwanza.

Katika ziara ameweza kufika wilayani Misungwi ambapo kupitia mkutano mkubwa wa Hadhara MNEC Mlao amempongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Kazi anayoendelea kufanya kuhakikisha watanzania wanapata maendeleo lakini pia amekemea vikali wanasiasa wanaopotoshaji na wanaosema uongo juu ya kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia ambapo amesema;

"Yupo mtu mmoja jana kafanya mkutano wa hadhara pale Dar es Salaam na waziwazi amewadanganya watanzania kuwa bei ya kilo ya Nyama na Maharage ni sawa Tanzania kitu ambacho ni uongo sote tunajua bei ya nyama kilo ni Tsh 8000-9000 huku Maharage bei ni Tsh 3500-4000 hapo tunaona utofauti mkubwa hivyo mtu huyu anapaswa kupuuzwa kwa upotoshaji huo"

Aidha MNEC Mlao ameweza kushiriki katika zoezi la upandaji miti katika Hospital mpya ya wilaya ya Misungwi sambamba na kupandisha Bendera katika Shina namba tano kata ya Misungwi na kuzungumza na mwenyekiti wa shina Ndgu Juma Malangu ambapo amemshukuru sana MNEC Mlao kwa kuthamini na kutambua kazi kubwa ya chama inayofanywa kwenye mashina ya CCM.

Pia MNEC Mlao amesisitiza wanachama wa chama cha mapinduzi kuelekea maadhimisho ya miaka 46 ya CCM kuendelea kukijenga chama katika maeneo yao yote na kuwajuza kuwa uimara wa CCM utatokana na namna ambavyo tutaendelea kufanyakazi za chama kwa kujitolea vyema kuhakikisha idadi ya wanachama inazidi kukuwa sambamba nakufuatilia vyema utekelezaji wa ilani.

#MimiNiNyinyi

Imetolewa na:

JOSHUA KANDUMILA.

KATIBU WA UVCCM MKOA WA MWANZA.

View attachment 2496588
View attachment 2496589
Wilbroad Slaa ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa Chadema kabla ya kurejea CCM, ameisifu hotuba ya Tundu Lissu aliyoitoa Temeke huku akidai kwamba imegusa penyewe hasa.

Amedai kwamba kitendo cha Lissu kuzungumzia ugumu wa maisha na kupanda kwa bei za vyakula kwa kiwango cha kutisha kama bei za sasa ni jambo la muhimu sana , ambalo linagusa jamii yote ya Kitanzania wakiwemo Polisi , ambao amesema hawana masoko binafsi ya kununua mahitaji yao ya vyakula , bei ikipanda hata polisi wanasota , amesema kwamba bila wananchi kushiba huwezi kuwaeleza kuhusu SGR wala Madaraja maana hawatakuelewa .

Dr Slaa pia amesifu muunganiko wa Hotuba ya Lissu na Mbowe na hasa baada ya Mbowe kurudisha suala la Katiba kwa wananchi kwa kutaka wajiorodheshe kwa majina yao kwa kila mtaa .

Amesifu lugha iliyotumika kwenye Hotuba hiyo , akidai kwamba ni lugha ngumu ambayo ilibidi kutumika ili kufikisha ujumbe , japo amedai pamoja na ugumu wake hakuna maadili yaliyokiukwa

Kwa ujumla Dr Slaa ameona fyucha ya Chadema katika mtazamo Chanya , ambao anasema kuna dalili ya Chama hicho kutwaa madaraka 2025
 
Huyo ng'ombe wa kuuza nyama yake kilo elfu 4 labda Zanzibar
Kama umeme iliwezekana kuunganishiwa kwa tsh. 27,000 kwa nini unashangaa bei ya ng'ombe waliopo humu ndani ya mipaka yetu kuuzwa 4000/=kwa kilo ya nyama. kinachotakiwa ni kuweka sera wezeshi.
 
Hivi huu UNEC sikuhizi umekuwa ni utaita flani naona wanajitutumua wanaanda mapokezi hadi Ma RC wanawatetemekea.
Wa NEC wa sasahivi wana hekaheka sana ila nimegundua wengi wao wanafukuzia ubunge hawana lolote

Wabunge hawafanyi Kazi zao majimboni, wanasubili kwenda bungeni kugonga meza wachukue Posho, muda ukiisha waludi majimboni kuomba kura , WANEC hawana posho tuwaache wenye uchungu na Nchi wawasaidie wabunge kufanya kazi
 
Zipo juu kitokana na sera mbovu. Utazunguka mbuyu, lakini chanzo kipo hapo
Nenda kale dagaa, siwezi kufuga n'gombe wangu kwa gharama kubwa, wewe umejikalia Dar es salaam ununue nyama kwa bei rahisi
 
Kwa hiyo kasikiliza hotuba nzima ya TAL akaona hoja ni maharage kufananishwa na nyama hadi akaandaa na hotuba ya maharage na nyama kuwa na utofauti wa bei? Hivi kweli hawa chawa ndivyo waliyokubaliana kukomaa na vitu vya kitoto namna hii?
Na hii ndiyo njia nzuri ya kuwaondoa kwenye reli unawapa hoja ndogo wanaikomalia lakini hoja nzito na fikirishi zinabaki bila kujibiwa mwisho wa siku tunafanya majumuisho.
 
Nenda kale dagaa, siwezi kufuga n'gombe wangu kwa gharama kubwa, wewe umejikalia Dar es salaam ununue nyama kwa bei rahisi
Tuludi kwenye Mada, Lisu hajapotoka. Kama bado kunielewa, rudia kusoma point zangu huko nyuma, tusihamishe magori.
 
Kwahiyo mnajivunia kilo ya maarage kuwa elfu nne?
NDIYO kwa sababu itawafanya msiolima mlime. Kwa nyinyi kununua kilo ya maharage TSHS 4000 sasa mkulima anapata bei ya 3000 kutoka 1500. CCM OYEE
 
Back
Top Bottom