You are conflating two different issues. Kutumia law fare kumuonea mtu si hekima. Ila kumuachia mtu baada ya shinikizo ni hekima. Kuendelea kumshikilia ndio kukosa hakima. Kugoma kutoka baada ya kuachiwa nako kutakuwa sio hekima.
Amandla...
Kuna kitu unashindwa kukielewa hapa.
CCM ni repeat offenders wa kutumia lawfare.
Hivyo, wanafanya hivyo kwa makusudi kabisa .
Lissu si mhanga wa kwanza na hatokuwa wa mwisho.
Wanasiasa wangapi hapa Tanzania wamekuwa wahanga wa lawfare?
Watu ambao wanatumia lawfare kama silaha dhidi ya wapinzani wao wa kisiasa, na wanaitumia si mara moja, mbili, tatu, wala nne, watu hao wana hekima gani wanapoamua kutokuendelea na hizo kesi za za kubambikia watu?
Au wewe safari hii ya Lissu kufungwa ndo umeyaona hayo matumizi ya lawfare?
Tena hata sasa hivi bado wanawakamata watu na kuwafungulia kesi za ajabu ajabu tu zisizo na kichwa wala miguu.
Halafu baadaye utasikia ‘Rais’ kawasamehe au mwendesha mashitaka kaamua kutokuendelea na kesi.
Yaani kila mara wakimwona mtu anahatarisha maslahi yao ya kisiasa, wanatumia sheria kumnyamazisha halafu baadaye wakiamua kutokuendelea naye, wewe unaona hiyo ni hekima?
Matumizi mabaya ya sheria yanayojirudia rudia miaka nenda rudi, wewe unaona ni hekima?
Unatetea kisichoteteeka Fundi!