Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Lissu alisema Mnyika alipeleka suala la Mbowe (na mengine) TCD kwa ajili ya kuomba ushirikiano wao katika dai kuwa kesi hizo zinastahili kufutwa kwa sababu ni za kisiasa. Mangula alipinga hoja yao kwa kusema kuwa kesi ya Mbowe ni ya jinai na sio ya kisiasa. Ndipo Mnyika akawakabidhi hayo makabrasha ya Mahakama ( committals) kuwathibitishia kauli yake kuwa ni kesi ya kisiasa na sio ya jinai. Hayo makabrasha ni public information kwa hiyo kila mtu ana haki ya kuyasoma. Na inaelekea alifanya hivi kwa maagizo ya chama chake. Nadhani CDM inatofautiana na Zitto kwenye yeye kutumia lugha ya kubembeleza ( kuomba ) kwenye kitu ambacho wao wanaona ni stahili yao. Kwa maneno mengine, hawataki Mwenyekiti wao aachiwe kwa hisani bali aachiwe kwa sababu ni haki yake.
Amandla...
Amandla...