Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Nilishangaa Jana kuona baadhi ya wanachama wa chadema baadhi wakijiapiza kuhama chama na wengine kuchoma bendera. Kwangu Mimi inanionyesha vile ambavyo wanafuata siasa za kuwafuata watu( politics of personalities) na siyo siasa za masuala( politics of issues) au instutionalized politics ukitaka.
Suala la watu kuasi alikuanza leo. Watu ni waasi kwa asili hivyo ukifuata watu badala ya kufuata itikadi au masuala utakuwa hujitendei haki...
Mdee na wenzake siyo waasi wa Kwanza. Au niseme siyo wasaliti wa Kwanza (Betrayers) kutokea duniani na hata kwenye vyama. Kama Mitume Kama Yesu na wengine walisalitiwa na bado wengine wakaendelea na itikadi zao,why kuona ajabu wakati huu.
Tuanze kufuata siasa za masuala tafadhali maana A natural human being is to greater extent susceptible to rebellion.
Rudini kwenye chama chenu maana taasisi bado ipo. Watu huja na kupita!!
 
Mkuu Chige ,binadamu timamu wa afya ya akili lazima ahoji hilo la Nusrat kutolewa mahabusu bila ya mahakama kuamua apewe dhamana na kwenda kuapishwa kesho yake.
Hapo ndipo inaonyesha jinsi tulivyo na mihimili mitatu isiyo na watu wenye akili ya kuweza kuandaa "mpango ovu" bila ya kuacha maswali.
Hili ni kweli mfumo umehusika,na mtekelezaji mkuu ni "0".
 
Hebu nisaidie hapa umeelewa nini mkuu na Mimi naona chenga tu hapa Siamini kabisa mkuu.
 
Mataga nakuonea huruma wewe ambaye unajua ukweli ila mahaba ya ccm yamekulevya hadi inabidi ujivue ufahamu.

Ni hivi, tarehe 27 kamati kuu ya chadema ikiongozwa na Freeman Mbowe inawavua uanachama hawa wasaliti 19 mnabaki nao kama wabunge wa mataga.
Baada ya hapo tutapata Trilioni 2 zetu au bila bila?
 
S Sijaona umamluki hapo.kama atakuwa amehusika mimi namuona atakuwa na busara sana halafu Mjanja. I can tel you hawa vitu maalum wataiganya chadema isife .anayeamini kuwa uchaguzi unaweza kurudiwa sijui anatumia akili gani kufikiri hivyo.
 
UVCCM mnajitahidi kweli, mnaanzisha uzi halafu mnaalikana kuchangia. Ina maana hamjasikiliza maelezo ya Mnyika leo, au mnataka chadema wakurupuke kila mmoja kutoa maamuzi ili mpate sababu ya justify uhuni mlioufanya wa kufoji fomu za hao kinamama?
They are joyful but in dis-ray.
 
Chadema hawatakaa wamsahau mh Halima Mdee aka Sauti ya Zege mwenyekiti wa Bawacha na mbunge wa viti maalumu mkoa wa Dar es salaam.

Sauti ya Zege jasiri muonesha njia.

Maendeleo hayana vyama!

Huyo hawezi kulinganishwa na akina Dk Slaa, Zito na Kitila waliondolewa na chama hakikutikisika
 
"Waliokwenda kuapa, hawakua na baraka za chama. Hakuna kikao chochote cha maamuzi ndani ya chama kilichokaa kuwapitisha. Wamejikusanya wenyewe na kwenda bungeni. Kauli aliyotoa Halima kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe aliwapa baraka, huo ni uongo. Mbowe ameitisha kikao cha kamati kuu tarehe 27 Novemba ili kuwahoji kwanini wamekiuka utaratibu wa chama, pamoja na kuwachukulia hatua.

Uhakika nilio nao, hao 19 walioenda kuapa, walishirikiana na ofisi za NEC, pamoja na bunge kughushi nyaraka za chama, kujiteua bila kikao na kujipeleka kwenda kuapa. Huu ni USALITI mkubwa. Wote 19 wanafahamu orodha haiwezi kwenda NEC bila kupitishwa na Kamati kuu ikiwa na saini ya Katibu mkuu na mihuri ya chama. Na mimi sijasaini wala Manaibu wangu. Sasa NEC watueleze hiyo orodha waliyopewa ina saini ya nani?

Kughushi ni jinai. Na ni jambo la aibu kama ofisi ya bunge na tume ya uchaguzi wanaweza kushirikiana na watu wachache ndani ya chama kufanya jinai ya kughushi kwa maslahi yao wenyewe. Naomba wanachama wa CHADEMA, mtoe maoni yenu ni hatua gani zichukuliwe dhidi ya akina Halima Mdee na wenzake. Maoni hayo yawasilishwe kabla ya kikao cha kamati kuu Novemba 27.

Ieleweke hawa sio wabunge wa Chadema. Ni wanachama wa Chadema walioamua kutumia mwavuli wa Chama kunajisi heshima zao na heshima ya chama chao. Chadema hatuwatambui. Ni wabunge wa viti maalumu kwa matakwa ya CCM, ni wabunge wa NEC na ni wabunge wa Spika Ndugai. Kwa ujumla CCM imeamua kujiundia kambi yake ya upinzani bungeni ili kuokoa Trilioni 2 za wafadhili zisipotee."

John John Mnyika, Katibu Mkuu wa CHADEMA, 25 Nov 2020, Kinondoni, Dar.!
 
Si- hasa, Kama upinzani utaitaka kuchukua dora, unaitaji mabadiliko ya kimfumo, uendeshaji na ki fikra
 
Inamaana unataka kusema kuwa wanawake wote 19 walienda kula kiapo bila hata mmoja wao kumwaga bosi wao? Dahh
 
Sawa kabisa. Kila kaya inautaratibu wake.
 
Sidhani kama katika hili kuna mtu wa kudanganywa.Macho yanaona na masikio yanasikia.
 
Soma kitabu cha Mh slaa,nyuma ya pazia .utagundua mchezo huuu hauitaji hasira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…