Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Hii ni changamoto kubwa kwa chama chetu CHADEMA. Maelezo ya Katibu Mkuu wa chama cha CHADEMA yameeleweka na kujibu maswali yote. Tunasubiri hiyo tarehe 27 November 2020 kusikia maamuzi ya chama.
 
CHADEMA jamani ni watu wa ajabu mnooo
Watu wake zao wameapishwa Jana lakini wakiwa live hapa wanajidai wamehujumiwa😁😁😁 Hivi kweli mke anavaa kwenda Kula kiapo bila makubaliano na mume?!
 
Jana nilishangaa kuona mahali baadhi ya wanachama wa Chadema wakichoma bendera na wengine kadi za uanachama.

Mantic ilikuwa ni kuonyesha hasira dhidi ya wabunge walioenda kuapa. Na wengine walisikika wakisema chadema tena basi, kwa maana ya kuachana na Chadema.

Bila kuingilia undani wa Jambo ( maana bado vikao vya chama vinashughulikia Jambo hilo), upande wangu naona bado hatujui siasa za masuala( politics of issues or instutionalized politics) badala yake tunashabikia Sana watu( politics of personalities).

Kwa nini kuacha imani yako ya kisiasa eti kwa sababu tu mtu fulani kasaliti?

(Nimesema bado hatujui Kama kweli Kuna usaliti kutoka kwa akina Mdee, maana tunasubiri conclusion ya vikao vya chama). Lakini hata Kama wangesaliti Cha ajabu ni kipi? Mwanadamu yeyote kwa asili ni msaliti.

Kama tunataka kujenga taasisi za kisiasa zenye maana, lazima mwelekeo wetu iwe itikadi na siyo watu. Ndiyo, kumfuata mtu ni sawa wakati hajakengeuka,akikengeuka kwa nini uache malengo yako yalikupeleka kwenye taasisi hiyo kwa sababu ya uasi wa mtu maarufu?

Tutakuwa hatujitendei haki kukumbatia dhana ya kufuata watu vyovyote (following leaders unpurposely).

Watu hubadilika na ufuata wengine maslahi yao wakati fulani.

Hao wanaosemwa kuasi au kusaliti( kumbuka haijathibitishwa) hata Kama ndivyo, wao hawatakuwa wasaliti wa Kwanza ( Betrayers) hapa duniani na hata kwenye siasa zenyewe.

Mitume wa Mwenyezi Mungu walisalitiwa pia, bila Shaka kwa mfano, Tunamkumbuka yuda iskariot. Kama Mitume wamesalitiwa sembuse watu kusaliti chama au taasisi fulani?

Lakini huoni hata baada ya uasi wa watu wakiacha imani zao.

Siasa ni itikadi, Kama itikadi ipo na Kuna watu wanaifuata bado kwa nini watu no matter umaarufu wao wanakukatisha tamaa?
Narudia kwa msisitizo A natural human being is to greater extent susceptible to betrayal. Kama kweli mlifuata itikadi rudini mjenge chama chenu.

Maana wanadamu huja na kupita lakini taasisi hubaki.

Na kwa style niliyoona ya watu kuhama chama kwa sababu ya makosa ya watu maarufu, bado tuna la kujifunza. Tufuate siasa za masuala na siyo kuwa kondoo wa kuchinjwa wa wanasiasa.

Wasalaam.
 
Hakuna tena kitu au chama kinacho itwa chadema.
eti chama kikuu cha upinzani nchini!!! loo!!!Halima mdee Oyeee!! mwenyekiti wa umoja wa wanawake oyeee!! Tanzania kwanza vyama badae.
Ukiwa ambiwa toa ela ya mafuta unakiambia
 
Ndugu zangu, leo Katibu mkuu wa CHADEMA, Mh. Mnyika amejitokeza mbele ya waandishi was Habari na kusema wazi kwamba Chama hicho hakijawasilisha NEC orodha ya majina ya wabunge wa viti maalum kwa ajili ya kuapishwa! Kwamaana hiyo anatuambia orodha ile ni feki.

Lakini naomba tutumie akili zetu vizuri kuwaza na kuhoji. Wale walioenda kuapishwa sio watu wadogo, ni makada kindakindaki kuliko wengi wenu humu mnaokomenti, wanakijua chama kuliko ninyi, ni wajumbe wa vikao vikuu vya chama, kama kweli orodha hiyo ni feki inamaana wao ndio wameifoji? Siamini na haiingii akilini eti Mdee, Matiko na Bulaya na MAKAMANDA wale wengine wajiendee tu kuapishwa bila ruhusa! Na hapa nazungumzia ruhusa ya Mwenyekiti Mbowe! Naamini Mbowe amebariki wale wabunge wakaapishwe

Naamini amebariki kupeleka majina yale! Kweli kabisa Mdee na akina Matiko na Bulaya wajiamulie maamuzi haya makubwa namna hii? Hapana, Mwenyekiti ameamua kukinusuru chama kwa kuwaambia waende bungeni, liwalo na liwe! Chama kinahitaji kufanya siasa, na yeye anajua madhara ya kufanya siasa bila ya kuwa na wawakilishi bungeni! Chama kinahitaji ruzuku, ruzuku ni sawa na damu ndani ya mwili wa mwanadamu, bila damu kifuatacho ni kifo! Mbowe amekinusuru Chama kisife!

Mbowe amefikiria sana, hawa wapiga kelele kwenye Mitandao ni wanafiki, kura hawapigi, maandamano hawataki, kadi zao hawalipii ili kupata mapato ya chama! Wao kazi yao ni makelele tu! Wenzake wamemkimbia, eti wametishiwa maisha, wanasubiri Mbowe akijenge chama 2025 warudi waje wagombee, kwao wao chama kikipotea watahamia kwengine, Mbowe amepiga hesabu zake vizuri! Akipata ruzuku na wale wabunge 20 wakikatwa kila Mbunge mil 1.5 kwa mwezi, basi angalau hata hela ya kujaza mafuta gari ya Mwenyekiti kufanya siasa za chama zitapatikana!

Haya matamko ya Mnyika na Lisu ni Maigizo tu na Naamini Muda wao umewadia!0000
 
Endapo chadema haitawafukuza hao wabunge walionunuliwa na CCM kwa njia haramu za kishetani itambue kuwa inaenda kufariki kifo kibaya itabakia kuwa kama TLP NCCR na CUF ya Lipumba
 
Wanawake wenu wameamua wenyewe kuunga mkono juhudi za Rais mkuu
Kwani huo uhuni umefanyika wapi na nani?
🙄Kwa hiyo Nusrat alijaza form wap na aliapa mahakama gani..??
 
CHADEMA jamani ni watu wa ajabu mnooo
Watu wake zao wameapishwa Jana lakini wakiwa live hapa wanajidai wamehujumiwa😁😁😁 Hivi kweli mke anavaa kwenda Kula kiapo bila makubaliano na mume?!
Kuna ujumbe wenu wanawake Dr Bagonza anao...
 
Makosa mliyoyafanya yanawafanya muhangaike kila siku na Chadema yetu karata zenu hamkucheza vizuri
Ona sasa mnafanya uhuni live bila chenga kuwapata Viti maalumu...🤭
Makosa gani.Hivi nyie chadema mngeibiwa kura mngeshindwa kwenda mahakamani. Acheni kujifariji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…