Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Chama sio biashara binafsi. Huwezi kufukuza watu kwenye chama kwa kigezo cha hisia tu....

Tumia akili yako hata kidogo basi. Umeambiwa utaratibu wa chama haukufuatwa kama ndivyo uhalali huo unataka wapi? Hapa ni ile haki ya kusikilizwa ndio inayofuatwa tu.

Kwa swala lilivyo wahusika baadhi au wote ni kufukuzwa tu kwani wanahusika kwa asilimia mia kuhujumu misimamo ya chama chao. Huwezi kwenda kuapa bila kujua kama chama kimebadilisha msimamo. Wote wamehusika

Sasa hivi siasa za Tanzania zimeingiliwa na watu washamba kweli na wasio na aibu hata chembe. Uchaguzi wa serikali za mitaa haukufanyika, uchaguzi mkuu haukufanyika yote ni mambo ya kishamba shamba tu. Haya sasa dola nzima inafanya jinai ya kugushi na kuingilia utendaji wa kamati kuu ya chama cha chadema kufanya uteuzi wa wabunge viti maalumu aibu.

Dola hii ingekuwa imeundwa na watu kama waliopo nje ya dola(serikali) ingerazimishwa kuachia ngazi. Kwakuwa imeundwa na wachumia tumbo wasijari hadhi zao watapongezana
 
KUTOKA JIKONI: BAWACHA Kupinga Mfumo Dume CHADEMA

Zaidi ya Wanawake 100,000 wa BAWACHA wamejipanga kusaini fomu ya kuonesha mshikamano na wabunge 19 wa viti maalum (CHADEMA) walioapishwa jana.

Wanawake hao wamesema mfumo uliopo ndani ya chama hicho ni changamoto kubwa kwa maendeleo ya BAWACHA, hivyo ni lazima waupinge mfumo huo unaokandamiza haki zao.
 
Chama sio biashara binafsi. Huwezi kufukuza watu kwenye chama kwa kigezo cha hisia tu....
Walioapishwa waliteuliwa na Chama? Tumia akili ndogo kuelewa na kujibu hoja. Kama hakuna ulazima wa kuteuliwa na Chama basi hakuna sababu ya kutaja kwamba wanatoka chama fulani. Watekeleze wajibu wao kwa namna yao wanayojua lakini siyo hiyo ya sasa
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA anazungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mchakato wa wabunge wa Viti Maalum ambao wameapisha siku ya jana tarehe Novemba 24, 2020....
Hili Jambo kama lisingekuwa na baraka ya "System" wahusika woote wa uchafuzi huu wakiwemo wakuu wa gereza waliohsuika kumtoa huyo dada Nusrat usiku kabla ya hukumu wangekuwa mikononi mwa Takukuru mpaka hivi sasa. Ila hakuna watu maboya kama waandishi wa habari wa nchi hii.

Hivi kuna hata mmoja ameenda Tume ya uchaguzi kuhoji na kulitolea taarifa hili? Nimesoma magazeti ya leo yoote likiwemo Mwananchi (Gazeti liliokuwa limebaki peke yake lenye kuandika habari za kubalance) hamna kitu woote wamenadika habari za upande mmoja (Kutokana na maelekezo nadhani). Sijui kama ntanunua tena magazeti ya nchi hii tena hivi karibuni aisee niombeeni
 
"Katibu mkuu wa chama sio tu anatakiwa apeleke orodha bali anatakiwa apeleke fomu namba 8(d) kwa kila aliyekuwepo kwenye orodha ikiwa imesainiwa na katibu mkuu. Tume ya Taifa ya uchaguzi ilituletea fomu hizi hapa(Anazonyesha) ili tukishateua kama tungeteua, tupeleke orodha ya majina 113 kwa ujumla tukiwa tumejaza hizi fomu.

Mimi kama katibu mkuu, hakuna fomu yoyote ya mtu yoyote niliyowahi kuijaza popote kuthibitisha uteuzi wa yoyote"

Hapa sasa naanza kupumua, maana Halima Mdee ameniumiza sana moyo wangu.

Hao wengine siwatilii maanani kabisa, maana walitoka CCM na Lowassa, ila Halima kwa nini Kiongozi wangu?! 😭😭
 
Mnyika hajui kwamba Halima awezi kufanya mipango yoyote bila Mbowe na wengine kujua?
 
Hapo aibu kubwa ni kwa Halima Mdee, Very senior leader kushiriki ujinga huo kwa kweli si kwa leve yake inasikitisha sana...
Huwa nampuuza Kigogo kumbe anayoyaandika ndio ukweli wenyewe unatokeaga.

Alilisema hili mapema tu na kuanza malumbano na Bulaya.
 
Chadema hawatakaa wamsahau mh Halima Mdee aka Sauti ya Zege mwenyekiti wa Bawacha na mbunge wa viti maalumu mkoa wa Dar es salaam.

Sauti ya Zege jasiri muonesha njia.

Maendeleo hayana vyama!
 
Katibu mkuu wa chama sio tu anatakiwa apeleke orodha bali anatakiwa apeleke fomu namba 8(d) kwa kila aliyekuwepo kwenye orodha ikiwa imesainiwa na katibu mkuu. Tume ya Taifa ya uchaguzi ilituletea fomu hizi hapa(Anazonyesha) ili tukishateua kama tungeteua, tupeleke orodha ya majina 113 kwa ujumla tukiwa tumejaza hizi fomu...
Hebu tunaomba utupatie kifungu hicho cha sheria.
 
Tumia akili yako hata kidogo basi. Umeambiwa utaratibu wa chama haukufuatwa kama ndivyo uhalali huo unataka wapi? Hapa ni ile haki ya kusikilizwa ndio inayofuatwa tu...
Unauhakika na unachoandika?? Wewe unadhani mwanasheria kama Halima Mdee anaweza kuvunja taratibu kwa jinsi mnavyo bwabwaja.Subiri 27/11 ndiyo utashangaa kwamba jambo lina baraka zoooote za chama.
 
Chama sio biashara binafsi. Huwezi kufukuza watu kwenye chama kwa kigezo cha hisia tu.

CHADEMA haina hoja ya kupinga matokeo ya Uchaguzi na kuzuia Wabunge kufanya kazi yao....
Swala hapa kaka ni forgery na makosa mengine mengi ya nidhamu na liko wazi..walifukuzwa wa CUF tena kwa kosa dogo tu ijekuwa hawa wachumia tumbo...tunajua akili ndogo zenu MATAGA mmeshajipanga mahakani kwa ajili ya pingamizi kwa kutumia mahakimu wenu ila ilo haliondoi haki ya chama kutekeleza wajibu wake. Kufukuzwa kuko pale pale.
 
siamini kama Halima ni sehemu ya huu ubatili.

ahsante Katibu Mkuu.
 
KUTOKA JIKONI: BAWACHA Kupinga Mfumo Dume CHADEMA

Zaidi ya Wanawake 100,000 wa BAWACHA wamejipanga kusaini fomu ya kuonesha mshikamano na wabunge 19 wa viti maalum (CHADEMA) walioapishwa jana.

Wanawake hao wamesema mfumo uliopo ndani ya chama hicho ni changamoto kubwa kwa maendeleo ya BAWACHA, hivyo ni lazima waupinge mfumo huo unaokandamiza haki zao.
Hao BAWACHA walipewa fursa ya kugombea (Halima alikuwa Kawe), "hakuchaguliwa". Mfumo dume umetumika wapi, CHADEMA au Kawe? Wangeandama kwenda Kawe, kule Halima alikokosa kura. Hizi nafasi za viti maalum ni za uteuzi, na zote ni za wanawake. Hakuna mwanaume atakayepewa nafasi hiyo hata kama anafaa, lakini sharti utaratibu utumike kuwateua siyo suala la kusema tu mfumo unaokandamiza wanawake. Mbona hawalalamike walipowaacha wanawake wenzao ambao hawakugombea kwenye majimbo wachukue nafasi hiyo badala yake wao hao hao waliogombea kwenye majimbo sasa wapo tena viti maalum.
 
Back
Top Bottom