Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Leo Novemba 25, 2020 katibu mkuu wa CHADEMA amezungumza na vyombo vya habari makao makuu ya chama hicho eneo la Ufipa, Kinondoni mada kuu ikiwa uteuzi wa wabunge wa viti maalum ambapo uapisho wao ulifanyika jana bungeni jijini Dodoma jana.

Yafuatayo ni maelezo kwenye mkutano huo kuanzia mwanzo hadi mwisho pamoja na maswali kutoka kwa waandishi wa habari.

PIA, SOMA=> Hatimaye Wabunge wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

=> Ester Matiko: Kama chama kikiona kuna mwingine anafaa zaidi ya Ester Matiko, niko tayari

============​

JOHN MREMA: Mbele yetu katibu mkuu wa chama, John John Mnyika akiwa na mkurugenzi wa Itikadi, Uenezi na mahusiano ya mambo ya nje na msemaji mkuu kwa siku ya leo atakuwa katibu mkuu wa chama.

JOHN MNYIKA: Tarehe 28 Oktoba kulifanyika uchafuzi ulioitwa uchaguzi mkuu ambapo mtakumbuka kati ya mambo yaliyofanyika ni hujuma za wazi za mfumo wa kiserikali ukihusisha tume ya Taifa ya uchaguzi kupika matokeo ya uchaguzi.

Chama cha demokrasia na maendeleo hakijateua wabunge wa viti maalum au wagombe ubunge viti maalum wala hakijawasilisha orodha yoyote tume ya Taifa ya uchaguzi ya uteuzi wa wabunge wa viti maalum.

Kwa katiba ya CHADEMA, mamlaka ya uteuzi wa wabunge yapo kwa kamati kuu ya chama. Kamati kuu ya chama haijawahi kufanya kikao cha kuteua majina ya wabunge wa viti maalum wakati wowote.

Pili katibu mkuu wa chama ambae ndie mwenye mamlaka ya kimawasiliano ya kuwasiliana na tume ya Taifa ya uchaguzi, katibu mkuu wa chama sijawahi kuwasilisha orodha yoyote tume ya Taifa ya uchaguzi ya wanaoitwa waliopendekezwa wabunge wa viti maalum.

Katibu mkuu wa chama sio tu anatakiwa apeleke orodha bali anatakiwa apeleke fomu namba 8(d) kwa kila aliyekuwepo kwenye orodha ikiwa imesainiwa na katibu mkuu. Tume ya Taifa ya uchaguzi ilituletea fomu hizi hapa(Anazonyesha) ili tukishateua kama tungeteua, tupeleke orodha ya majina 113 kwa ujumla tukiwa tumejaza hizi fomu.

Mimi kama katibu mkuu, hakuna fomu yoyote ya mtu yoyote niliyowahi kuijaza popote kuthibitisha uteuzi wa yoyote.

Mchakato huo wote haukufatwa, kwa hiyo kwa tafsiri nyepesi, kilichofanyika ni biashara haramu ya kughushi ambayo imehusisha mfumo wa kiserikali, tume ya Taifa ya uchaguzi na kwakweli niseme vilevile imehusisha hao waliokwenda kuapa bila ridhaa ya chama na bila baraka za chama na bila kupishwa kwa mamlaka halali za chama.

Chama inabidi kichukue hatua, katiba yetu inasema hatua zozote zisichukuliwe bila ya wahusika kuitwa, kujieleza. Sasa kwa kuwa hili jambo ni la dharula, chama kitatumia utaratibu wa dharula katika kushughulika na jambo hili na tutaongozwa na kanuni za chama.

Kwa kuwa mamlaka ya jambo hili ni kamati kuu ya chama, naomba kuwatangazi kwamba tumeitisha kikao cha kamati kuu ya chama maalum, kitafanyika siku ya Ijumaa tarehe 27 hapa jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kuwa tutawaandikia wahusika, ili kusitokee kisingizio kwa yeyote kwamba hakuitwa, hakupata taarifa ya kuitwa naomba kutangaza 'Public notice' kupitia vyombo vya habari kwa wanachama wetu 19 walioshiriki kwenda kula kiapo jana tarehe 24 kufika makao makuu ya chama bila kukosa.

Kuna tukio la mwanachama wetu ambae ni kiongozi wa baraza la baraza la vijana la CHADEMA, Nusrat Hanje ambae amesota ndani kwa kesi ya kubambikiziwa kwa siku 133 akiwa mahabusu na leo tarehe 25 mahakama kuu ndio ilikuwa inakutana kutoa uamuzi juu ya rufaa ambayo amekata baada ya kusota ndani kwa muda mrefu.

Kituko kinachoashiria mfumo kuhusika katika huu mchezo, tarehe 23 usiku alikwenda kutolewa gerezani ili kesho yake apelekwe kuapa na alitolewa na mfumo bila hata kuzingatia masharti ya kisheria. Tunashkuru kwamba mwanachama wetu na kiongozi wetu ametoka baada ya kusota ndani kwa muda mrefu lakini mfumo ulimtoa ili kutekeleza malengo yao.

Sasa Ndugai amesema alipelekewa majina tarehe 20 Novemba na tume, Nusrat Hanje alietolewa gerezani tarehe 23 Novemba, uteuzi wa tume unasema umefanyika tarehe 20, fomu yake aliijaza lini, hakimu aliemuapisha alikuwa wapi kabla ya tarehe 20 tume ilipomteua mambo ambayo yanadhihirisha wazi kwamba hili jambo ni kazi ya mfumo.

Lengo la wazi la mfumo ni kutaka kufifisha ajenda ya kwamba Tanzania ilifanya uchaguzi haramu tarehe 28 Oktoba ulioitwa uchafuzi wakati umma ukishinikiza, jamii ya kimataifa ikishinikiza, bunge likionekana la chama kimoja ili kujaribu kulipa uhalali serikali ya illegitimate president Magufuli ikaamua kushiriki huu mchezo haramu wa kuhusisha tume, spika wa bunge na hatimaye tumefika hapa tulipofika.

Nitoe rai kwa watanzania, jambo hili lisitutoe watanzania kwenye mjadala mkubwa na muhimu zaidi kwamba tarehe 28 Oktoba kulifanyika uchafuzi na kwamba sisi tunataka uchaguzi ufanyika upya chini ya tume huru ya uchaguzi.

Sisi tunaotaka hilo tunatengenezewa mazingira ya mjadala kuhama, umma wa watanzania usikubali kuingizwa kwenye mtego wa dola wa kuhamisha mjadala na kufifisha hasira za wananchi.

Kauli iliyotolewa jana wakati wa kuapishwa iliyotaka kujenga ishara kama mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe alihalalisha hili linaloendelea, hii kauli sio ya kweli na mwenyekiti wa chama ndie atakaeongoza kikao cha kamati kuu ya chama kitakachofanyika tarehe 27.

2015 I told you! The effect of Willibrod Slaa Ambassador will be seen in the 2020 election.
Now here you are!
 
maswali mazito haya duuu! haswa kuachiwa na kuapishwa! huu mchongo mzima una baraka zote kutoka juu
Hiyo ni rushwa kabisa, kumfunga mdomo..Kwanini umnyime mtu haki yake kumshikilia muda wote huo bila kosa halafu in less than 48 hrs anaapishwa kuwa mbunge??? HII NI RUSHWA KABISA..
 
masikini mataga mmeacha vinywa wazi mlidhani chadema watakubali kuzama na wasailiti mwisho wasiku mmebaki na bosheni [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
Mkuu wewe ni kidagaa tu hapo chadema,

Hujui chochote kinachoendelea
 
NCCR-Mageuzi ilikuwa hivi hivi 1997.Ngoja akina Halima waje na vielelezo vya kiofisi halafu utashuhudia Mnyika atakavyopata kesi ya udhalilishaji wa wanawake ndani ya chama.Bawacha inakwenda kumshitaki Mnyika
 
Tumia akili yako hata kidogo basi. Umeambiwa utaratibu wa chama haukufuatwa kama ndivyo uhalali huo unataka wapi? Hapa ni ile haki ya kusikilizwa ndio inayofuatwa tu.

Kwa swala lilivyo wahusika baadhi au wote ni kufukuzwa tu kwani wanahusika kwa asilimia mia kuhujumu misimamo ya chama chao. Huwezi kwenda kuapa bila kujua kama chama kimebadilisha msimamo. Wote wamehusika

Sasa hivi siasa za Tanzania zimeingiliwa na watu washamba kweli na wasio na aibu hata chembe. Uchaguzi wa serikali za mitaa haukufanyika, uchaguzi mkuu haukufanyika yote ni mambo ya kishamba shamba tu. Haya sasa dola nzima inafanya jinai ya kugushi na kuingilia utendaji wa kamati kuu ya chama cha chadema kufanya uteuzi wa wabunge viti maalumu aibu.

Dola hii ingekuwa imeundwa na watu kama waliopo nje ya dola(serikali) ingerazimishwa kuachia ngazi. Kwakuwa imeundwa na wachumia tumbo wasijari hadhi zao watapongezana
Jazba hazitawasaidia...jiunge na washindi...unga mkono juhudi...maendeleo hayana vyama...Mdee na wenzake wameenda bungeni na watakula kuku...Kibaraka Lissu amekwenda ulaya...wapiga kelele mitandaoni wameachwa solemba...
 
Ubavu huo Mnyika hana maana na yeye ni mchumia tumbo tu, kama kweli anaweza angejihudhuru yeye maana amedharauliwa.
Kujiuzulu kwa sababu ya makosa ya wengine ni kukosa utambuzi,,, yeye asimamie mamlaka yake basi na kuhakikisha utaratibu na sheria vinafuatwa! Huko ndiko kuonesha ukomavu wa kiongozi
 
Maneno ni matatu tu ndugu mnyika usirembe FU...KU...ZA hao political prostitutes
Dah...wakupitisha hayo nani? Dijei? ...Mburaaa.... watu wanatafuta ELA wewe [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2960]
 
Naona kama kawaida malalamiko ni kwa mfumo.

1.Ina maana Halima Mdee ambaye pia ni mjumbe wa hiyo kamati kuu hajui utaratibu wa kuwapata hao wanawake?

Hajui Kamati kuu huketi? Haujui msimamo wa chama chao kuhusu hilo ilhali jana yake tu "Mbelgiji" katamka wazi?

2.Ina maana hata mawasiliano ndani ya CHADEMA hayapo? Watu wanapokea barua "iliyogushiwa" tu na kwenda Dodoma bila kushirikisha chama ilhali ni jambo linalokinzana na msimamo wa chama chao?

3.Huu utaratibu wa kuita watu wajieleze mbona kwa wengine huwa hautumiki ilhali kumbe upo kikatiba?

Kwa maelezo ya Mnyika, either kuna mgawanyiko kuhusu viti maalumu au wameamua tu kutuletea utetezi wa kitoto kuzugia.

BTW:Last time,Mbowe alikata baadhi ya majina yaliyopitishwa na kamati kuu akapachika vimada na wachaga wa DSM.

Ngoja tuone hii Movie itaishaje.
 
Kujiuzulu kwa sababu ya makosa ya wengine ni kukosa utambuzi,,, yeye asimamie mamlaka yake basi na kuhakikisha utaratibu na sheria vinafuatwa! Huko ndiko kuonesha ukomavu wa kiongozi
unawezaje kuwa kiongozi wa taasisi ya watu wasiofuatautaratibu na kujiamlia mambo watakavyo bila kukujulisha wala kukushirikisha huoni kama ni dharau kubwa hiyo? aeendelee tu kuchumia tumbo sio dhambi.
 
Mmepigwa za uso na Mnyika mnashangaa !! Kudadeki zenu !
Nyie ni wajinga kabisa. Na wajinga kama nyie ndio Mbowe anawafurahia kweli.

Subiri uone kama kina Mdee watafanywa lolote ndio utajua hujui.

Na kama unafikri kina Mdee wamekurupuka basi wewe ni mjinga kiwango cha lami
 
Maswali yafuatayo yanapaswa kujibiwa na Mbowe/Mnyika:

1. Nani amepeleka Orodha ya Majina ya Wabunge wa Viti Maalum NEC?
2. Orodha hiyo imepelekwa kwa njia gani?
3. Kama msimamo wa chama na wa Katibu Mkuu ni kuwa Orodha haikupelekwa, walioapishwa jana walipatikanaje?
4. Hatua gani zinachukuliwa na CHADEMA ikiwa usaliti umetokea?
5. Ilikuwaje Nusrat Hanje aachiwe tu kutoka mahabusu na asubuhi yake aapishwe kuwa Mbunge wa Viti Maalum?
6. Nani yuko nyuma ya suitafahamu hii nzima ndani ya CHADEMA na anashughulikiwaje?
Mkuu mengi ya maswali yako hapo juu hayapaswi kujibiwa na Mbowe au Mnyika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni bora asingefanya hiyo Press maana imeonyesha jinsi gani CHADEMA ilivyo na mfumo mbovu wa uendeshaji na mawasiliano (kinaendeshwa kama kibanda cha Tigopesa)
Maswali muhimu
1. Ni kweli CHADEMA haikujua kuwa wanachama wake zaidi ya 10 wangeapishwa?
2. Nini msimamo wa CHADEMA kuhusiana na wanachama hao?
3. Kutotambua matokeo ya Uchaguzi mkuu wa October ni maneno ya viongozi au msimamo wa Chama?
4. Je mwenyekiti hajui chochote kuhusiana na swala hili?
 
Ndo maana katibu mwenezi anakiita chama cha mtu kile.

Wao hawajapata ubunge hvyo hawataki na wenzao waulate. Je wanavyodai uchaguzi wa mwaka huu ulivyofanyika Je ni tofauti na zile zingine ambazo walikataa kuutambua wakati wamepata ubunge na kuendelea kuapishwa. Hii yote sababu ya maslahi yao ya hela...
 
Chama ni mali ya umma hamuwezi kikundi fulani kujiamria tuu.

Hawa wamama ni wa kuwapongeza sana, niwapenda amani na MAENDELEO ya nchi hii na wazalendo wa kweli.
 
Wakuu sina mengi ya kusema maana roho yangu i dhaifu kiasi cha kufa.

Jana tulishuhudia uapishwaji wa wabunge viti maalumu was CHADEMA pale Dodoma, moja ya suala la kushitua ni kiongozi wa Wanawake hao kulitangazia bunge na Taifa kwa ujumla kuwa anamshukuru Mwenyekiti Fremon Mbowe kwa kufanikisha jambo hilo.

Hapa ndipo ulipo uasi wa Mbowe.

1. Amemwachia Katibu Mkuu kuzungumzia swala nyeti la uvunjifu wa katiba huku yeye kama kiongozi mkuu wa chama akiwa amejitenga.

2. Ametanjwa na Halima Mdee kama mtoa baraka.

3. Amekuwa kimya tangu suala hili liwe wazi.

Don't trust anybody. Nchi imejaa mamluki kila sehemu.
 
Back
Top Bottom