Katibu Mkuu wa CHADEMA anazungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mchakato wa wabunge wa Viti Maalum ambao wameapisha siku ya jana tarehe Novemba 24, 2020.
Tumewaita kuwaeleza kwamba CHADEMA hakijateua wabunge wa viti maalum wala hakijawasilisha orodha yoyote Tume ya Uchaguzi ya uteuzi wa wabunge wa viti maalum
Mimi kama Katibu Mkuu wa Chama sikuwahi kujaza fomu yoyote, kumthibitisha mtu yeyote mahali popote, kilichofanyika ni biashara haramu ya kugushi iliyohusisha mfumo wa kiserikali.
Mawasiliano yangu ya mwisho na Tume ya Uchaguzi zilikuwa ni barua 2, Nov 9 , niliiandika baada ya Mkurugenzi wa NEC kunukuliwa na vyombo vya habari kwamba
CHADEMA imewasilisha orodha ya wabunge wa viti maalum na yeye amekwishaipeleka bungen
Kwa katiba ya
CHADEMA mamlaka ya uteuzi wa wabunge yako kwa kamati kuu ya chama, na kamati kuu ya chama haijawahi kufanya kikao cha uteuzi wa majina ya wabunge wa viti maalum na mimi Katibu Mkuu sijawahi kuwasilisha orodha yoyote
Katibu Mkuu, John Mnyika amewataka wabunge wote walioapishwa kuwa wabunge wa Viti Maalum kufika kwenye ofisi za Makao Makuu ya Chama siku ya Novemba 27, saa mbili asubuhi bila kukosa kwa ajili ya utaratibu mwingine.
Mwanachama wetu aliyekuwa na kesi ya jinai ya kubambikiwa kwa muda mrefu Nusrat Hanje alitolewa gerezani tarehe 23 Novemba na mfumo ili watimize adhma yao.
Katibu Mkuu amesema kwamba wabunge wote walioapishwa Novemba 24 wamewekwa na mfumo na hawana baraka za chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Kauli iliyotolewa jana na kumhusisha Mwenyekiti, Freeman Mbowe haina ukweli. Mbowe ataongoza kamati kuu na itawasikiliza wahusika. Kati ya walioapishwa kuna wajumbe wa kamati kuu wanafahamu uteuzi haukufanyika na wanajua wameshiriki biashara haramu
==========
JOHN MREMA: Mbele yetu katibu mkuu wa chama, John John Mnyika akiwa na mkurugenzi wa Itikadi, Uenezi na mahusiano ya mambo ya nje na msemaji mkuu kwa siku ya leo atakuwa katibu mkuu wa chama.
JOHN MNYIKA: Tarehe 28 Oktoba kulifanyika uchafuzi ulioitwa uchaguzi mkuu ambapo mtakumbuka kati ya mambo yaliyofanyika ni hujuma za wazi za mfumo wa kiserikali ukihusisha tume ya Taifa ya uchaguzi kupika matokeo ya uchaguzi.
Chama cha demokrasia na maendeleo hakijateua wabunge wa viti maalum au wagombe ubunge viti maalum wala hakijawasilisha orodha yoyote tume ya Taifa ya uchaguzi ya uteuzi wa wabunge wa viti maalum.
Kwa katiba ya CHADEMA, mamlaka ya uteuzi wa wabunge yapo kwa kamati kuu ya chama. Kamati kuu ya chama haijawahi kufanya kikao cha kuteua majina ya wabunge wa viti maalum wakati wowote.
Pili katibu mkuu wa chama ambae ndie mwenye mamlaka ya kimawasiliano ya kuwasiliana na tume ya Taifa ya uchaguzi, katibu mkuu wa chama sijawahi kuwasilisha orodha yoyote tume ya Taifa ya uchaguzi ya wanaoitwa waliopendekezwa wabunge wa viti maalum.
Katibu mkuu wa chama sio tu anatakiwa apeleke orodha bali anatakiwa apeleke fomu namba 8(d) kwa kila aliyekuwepo kwenye orodha ikiwa imesainiwa na katibu mkuu. Tume ya Taifa ya uchaguzi ilituletea fomu hizi hapa(Anazonyesha) ili tukishateua kama tungeteua, tupeleke orodha ya majina 113 kwa ujumla tukiwa tumejaza hizi fomu.
Mimi kama katibu mkuu, hakuna fomu yoyote ya mtu yoyote niliyowahi kuijaza popote kuthibitisha uteuzi wa yoyote.
Mchakato huo wote haukufatwa, kwa hiyo kwa tafsiri nyepesi, kilichofanyika ni biashara haramu ya kughushi ambayo imehusisha mfumo wa kiserikali, tume ya Taifa ya uchaguzi na kwakweli niseme vilevile imehusisha hao waliokwenda kuapa bila ridhaa ya chama na bila baraka za chama na bila kupishwa kwa mamlaka halali za chama.