Wakuu Salam,
Naomba nitangaze maslah, mimi ni mfanyabiashara, nipo Kariakoo, nje ya kariakoo na mkoa wa Pwani.
Malalamiko yetu wafanyabiashara mengi ni justifiable.. lakini hili la kumlaumu Mwigulu Nchemba bila supporting evidence is ungrounded.
Kuna watu wanatumia udhaifu wa migogoro ya sheria zilizopo kumgandamiza bila sababu.
Mfano.
1. Hoja ya fine ya kutokutoa EFD recept sio ya leo, na hii ilipingwa sana na aliekuwa mbunge wa Muleba Anna Tibaijuka, nilishangaa saana yale mapendekezo, kama kawaida ya bunge letu.. papatu papatu hoja ikapita ikawa sheria, Kipindi hicho Mwigulu ni Wazir wa mambo ya ndani.
2. Hoja ya ushuru wa malori, Ndugu Chuki anaweza kuwa ana issues personal na Mwigulu na siwez kuwaingilia , ila kodi ya 2.7M sio kubwa kama anavyodai, kumbuka kubeba tonneau 10 had mwanza ni zaid ya 1.5M na hiyo ni non negotiable.... kutaka hiyo gharama iingizwe kwenye diesel ni ku shift tax burden to non beneficiaries, ambayo ni unfair taxing.
3. Hoja za registration of warehouse sio kitu kipya na wengi tumesajili nikiwemo, hoja za umiliki ni jambo jingine, labda tuseme issue ya With holding Tax ndio haijakaa Sawa, lakini kulalamika kwamba tusisajili sio Sawa kabisa.
Kwenye ethical business ni lazima usajili store na ulipie usimamiz wake, ikiwa na vigezo vyote.... hii ni excuse ambayo kumlaumu nayo Mwigulu ni ku choose easy victim.
4. Hoja za task force zilikuwepo toka kipind cha mwendazake... kwamba tunasumbuliwa hili ni kweli na ni sualq la kuweka utaratibu tu wa namna ya ku control, ambayo sikuona sabab ya kumzodoa mwamba vile.
5.Utitiri wa kodi kwenye biashara na mamlaka nyingi zinazosimamia jambo moja ni suala la kurith na Mwigulu sidhan kama ni wa kulaumiwa 100% , issue hapo ni CCM kuweka na kuunda hizi taasisi kutafutia washkaj wao ulaji.
Kuna kila sabab ya kuunganisha taasisi nyingi sana ili kuondoa usumbufu.
Ni hayo tu... tumuhukumu Mwigulu kwa mengine lakini sio moja kwa moja kwa baadhi ya sheria ambazo amezikuta.