Mo afafanua ununuzi wake kwa Simba

Mo afafanua ununuzi wake kwa Simba

Majibu

1. Simba ya wanachama wa Simba. Hii club inamilikiwa katika zama za Mwl wetu JK Nyerere japo tupo kwenye digial world. Anayeuza ni wanachama wa Simba ambao wao ndio wamiliki. Faida atakayopa itaonekana baada ya mahesabu ya mwaka kufanyika

2. Hio 20bln ni kununua maamuzi yaani kumiliki Simba kwa 51%. Kwa maneo mengine kuiendesha na kuisimamia Simba iwe kwa kutumia hizo 20bln pamoja na hela zingine na Assets zingine Simba walizonazo

3 & 4. 49% wanaendelea kumiliki wanachama wa Simba. Hizo hisa so far bado wanamiliki wanachama, lkn baadaye wakiamua kuuza watajua wenyewe huko. Ila kitakachobadilika kikubwa sana ni kuwa Mo ndio mwenye last say kama Ibra alivyo Chelsea. Akiamua kula sahani moja na Kocha anakula, na wanachama hawatakiwi kufungua mdomo.

Akiamua mchezaji fulani asisajiliwe ndo inakuwa hivyo na wanachama wanatakiwa ku shut up!

Asante mkuu, ninadhani nakuelewa kwa mbali kidogo.

Lakini wewe unaona ni sahihi Mo kuinunua Simba kwa 20bln halafu aje aindeshe kwa kutumia hela hizo hizo?

Yaani awe na control juu ya matumizi ya hiyo hela?
 
Na MO akishachukua 51% yeye ndo mwenye maamuzi ya vikao.
49% haiwezi kuilazimisha jambo 51%.
Kwa hiyo swala la hata nani atapata share ya hizo 49% ataamua MO isipokuwa pale tu maamuzi yatafanyika kabla ya kumkabidhi MO na iwe sehemu ya mkataba wa makabidhiano
Anachokita mo ni money secure sio kununua timu mana kununua ni 100% ya hisa na kwa mana leo simba ikisema ifanye valuation ya mali na kuweka kwa dhamani ya hisa 100% sokoni uwenda simba isifikie bil 20 ndo mana matumizi ya pesa anayotaka yeye yawe sahihi kwa timu na sio kwa viongozi akatoa mfano akitaka matumizi yawe kwa kids funds na usajili na wengine au uongozi ukisema apana hela inaenda kwenye ndege ya club badae hela ile bil 20 ikikata nani mwenye kuumia kwasasa simba na dhamani yake aiwezi kutengeneza hela coz aijawekeza pakubwa inapata hasara na ye anataka money security si kingine kwan iyo pesa simba wakipewa watafanyia nn wakati wana asilimia 49 je na ye atoe hela yake mfukoni kwa kufanya malekebisho wakati nyie mnakula hela nje ya iyo pesa kama kuna faida mtagawana na hasara pia kwa asimilia na kama kuna mahitaji ki club nae atatoa kwa 51% na simba 49% sasa simba kama atatumia iyo bil 20 sawa au jingine
 
Inaonekana huelewi hata unachokisema

Simba wameshaona hayo matatizo ya Muundo na Mfumo ndio maana wameamua kuubadilisha

Na mfumo waliochagua Simba ni sahihi sana kwenda kwa kipindi hiki na ni mfuo unatumika na klabu zote zilizofanikiwa duniani na Africa

Tunachosema sisi....Ni Transformation hii ifanyike ki utaalamu sana ....Na kwa umakini mkubwa

Ila ishu kama tubadili mfumo au la...simba tumeshaaamua kuubadili huo mfumo

Naona wewe ndie huelewi.

Unabadilisha mfumo halafu ndio unakaribisha watu wa kununua hisa au timu kamili.

Wenye pesa wananunua mfumo au "business model" na si timu pekee- mfumo ni pamoja na mapato ya uwanjani yaani viingilio, mauzo ya jezi na vifaa au "merchandise", mauzo na manunuzi ya wachezaji na mapato yanayotokana na majengo au jengo.

Kwa kuwa yupo mtaalam bwana Hans Pope lakini bado naona timu haina mfumo wake wa biashara.

Wapenzi wa simba mpaka sasa hakuna wenye sauti na mfumo uliopo na si hao tu hata kule Yanga, na hii ndio chanzo cha migogoro ya kila wakati.

Labda nikuulize suali, mfumo wa uendeshaji wa klabu ya Simba unaufahamu?

Tunajadiliana na mimi ni mpenzi na nna kashea kangu timu ya Arsenal na huwa nakaa kuwasikiliza Arsene Wenger na Iva Gazidis kwenye mkutano wa kila mwaka wa shareholders, hivyo nazungumza kutokana na uzoefu.
 
Raimundo ameuliza swali zuri hapa

Na katika swali hili la mkuu...naomba kukuza mjadala kama hivi....MO akipewa 51% anakuwa na Control ya Kampuni ya Simba.Investment kwenye TBond itafanywa na kampuni ya Simba. Return from Investment ya Bond itaingia kwenye kampuni ya simba ambayo MO ndiye mmiliki....Hauoni hapo kuwa hakuna SALE transaction? Kwa sababu mwenye kampuni MO atakuwa tu anatumia hela yake aliyoiweka kule BOT/Hazina kwenye TBond.

Ndio maana mi naona kuna umuhimu wa kuajiri Proffesional law firm ili kushauri muundo sahihi

Mkuu una akili mno.

Jamaa hela kaizungusha inarudi mfukoni mwake kama 51%.

Kununua ni kama kawalipa waliokua wameshika hiyo 51% earlier akafanya buyout,hao watu wakashika mshiko wao 20Bil wakasepa,then akaanza kuwekeza kwenye timu afresh.

Jamaa hajanunua kitu,kapewa timu bure 51%,halafu hiyo 20B ni ya kuendeshea timu.

Infact naweza hisi Simba haikua na mmiliki,ilikua kama NGO/Association tu,nadhani Trustees walikua wanashika madaraka kwa niaba ya washika kadi.

Aisee jamaaa ana-close business of the century,kapewa timu bureeee!
 
Plan kubwa sana,Jamaa ni STRAIGHT VISIONARY..
Klabu kubwa mbele ziko ktk mfumo km Huu,na zimefanya vitu vikubwa..
I hope wanaopinga mabadiliko haya,wana Interests zao binafsi si interests za kuisogeza klabu mbele,all z best Mo
 
However,...hata kama akitumia hiyo advantage...its not a problem so far

Timu ibadilishe mfumo iwe kampuni.......

Katika hiyo miaka yote 80 Timu ilikuwa na hela? na ilifanya nini? Mpira wa sasa sio wa ujanja ujanja kama simba na yanga za miaka 80 iliyopita
Kweli mkuu nakubaliana na mabadiliko kwa timu ya simba lakini kwa njia anazozitumia mo kutaka kujimilikisha simba sio nzuri na sikubaliani nazo kwasababu anaforce mambo yaende fasta wakati wapenzi na wanachama wa simba awajapata elimu ya kutosha kuhusiana uwekezaji mkuu
 
Mwandishi kasahau swali moja la msingi. Nalo lingeulizwa hiviii.

" Mo unaonaje kama mwana simba na unaeipenda simba ungepeleka ombi kwa uongozi watathmini thamani ya klabu kisha waje na jibu klabu ina thamani gani na baadaye watangaze kuuza hisa katika soko huria ili wenye uwezo muingie kwenye mchakato wa kumpata mshindi ambaye ndo atakuwa mmiliki wa timu. Badala yake unataka wewe upewe direct timu pasipo kushindanishwa na wengine.?"
 
Mkuu hili kuyumba kwa uchumi wa vilabu ni wimbi la dunia nzima si Simba tu.

Yanga wanasahau mapema hata Manji alishawahi kudokeza hili la Yanga Kampuni na Katiba yao ilipitishwa kwa nusu saa tu pale Polisi Mes ambapo Maniji alitaka 75% na 25% awanunulie Yanga hizo hisa

Kama tunafuatilia kwa makini, hamasa ya soka imeshuka duniani kote kutokana na mdororo wa kiuchumi na pengine njia mbadala kwa vilabu vingi kwa sasa ni kutegemea zaidi wazalishaji wa bidhaa za ndani kuwadhamini.

Roy Miller kutoka kitengo cha biashara ya michezo katika chuo kikuu cha Liverpool anasema kuwa hali kama hiyo haijawahi kuonekana kwa muda mrefu na ni ishara ya kwamba uchumi uko katika hali mbaya.

Wachambuzi wanaamini hata hivyo kuwa vilabu vikubwa kama vile mabingwa wa Uingereza Manchester United, Real Madrid na kadhalika siku zote zitaendelea kuwavutia wafadhili na washabiki wengi, lakini kwa vilabu vidogo hali ni tofauti.

Ligi kuu ya Uingereza ndiyo ligi yenye kuingiza fedha nyingi kabisa ambapo mwaka jana mapato yake yalifikia kiasi cha paundi billioni 1.5.Lakini ni vilabu vinane tu kati ya 20 vya ligi hiyo vinavyojiendesha kwa faida.

Maswali yameibuka juu ya majaaliwa ya udhamini wa kampuni ya kimarekani ya AIG kwa timu ya Manchester United wa dhamani ya paundi millioni 56.5 ambayo ni rekodi nchini Uingereza.Kampuni hiyo ya kimarekani imelazimika kuokolewa na serikali iliyonunua hisa kubwa za asilimia 80 baada ya kuwa katika hali mbaya ya kuelekea kuwa mufilisi.

Timu nyingine ya ligi kuu ya Uingereza ya West Ham Unitd hivi sasa haina udhamini katika jezi zao baada ya kampuni iliyokuwa ikiidhamini ya XL Leasure Group kufilisika.Nayo West Bromwich Albion iliyopanda daraja imeshindwa kupata ufadhili kufuatia kujiondoa kwa aliyokuwa mfadhili wake kampuni ya simu ya Ujerumani ya T-Mobile.

Newcastle United nayo ilikaribia kuwa katika hali hiyo baada ya mfadhili wake benki ya Northen Rock kuokolewa na serikali ya Uingereza kufilisika ambapo huko Italia timu ya Lazio kwa sasa inacheza bila ya kuwa mfadhili .

Hata hivyo kwa mujibu wa wachambuzi na watalaam wa masuala ya ufadhili katika michezo, timu kama Manchester Uinted haitopata shida kupata ufadhili mwengine iwapo serikali ya Marekani itaamua kuondoa ufadhili wake baada ya kuwa imechukua hisa kubwa katika kampuni ya AIG. Pippa Collet ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni inayohusika na ufadhili kwenye sekta ya michezo anasema kuwa udhamini katika kandanda kwa muda mrefu umekuwa ukipewa thamani kubwa kuliko inavyostahili, na kwamba hivi sasa kunafanyika marekebisho katika soko la udhamini.

Tanzania haipo kwenye kisiwa, unaona hata mfadhili wa hivi karibuni wa simba kwa kiasi kikubwa HZP amenza kuchoka kutumia fedha zake kusajili, ilihali hata idadi ya watazamaji imepungua sana, na mzalishanji wa bidhaa anayejitutumua kwa sasa ni Azam pekee kupitia udhamini wa TV yake

hakuna namna

nitaurid nikupe udadavuzi wa HISA ZA MO

Hii article yako ni ya zamani sio relevant kwa sasa (AIG sio wadhamini tena wa MUFC wadhamini ni Chevrolet ) .Ligi ya England hakuna hilo tatizo,liko sana Italy ndio maana wamiliki wengi wa timu wameanza kuziuza (AC Milan,Inter etc)

Hakuna uhusiano wa kuongezeka gharama za uendeshaji soka la ulaya na huku kwetu kwani model za uendeshaji wa ulaya na kwetu ni tofauti kabisa.
 
MO ametumia chance kwakuwa wanachama wako desperate kutokana na matokeo mabovu miaka ya karibuni,Nafikiri MO alipaswa kusisitiza kubadili mfumo wa uendeshaji ambao ungempa kila mwanachama nafasi lakini kitendo cha yeye ku-propose apewe 51% ndio kinatia shaka na kitendo cha kuwatia pressure viongozi kuwa mchakato ufanyike ndani ya miezi 3
 
Mkuu Belo, unaonaje Mo anafaa kuinunua Simba moja kwa moja kwa hizo hisa 51%

Watu wanapenda kuiga sana mambo, miezi mitatu ni michache mno.

Simba ibadilishe mfumo wake wa uendeshaji wa klabu (sio timu) halafu wanachama wote wawe na uanachama na walipe ada ya uanachama.

Pia Simba iwe na uwanja wake wenyewe wa kuwaingizia kipato na vyanzo vingine vya mapato na sio kula na TFF na pesa yote kupotea bila daftari.

Wanachama wanaohudhuria mikutano kama wa kule Oysterbay ambao ni 700 si wanachama wote wa Simba Sports Club.

Wanachama wote wa klabu ya Simba wasajiliwe upya na waingizwe kwenye mfumo wa klabu yaani majina yao na taarifa zao viwe kwenye computer.

Wanachama wote wakisajiliwa nchi nzima utapata watu Zaidi ya watu 500,000 au Zaidi (hiyo ni estimate tu).

Hii ni kwa timu zote hata Yanga pia na ukiishafanya hivyo, klabu inatafuta watu wenye sifa ya kuendesha klabu ya mpira kuanzia CEO hadi meneja wa timu.

Kule juu kunakuwa na bodi yenye , mwenyekiti, wamiliki wa klabu (wale wenye hisa kubwa) na wadhamini.

Hili suala ni gumu sana lakini kama mmiliki wa TP Mazembe ameweza basi Mohamed Dewji nae ataweza, ila Simba ibadili mfumo wa uendeshaji wake halafu Mo ndio aingie.
 
Mimi binafsi sio muumini wa timu kumilikiwa na watu wachache football ni mchezo wa wanachama/wapenzi na mashabiki so ni lazima wawe sehemu ya timu .Watanzania tunapenda sana soka lakini hatujapata viongozi ambao wana nia ya kusaidia soka letu wengi wao wanaingia kwenye soka ili biashara zao ziende vizuri wengine wanatengeneza umaarufu ili waingie kwenye siasa/biashara . Population yetu inakaribia 50 milioni lakini ajabu wanachama wa kubwa ( Simba +Yanga) hawafiki 20,000,timu zinaendeshwa na kundi la viongozi hata 20 hawafiki hao ndio wana maamuzi ya timu nzima Yanga/Simba.Naamini kama viongozi wangewashirikisha wapenzi na mashabiki hizi timu zingeweza kuwa hata na wanachama 2 million sidhani kama haya matatizo ya klabu kutokuwa na fedha yangekuwepo.

MO anataka kuimiliki Simba na na sio kubadilisha mfumo,Idea aliyoileta mwanzo ilikuwa nzuri tatizo viongozi walidharau na hii miaka wanavyofanya vibaya jamaa ametumia hiyo advantage kuwashawishi wanachama bila kuwashirikisha na kuwapa elimu ya kutosha kuhusu huo mfumo mpya
 
Mo anaforce haraka haraka na kama huu mchakato ukienda taratibu taratibu ili kuwapa muda na elimu kwa wapenzi na wanachama wa simba sport ili waelewe huu mfumo mpya utakuja kusikia mo kajitoa
 
So, hiyo hela ikitolewa watapata chochote?

Maana wao watakuwa ndo wameuza timu siyo?
Hebu tuwekane sawa tofauti ya kuuza na Ku share holding !! maana tusije kutoka mishipa ya shingo ilihali hatujui tofauti ya maneno haya mawili au msambamba wake
 
Hebu tuwekane sawa tofauti ya kuuza na Ku share holding !! maana tusije kutoka mishipa ya shingo ilihali hatujui tofauti ya maneno haya mawili au msambamba wake
Anza wewe kujibu Mo amesemaje .... Auziwe timu
 
Maswali mazuri sana........Nilichojifunza kwenye mchakato huu Mo anataka kukimbiza mambo kwa spidi ili kuwaingiza kingi simba

Hili zoezi inatakiwa samba ndio wawe on top of the game na sio MO........

Maswali yako ni ya Msingi sana...Na ndio maana katika transaction hii kuna umuhimu wa Simba kwenda taratibu sana

Kwa msingi wa kuhakikisha hii long living brand inabaki na thamani yake.....MO ni business man...anavutia upande wake wa faida za kipindi kijacho...sio miaka mitano ijayo...miaka mingi

Hivyo basi nikiwa naunga mkono transformation hii lakini please smart people wawe makini Simba I control hii process na sio MO

CC sembo grafani11 mkolaj Amavubi

.....wewe ndugu ndio ninakuelewa sasa!, kumbe wewe ni miongoni mwa kina Aveva mnaotaka simba iendelee kubaki hapa ilipo!, sijui mnafaidika na nini?!

Yaani yote "MO" aliyozungumza mnaona hana anachofanya!, hii ndio roho typical ya mswahili!, mfukoni masikini hana kitu, lakini full mdomo, maneno mengiiii, mipango mingiii...!!!

Hili zoezi Simba wanatakiwa wawe on top of the game for what?!, hawana pesa za usajili, mishahara ya wachezaji shida (mnaila na njaa zenu!), uwanja wa mazoezi, everything ni shida!, halafu eti mtu anapayuka tu, hili zoezi linatakiwa liende taratibu!

Hiyo brand ya Simba imekuwepo miaka na miaka hapo, mmeifanyia nini zaidi ya kujinufaisha binafsi?!, hivi nikiwauliza maendeleo ya uwanja wa Bunju unaweza kunijibu!, siku zote biashara ni faida, hakuna asiejua. Bora uwe na mfanyabiashara anaejulikana wazi, kuliko kuwa na nyie "wafanyabiashara uchwara" mnaoitegemea klabu kujinufaisha!

Hata km hilo zoezi likienda kwa mwendo wa konokono unaoutaka ndio itakuwaje?, kwamba ipo siku mtapata pesa za usajili?, au mnataka kutuchelewesha tu muendelee kupiga dili!, huku timu ikiendelea kufanya vibaya km kawaida?!

Lazima mbadilike kulingana na wakati, msilazimishe mambo yabaki km yalivyo siku zote wakati maendeleo ya klabu ni mabovu, nahisi KUNA KITU UTAKUWA ULIKUWA UNAKITAFUTA SIMBA, HUU UJIO WA MO UMEKUHARIBIA DILI, katege sehemu nyingine!
 
Mkuu hili kuyumba kwa uchumi wa vilabu ni wimbi la dunia nzima si Simba tu.

Yanga wanasahau mapema hata Manji alishawahi kudokeza hili la Yanga Kampuni na Katiba yao ilipitishwa kwa nusu saa tu pale Polisi Mes ambapo Maniji alitaka 75% na 25% awanunulie Yanga hizo hisa

Kama tunafuatilia kwa makini, hamasa ya soka imeshuka duniani kote kutokana na mdororo wa kiuchumi na pengine njia mbadala kwa vilabu vingi kwa sasa ni kutegemea zaidi wazalishaji wa bidhaa za ndani kuwadhamini.

Roy Miller kutoka kitengo cha biashara ya michezo katika chuo kikuu cha Liverpool anasema kuwa hali kama hiyo haijawahi kuonekana kwa muda mrefu na ni ishara ya kwamba uchumi uko katika hali mbaya.

Wachambuzi wanaamini hata hivyo kuwa vilabu vikubwa kama vile mabingwa wa Uingereza Manchester United, Real Madrid na kadhalika siku zote zitaendelea kuwavutia wafadhili na washabiki wengi, lakini kwa vilabu vidogo hali ni tofauti.

Ligi kuu ya Uingereza ndiyo ligi yenye kuingiza fedha nyingi kabisa ambapo mwaka jana mapato yake yalifikia kiasi cha paundi billioni 1.5.Lakini ni vilabu vinane tu kati ya 20 vya ligi hiyo vinavyojiendesha kwa faida.

Maswali yameibuka juu ya majaaliwa ya udhamini wa kampuni ya kimarekani ya AIG kwa timu ya Manchester United wa dhamani ya paundi millioni 56.5 ambayo ni rekodi nchini Uingereza.Kampuni hiyo ya kimarekani imelazimika kuokolewa na serikali iliyonunua hisa kubwa za asilimia 80 baada ya kuwa katika hali mbaya ya kuelekea kuwa mufilisi.

Timu nyingine ya ligi kuu ya Uingereza ya West Ham Unitd hivi sasa haina udhamini katika jezi zao baada ya kampuni iliyokuwa ikiidhamini ya XL Leasure Group kufilisika.Nayo West Bromwich Albion iliyopanda daraja imeshindwa kupata ufadhili kufuatia kujiondoa kwa aliyokuwa mfadhili wake kampuni ya simu ya Ujerumani ya T-Mobile.

Newcastle United nayo ilikaribia kuwa katika hali hiyo baada ya mfadhili wake benki ya Northen Rock kuokolewa na serikali ya Uingereza kufilisika ambapo huko Italia timu ya Lazio kwa sasa inacheza bila ya kuwa mfadhili .

Hata hivyo kwa mujibu wa wachambuzi na watalaam wa masuala ya ufadhili katika michezo, timu kama Manchester Uinted haitopata shida kupata ufadhili mwengine iwapo serikali ya Marekani itaamua kuondoa ufadhili wake baada ya kuwa imechukua hisa kubwa katika kampuni ya AIG. Pippa Collet ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni inayohusika na ufadhili kwenye sekta ya michezo anasema kuwa udhamini katika kandanda kwa muda mrefu umekuwa ukipewa thamani kubwa kuliko inavyostahili, na kwamba hivi sasa kunafanyika marekebisho katika soko la udhamini.

Tanzania haipo kwenye kisiwa, unaona hata mfadhili wa hivi karibuni wa simba kwa kiasi kikubwa HZP amenza kuchoka kutumia fedha zake kusajili, ilihali hata idadi ya watazamaji imepungua sana, na mzalishanji wa bidhaa anayejitutumua kwa sasa ni Azam pekee kupitia udhamini wa TV yake

hakuna namna

nitaurid nikupe udadavuzi wa HISA ZA MO

....wewe nimekuelewa!, watu wanapiga kelele sana MO mwizi sijui nini!, anakwambia Simba ina thamani kubwa, kisa ina mashabiki milioni whatever...., hivi mmeshawahi kuwa-organise hao mashabiki mkapata idadi yao ya kweli?, mna uhakika gani hao mashabiki km kweli kwa wingi wao watakuwa na nia ya kujitolea kuichangia klabu?, na uongozi utakuwa thabiti kulinda kile wanachama wanachochangia?, sio watakuwa wapiga dili km hawa waliopo?, halafu tena, mnataka muda gani kuyakamilisha yote hayo?, huku timu inaendelea kufanya vibaya tu...mnasema iko siku, iko siku....!!

Muhimu hapa iwepo kampuni ya sheria, itakayowaelekeza Simba nini cha kufanya, eventhough i still doubt, hizo hisa za MO lazima zitakuwa nyingi tu, sababu ndie katoa pesa, na kiuhalisia, huwezi toa pesa yako popote pale, halafu usiwe na last say!, NEVER, hili tukubali!.
 
Precisely....kimsingi hiyo ndiyo position yangu...na hapo ndipo umakini wa wanasimba unatakiwa kuwepo

Hii timu ina historia yake ...kumpa tu mtu mmoja hivi bila utaratibu makini ni hatari

Hii kazi ingefanywa na professional firm ya sharia katika kushauri structure nzuri

....hapa sawa, kazi ifanywe na proffessional law firm!, good!, but thn again for how long?!, nina uhakika, kwa huu uongozi uliopo, mkiwapa tu nafasi ya kuruhusu kuleta neno "mchakato unaendelea", ndio imetoka mazima, hawa wapiga dili watakomaa na mchakato unaendelea mpk mwisho wa dunia!

Hii iwe ni long term strategy, but what's the short term kuitoa Simba hapa ilipo?!, ndio sababu nina support ujio wa huyu jamaa!, badala ya kuendelea kusajili "rejects" kuanzia makocha mpk wachezaji kwa ukosefu wa fedha,bora sasa tusogee hatua moja mbele!
 
Plan kubwa sana,Jamaa ni STRAIGHT VISIONARY..
Klabu kubwa mbele ziko ktk mfumo km Huu,na zimefanya vitu vikubwa..
I hope wanaopinga mabadiliko haya,wana Interests zao binafsi si interests za kuisogeza klabu mbele,all z best Mo
Kwel kabisa mkuu watakua wananufaika na mfumo uliopo, kwa maana kwamba watakua wanapiga hela, haiwezekani litimu linaboronga kila siku migogoro, hela halina, halafu anakuja mwekezaji tena sio mwekezaji tu bali nae ni mpenz na mwanachama wa simba, kwa mapenz alonayo na maumivu anayopata kutokana na timu kuboronga anataka kuisaidia isiboronge af watu wenye interest zao binafs wanampinga, sisi mashabiki tunakuunga mkono Mo, half ao wanaopinga mchukue mmoja muulize kipind iki ambacho klabu haina hela we umetoa shilingi ngap kuisaidia katka usajili na vingine? Mo katoa 100mil
 
Back
Top Bottom