Belo
JF-Expert Member
- Jun 11, 2007
- 12,897
- 10,213
Mkuu...sasa kila mkutano ili uweze kuendelea si unahitaji Quorum kutimia....Na kadri ya katiba ya Simba quorum ilitimia na kikao kikaendelea...
Kitu ambacho hujui hii timu ina mashabiki wengi na wanachama ni wachache...Jiulize why hata wewe sio mwanachama?
Kikao kilikuwa na mamlaka ya kupitisha maamuzi then
Pia nikuulize umetaja 3000,Je simba ina wanachama wangapi?
Then toa argument zako kwanini hukubaliani na 51%...kwamba zito naye kasema....eeeeeeeeh....mkuu...Kwani zito ni Mungu...hayo ni maoni yake....make your own argument.
Ongea fact sio hisia.......Simba kama imeshindwa kwa miaka 80 kuwa na idadi hiyo itaweza lini na kwa miujiza gani?
Tuwe realistic.....Mfumo unaoutaka wewe wa kumilikiwa na watu weeengi unafaa sana kwenye timu za ndondo...za mchangani...Ila kwa Mpira wa sasa wa wa kibiashara unahitaji kuwa serious on business kama zifanyavyo timu nyingi
A good ccase ni TP mazembe....ilikuwa inamilikiwa na wanachama na haikuwa na kipya...baada ya kuchukuliwa na Moise...it is one of the best teams in Africa and world
1.Viongozi waliopo wameshindwa kuwashirikisha wapenzi na mashabiki walikuwa na uwezo wa kuwafanya hao wapenzi mashabiki wawe WANACHAMA,Hao wanachama wachache ni rahisi kuwahadaa ndio kinachofanyika miaka yote.Sidhani kama kwenye vikao vyao,vya mwaka huwa wanataja idadi ya wanachama waliongezeka.Kwenye proposal ya MO ambaye anataka kuendesha timu kitaalamu nilifikiri atalifikiria hili lakini yeye hana huo mpango
2.Kabla hata jamaa hajainunua tayari ilikuwa timu ambayo imefanikiwa sana on pitch. Mazembe inamilikiwa 100% na Moise Katumbi now ni kama Azam na Bakhresa .Barcelona,Real Madrid,Bayern Munich ni timu ambazo zinamilikiwa na wanachama na bado zinafanya vizuri while AC Milan,QPR,Cardiff zinamilikiwa na watu binafsi na zinafanya vibaya.Kumilikiwa na mtu sio kigezo pekee cha timu kufanya vizuri
3.Akiwa na 51% yeye ndio decision maker anaweza kuamua chochote bila kuwashirikisha na hamuwezi kumfanya chochote.Ni sawa na bunge letu sasa wanachokitaka CCM ndio kinapitishwa bungeni kiwe kizuri au la (Sheria ya mtandao,fao la kujitoa)
4.Simba/Yanga zina fan base kubwa ndio maana hata MO/Manji wanazitaka na hawaanzishi timu zao.Kuwashirikisha wanachama wengi ni kuongeza wigo wa kuongeza mapato na kupunguza utegemezi kwa watu binafsi,kukiwa na uongozi mzuri hizo klabu zinaweza kuwa na wanachama 1 m imagine kila mwanachama akilipa fee 5000 kwa mwaka klabu itakusanya 1 bilion
5.Nothing is impossible kama wanachama wakipewa elimu ya kutosha kuhusu kubadili mfumo.Leo wapinzani wana wabunge Mbeya,Morogoro,Iringa,Mtwara,Singida,Tanga vitu ambavyo miaka 10 iliyopita ilionekana haitawezekana