mnadhani hivi vyote vimetokea kimiujiza ? furaha tulizokuwa tunazopata hasa kimataifa mnadhani ni mpera umetoa zabibu ?
- Kufuzu robo fainali mashindano ya caf ishakuwa kawaida,
- timu kubwa kama al ahly zinaiheshimu Simba,
- Simba ni klabu ya 7 kwenye ranking za Afrika,
- wachezaji wa simba wana soko kubwa wapo waliosajiliwa Al Ahly, Ufaransa, n.k.
- Makocha wa klabu kubwa Afrika wanatamani kufanya kazi Simba
Imekuwa ni dhahiri kwamba wanasimba wengi hawana elimu ya hizi bilioni 20 na hivyo wana kila haki ya kuzihoji zilipo sababu hawana elimu, Mjinga ni mtu anaebisha sababu hajui hivyo inahitaji aelimishwe nami natoa elimu, lakini hata baada ya kuelimika ukishupaza shingo unapandishwa cheo kuitwa mpumbavu.
Simba ya enzi hizo kabla ya Mo ilikuwa imejichokea, Mo akaahidi kununua asilimia 49 ya umiliki wa timu kwa bilioni 20, Kwa mantiki ya kawaida timu inapopata pesa huwa inawekeza kwenye timu ifanya vizuri zaidi, Mo alianza kutia pesa na kweli tulijionea kwa macho yetu mapinduzi makubwa sana hayajawahi kutokea hapa nchini kwenye soka letu, Kwa misimu minne mfululizo alikuwa anatia bilioni 5 kwa njia ya kuigharamia timu na mwaka 2021 rasmi akamaliza deni lake na kupewa umiliki wa timu.
Wanoulizia aliingiza benki gani hawa ndio kundi wanalodhani kila kitu kinauzwa kwa pesa taslimu, ningependa kuwaeleimisha si kila kitu huuzwa kwa pesa taslimu, Mfano Diamond Platnumz ni mwanahisa wa wasafi tv na radio kapewa hisa za umiliki wa asilimia kadhaa kwa kuweka jina lake tu ambalo lina thamani kiasi flani, Mtu unaweza kuwa na hoteli yako imechoka ukawa unatafuta mwekezaji umuuzie umiliki nusu kwa milioni 100, lakini pia ni sawa hata yeye mwenyewe akifanya ukarabati unaoweza kuthaminika ni milioni 100, Basi ndicho kilichotokea simba, umiliki wa asilimia 49 enzi hizo ulithaminishwa kuwa bilioni 20, Haikuwa lazima Mo atoe pesa cash Taslimu, kilichotokea ni kwamba aliigharamia timu kwa miaka minne kwa thamani iliyofikia bilioni 20 na timu ilipojiridhisha kweli ni kiasi hicho ikampa umiliki, hizi ndizo gharama alizotumia.
- Usajili wa wachezaji + signing fee (hasa wachezaji ghali wa nje)
- Gharama za kuvunja mikataba ya wachezaji ili kuwapisha wapya
- Mishahara wachezaji (hasa wachezaji ghali wa nje)
- Makocha ghali wenye uzoefu mkubwa kimataifa
- Usafiri (Safari za ndege mikoani na nje ya nchi, gharama za basi, n.k.)
- Malazi (Hoteli za kifahari mikoani na nje ya nchi, Hostel, n.k)
- Vyakula na vinywaji (wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, n.k.)
- Matibabu kwa wachezaji wenye majeraha
- Kiwanja cha Bunju
hayakuwa mazingaombwe ni PESA !!!