View attachment 3013139
Kufuzu robo fainali mashindano ya caf ishakuwa kawaida, timu kubwa kama al ahly zinaiheshimu simba, Simba ni ya 7 Afrika, wachezaji wa simba wanagombaniwa na klabu kubwa kama Al Ahly, n.k. mnadhani hivi vyote vilitokea kimiujiza, LA HASHA, ni pesa nyingi sana zimetumika, hakunaga cha bure !
Imekuwa ni dhahiri kwamba wanasimba wengi hawana elimu ya hizi bilioni 20 na hivyo wana kila haki ya kuzihoji zilipo sababu hawana elimu, Mjinga ni mtu anaebisha sababu hajui hivyo inahitaji aelimishwe nami natoa elimu, lakini hata baada ya kuelimika ukishupaza shingo unapandishwa cheo kuitwa mpumbavu.
Simba ya enzi hizo kabla ya Mo ilikuwa imejichokea, Mo akaahidi kununua asilimia 49 ya umiliki wa timu kwa bilioni 20, Kwa mantiki ya kawaida timu inapopata pesa huwa inawekeza kwenye timu ifanya vizuri zaidi, Mo alianza kutia pesa na kweli tulijionea kwa macho yetu mapinduzi makubwa sana hayajawahi kutokea hapa nchini kwenye soka letu, Kwa misimu minne mfululizo alikuwa anatia bilioni 5 na mwaka 2021 rasmi akamaliza deni lake na kupewa umiliki wa timu.
hayakuwa mazingaombwe ni PESA, Ndizo pesa zilizofanya Simba iwe na wachezaji wzuri ngazi za kimataifa, makocha wenye uzoefu kimataifa, bonas kila mechi, safari za ndege nje na ndani ya nchi kama vile ni daladala, n.k. ni PESA, sio mazingaombwe.
Kimsingi wote wanaomsema Mo wanatakiwa waombe msamaha
Usajili wa wachezaji + signing fee (hasa wachezaji ghali wa nje)
Gharama za kuvunja mikataba ya wachezaji ili kuwapisha wapya
Mishahara wachezaji (hasa wachezaji ghali wa nje)
Makocha ghali wenye uzoefu mkubwa kimataifa
Usafiri (Safari za ndege mikoani na nje ya nchi, gharama za basi, n.k.)
Malazi (Hoteli za kifahari mikoani na nje ya nchi, Hostel, n.k)
Vyakula na vinywaji (wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, n.k.)
Matibabu kwa wachezaji wenye majeraha
Kiwanja cha Bunju