Well said. Hivi km kuna watu wanafikiria matangazo kwenye jezi na udhamini Wa Azam, Mbet au Sportpesa vinaweza kuendesha timu kwann Yanga haikutoka kwenye dhiki hadi alipoingia GSM? Au bado anafanya nn pale Yanga kama mapato hayo yanatosha? Watu hawajui wanachokiongea. Akitoka Mo ndo watajua walikuwa hawajui. Biashara ya uwekezaji katika hizi timu za Nchi km Tanzania bado hazitoi faida yoyote ya kuweza kuwavutia wawekezaji. Hawa tulio nao/ tuliye naye si muwekezaji hasa, bali ni kama mfadhili tu mwenye mapenzi na timu. Ht Mo mwenyewe najua anajua kuwa hatarajii faida yoyote ya kifedha kutokana na huo uwekezaji wake any time sooneri. Ndo mana huku kwetu hatujawekewa ile Sheria ya FIFA ya financial fair play ambayo inavilazimisha vilabu kutumia kile tu kinachopata kutokana na biashara ya mpira. Sisi bado tunajiendesha kwa ufadhili wa matajiri wenye fedha, wawe wamiliki au wapenzi Wa vilabu hivyo.
Kumtoa Mo mnaweza kuona ni ushindi lkn huyo mnayemfikiria atawatoa hapo mlipokwama, hawezi kuwa Kigwangwala wala huyo CPA Massoud. Hawana uwezo huo.