MO alishatia Bilioni 20 kitambo na bado anaendelea kugharamika kwa mapenzi ya timu, ni wajinga pekee wanahoji nami nawaelimisha kuwatoa ujinga

Alikuwa na timu zikamshinda ngoja awanyooshe Mikia FC.
 
Wewe ndio umemmilikisha hiyo team au??
Ni wanasimba tuiommilikisha kihalali kabisa, si kwa furaha zile alizotupa akiwa anaingiza bilioni 5 kila mwaka 2017/18 hadi 2020/21,,, unakumbuka simba ilivyokuwa moto wa kuotea mbali ?? unadhani ilikuwa miujiza ya zabibu kudondoka chini ya mpera ?

imekuwa kawiada timu kufuzu robo fainali, ni BILIONI 20 zilizosajili wachezaji wa kimataifa, makocha wazuri, bonasi za mechi, ndege kuwa kama daladala, mahoteli ya nyota tano, n.k.
 
Pesa ambazo hao hao wanabodi wanadai huwa anazidai?? Huo sio uwekezaji bali ni unyonyaji
 
Pesa ambazo hao hao wanabodi wanadai huwa anazidai?? Huo sio uwekezaji bali ni unyonyaji
Ni tamaa zao tu, MO alishaweka mzigo na ni halali timu kuwa yake, Mo kafanya mambo makubwa sana kwa pesa alizoweka, sikuhizi kufuzu robo fainali ishakuwa kawaida, timu kubwa kama al ahly zinaijua simba si ya kuibeza, n.k.
 
2021 rejea we are 2024 now
 
Unajua kitu ambacho watanzania tuko nacho vizuri ni kuongea na hasa kwemye criticism.

Kuongea ni kitu rahisi sana ambacho kinaweza kufanywa na mtu yeyote ila linapokuja swala la utendaji ni watu wachache sana wenye kuweza.

Kama matangazo yanalipa kiasi cha kuifanya timu iweze kujiendesha bila mwekezaji kwanini hatukuprint jezi zenye nembo ya Simba ili tupate hela ambazo zingeingia direct kwenye Account ya Simba kuliko kumtafuta mwekezaji ambaye anaenda kunufaikia kupitia brand ya timu?

Kama wewe una amini mwekezaji akiweka matangazo kwenye jezi ya timu yako anaenda kunufaika kwanini usitumie hiyo fursa kujiendesha mwenyewe kwa kuweka matangazo ya Club yako ili uwe unanufaika mwenyewe?

Mpaka unamuachia mtu aweke matangazo yake kwenye jezi yako ili wewe uweze kuendesha timu kupitia hela zake maana yake ni kwamba wewe umeshindwa kupata hiyo faida ambayo saizi unaiona.

Sasa kwanini uwe obsessed na mtu anayepata faida kupitia rotaion ya hela zake?

Vipi wanaomiliki 51% ambayo ni kubwa wao wametoa bei gani mpaka sasa?

Au sisi wenye 51% kazi yetu ni kuchambua faida anazopata mwekezaji kupitia ads?

Kabla ya MO Dewj Simba ilikuwa katika hali gani?

Naskia chinichini kuna mwekezaji ambaye anatajwa kuwa yupo tayari kuichukua Simba, na huyo mwekezaji yupo nyuma ya hao wanaopiga kampeni za Mo atoke

Alikuwa wapi kipindi hicho ambacho Simba ilikuwa inataabika?

So ni wazi kuwa ameanza kuiona value ya Simba kutokana na hela za MO.

No offense lakini namuona kama shangingi wa bar anayefuata meza yenye bia nyingi.

Ni kama Zubeda mke wa Profesa Jay aliyemtoa kijijini sitimbi akila magimbi akijipaka mafuta ya kupikia lakini alipomleta mjini na kuanza kumgharamia demu akaamza kushoboka na mataita wa mjini.

Some spazz gotta say "Ooh MO unajua anapata sana faida halafu anasingizia Simba inampa hasara"

Mimi na wewe kama mashabiki hatufaidiki na chochote kwenye Simba zaidi ya furaha (labda kama kuna wenzangu mpo kwenye payyrol) ni Furaha ambayo tunaipata kupitia matokeo mazuri tu ndio malipo yetu.

Kama MO anapata faida ni non of our business just like Man U au Man City ambazo tunazishabikia kwa mapenzi yetu kwa lengo la kupata furaha.
 
Aliweka Benki ipi mkuu??
 
20bn plus za wanachama ziko kwenye account gani . Tuache kupiga kelele za Mo peke yake. Leteni balance ya hela za wanachama period.
 
Aliweka Benki ipi mkuu??
kwani manunuzi yote ni kwa mfumo wa benki ?

Naweza kuja kwako nikakwambia nahitaji uniuzie nusu ya umiliki wa hoteli yako kwa njia ya kuikarabati iwe nzuri zaidi, yaani mafundi, vifaa, finishing, ulinzi, n.k. nagharamia mimi. hata Diamond hakuna pesa aliyoweka pale wasafi yeye kaweka jina lake tu, sembuse mtu kupewa umiliki kwa kugharamia ?

Tatizo naloona ni kwamba watanzania wengi elimu bado ni tatizo kubwa sana
 
Pesa za matangazo kwenye jezi zingekuwa zinafaida kuliko pesa anazotoa mwekezaji kwenye gharama za uendeshaji wa timu.

Basi Yanga wasingetembeza bakuli kwasababu walikuwa na option ya kutengeneza products nyingi na kuzitia logo ya Yanga kisha wao wakaendelea kuingiza mpunga.

Lakini kingine ambacho wanasahau ni hiki.

Watu wanasema Mo anapata faida kwenye matangazo as if ni upande tu wa Mo unaofaidika kwenye hilo.

Lakini wao hawafikirii pia kupitia malengo ya MO kutangaza biashara yake pia kumeweza kuifanya hata Simba nayo kutangazwa na kujulikana.

Simba kabla ya Mo ilikuwa haina jina kimataifa lakini kupitia MO imejulikana na kuna percent ya pesa imeweza kufaidika. Lakini hiyo watu hawaisemi wanasema ya Mo tu
 
Mo ni mwizi narudia ni mwizi anayenibishia kesho aende kwenye maduka yake yaliyopo mataa ya mnazi mmoja kuelekea mnara wa saa Kuna kanga za Simba zinauzwa zimezalidhwa na kiwanda chake Cha morogoro bila Simba kuwa na mkataba na hawapati hata senti tano.
Watu wanaomtetea mitandaoni Tena anawalipa kijiwe Chao kipo msikitini karibu na Zahri hotel Kama inaelekea DTB bank nyuma ya ofisi zake.
Mo akiondoka hauzidi nusu saa wawekezaji wengine wanajitokeza.
 
unadhani pesa zinazotumika kuwaleta kina Benchikicha zinadondoka kama mvua ?
 
Ndiyo kusema wakati hayo yote yanafanyika timu haikuwa na mapato yake nje ya udhamini wa Mwekezaji?
Yaani mapato yaliyotokana na gate collection, fedha za CAF, wadhamini kama Sportpesa, Mbet, Azam Media, nk!!!
 
wanachama wapi?
 
Ni documents gani Simba Sc ilisaini na mwekezaji...

Ya kwamba asilimia 49 ya hisa zake zitalipwa kwa mfumo wa matumizi ya timu?

Kitu usichokijua we mbwiga, kwasasa tunapambana wajumbe wa bodi upande wa wanachama wajiuzulu then turudi kuzaa na mwekezaji.
 
Hakuna mwekezani anayelipa zote kwa maramoja bali huwa mnakubalina schedules.Kama mnaona za Mohammed haIkuwa za maana mngeziacha hizo fedha na siyo kuItumbua harafu baada ya kufaidi ndo mnadai ushahidi wa pesa.
Ukitaka ushaidi waulize viongozi walikuwa wansema kila kitu Kiko vizuri
 
Mambo ni kimya kimya hapa bongo, Umewahi kuuona hata mkataba original wa jezi wa Simba na Vunja bei ???
 
Ndiyo kusema wakati hayo yote yanafanyika timu haikuwa na mapato yake nje ya udhamini wa Mwekezaji? Yaani mapato yaliyotokana na gate collection, fedha za CAF, wadhamini kam Sportpesa, Mbet, Azam Media, nk!!!
Kawaulize wazee wa Simba, watu washajenga na kununua magari ya kifahari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…