MO alishatia Bilioni 20 kitambo na bado anaendelea kugharamika kwa mapenzi ya timu, ni wajinga pekee wanahoji nami nawaelimisha kuwatoa ujinga

Kwa huu mgogoro unaoendelea sina imani kama simba itafanya vzuri msimu ujao tena. ILA mbali ya yote hata kama mo ni tapeli au viongozi wanahujumu kwa timu zetu za kitanzania hazina uwezo wa kujiendesha zenyewe kwa mapato yake yenyewe
Timu zinaweza kujiendesha ila upigaji ni mkubwa sana, kila anaeingia anataka apige asepe.
 
Timu zinaweza kujiendesha ila upigaji ni mkubwa sana, kila anaeingia anataka apige asepe.
Mkuu mimi sijui sana ila Embu nipe roughly estimation kwamba nature ya Tanzania mpira kujaza mpaka simba na yanga au kununuliwa kwa jezi. Hivi unafikiri unaweza kuendesha timu kama simba na yanga kwa gharama zote kuanzia wachezaji, watumishi, safari ,maradhi, marupurupu unafikiri ni rahisi hivyo mkuu?
 
Sio rahisi ila hizi timu zinahujumiwa sana na wanaopewa mamlaka ya kuziongoza.
 
Kupitia haya maelezo yako, hivyo vyanzo vya mapato havina tija, na ndiyo maana mwekezaji wenu anadai mpaka hela aliyonunulia mchicha siyo!
Sasa kama kilichotokea ilikuwa ni makubaliano yaliyoafikiwa na pande zote mbili, kwanini uanze kuleta tamaa?

Kama terms walizokubaliana ili pesa ziingie moja kwa moja kwenye Club bila MO kuzidai ilikuwa ni kukamilisha hiyo transformation na nyie ndio mnaokwamisha hiyo transformation kwanini tena muanze kulalamika mkidaiwa?
 
Wanasema huwezi ukajua value ya ulichonacho mpaka pale utapokipoteza.

Pale Simba wanaosema Mo aondoke wengi wameahidiwa hongo na huyo mwekezaji kivuli.

Lakini kitu ambacho nimeshangaa wanasimba wengi hawakifikirii ni kwanini wachezaji, makocha wamenyooshea vidole uongozi na bado mashabiki wamejipumbaza na kumvamia MO?

Pale Simba kuna skendo nyingi za viongozi wanaofanya kazi ya udalali kwa wachezaji hivi ni kweli hili hatulioni kuwa ni tatizo na badala yake tatizo tunaona ni MO?

Kuna interview ya MO aliwahi kuhojiwa akiulizwa kama imewahi kutokea akiombwa milion 200 za kumsajili mchezaji na badala yake akaletewa mchezaji wa milioni 90.

MO alisema hilo linawezekana ila sina uwezo wa kulithibitisha.

Sababu kubwa ya Kibu kuwakomalia Simba usajili kwa kutaka pesa ndefu ilikuwa ni kwasababu ya middle man aliyemsajili kutoka Mbeya City alikuwa anachukua percent kadhaa kwenye signing fee ya Kibu.

MO alipogundua na kuamua kuwaambia wajiuzulu wote ili kuijenga upya Simba ndio hapo mjadala wa MO aondoke ulipoanzishwa.
 
Mwamedi mhuni Sana,

Zikiingiaga tu zile pesa za caf ndo utaskia zile kauli zake jinsi gani Simba sc inavomtia hasara

Lengo tu zisihojiwe, kisingizio Ni alitoa pesa za usajili na mishahara ya wachezaji.

Simba ingekua inamtia hasara angeiachia Tu.
Hakuna mhindi wa hivyo yani, afanye kitu kwa hasara? Hajazaliwa.
 
Hakika umenena✔️
 
Hivi kulikuwa na makubaliano ya maandishi (mkataba) uliokuwa unasema MO alipe Bilioni ishirini kwa namna hiyo? Au hili limekuja baadaye?
 
Kha!! Mimi nahusika vipi sasa kwenye hayo madai!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…