Yaani hii ni thread iliyopo jukwaa la sports na wadau wanavotiririka kuchangia hii mada yaonesha wazi ni namna gani bado watu wengi ni mbumbumbu katika maswala ya soka.
Yaani watu hamjui lolote kuhusu CLUB LICENSING!???
Eti Bakhressa amebid kuinunua Simba na nyinyi mnaamini wakati tayari ana umiliki wa Azam FC.
Timu za majeshi huko daraja la chini zimeshaanza kubinafsishwa, majuzi Simba Sc alikuwa Dodoma kucheza friend match na Dodoma Football Club (DFC) ambapo ilikuwa ikiitwa Polisi Dodoma FC.
Na kuna timu nyingine ya majeshi nayo imebinafsishwa inaitwa Biashara FC sikumbuki ilikuwa Polisi ya mkoa gani.
Ila kifupi habari ndio, hakuna tena 'ruksa' kwa taasisi, mtu, kampuni kuwa na umiliki wa timu zaidi ya moja katika soka la nchi husika!!!