Mo Dewji akana kujiuzulu Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba na Kubakia kuwa Mwekezaji

Mo Dewji akana kujiuzulu Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba na Kubakia kuwa Mwekezaji

Status
Not open for further replies.
simba walifanya kosa kubwa sana kumfukuza Uchebe, ni bora wangemuacha maana alikuwa tayari amezoea ligi ya Tanzania. Kwa huyu kocha mpya sidhani kama atamaliza msimu mmoja bila kufukuzwa, kocha hana mbinu kabisa na mwisho kuna wachezaji pale wanakula pesa ya bure simba iangalie namna ya kuachana nao msimu ujao..
 
Kama Haji Manara alivyosema baada ya droo ya Yanga kuwa wachezaji hawako makini kutendea haki katika viwango vyao na motisha wanaopata kutok kwenye uongozi. Pole sana kwa wana Simba wenzetu Mo ni binadamu na mwenye hisia anafanya kazi kama mtu mwingine ni mda ajipumzishe kwenye jukumu moja na wengine wapewe nafasi.
 
Kwani kuna nini kinaendelea?Nipo gizani ati!
 
Critics wengi wanasubiri mambo yaharibike ndio waanze porojo

Mechi ile ya yanga tulivyoongoza zile goli mbili mlipiga sana kelele kua this is simbaa na round hii hadi kocha tulimsifia. Lakini baada ya yanga kurudisha mkaanza kumtupia lawama kocha tena wakati ni kikosi kile kile kilicho pata magoli mawili ya kuongoza na hakijabadilika.


Kocha ndio kwanza ana mwezi hajawajua wachezaji vizuri na usikute kikosi cha leo asilimia 80 alipanga msaidizi, lakini lawama zote kwa kocha mkuu sijui kwanini?



It's Scars
 
Serikali ya muungano ina watumishi wangapi??
 
MO ni tapeli tu kama matapeli wa Ubungo aseme sababu ya msingi ya kujiuzulu asijifiche kwenye kichaka cha Mapinduzi cup.
 
Kama Manara alivyosema kuwa wachezaji hawatendei haki namna wanavyopewa huduma nzuri kutoka kwenye uongozi wa klabu na matokeo yanayotokea wakiwa na viwango bora kabisa. Mo apumzike wengine wapewe nafasi. Chungu lakini dawa!
 
Huu ni muda muafaka wa YANGA kutengeneza kikosiimara wakati watani wanataabika. Katika hilo inabidi isafishe kabisa mauchafu yanayoharibu sifa na heshma ya jina la timu, mtaa wa timu rangi ya timu pamoja na nembo ya timu. Kuna ka jarida kanaitwa JANGWANI ni cha michezo sijui kinamilikiwa na nani ila ndani yake kuna matangazo ya kitapeli ya FREEMARSON a.k.a CHAMA HURU pamoja na ya nguvu za kiume hayo yote ni matapeli na serikali imekataza na inawakamata hao wanaojiita chama huru lakini hili gazeti mbona tunaolisoma ni watu wenye hesma zetu nani anaruhusu uchafu huu?
 
MO ni tapeli tu kama matapeli wa Ubungo aseme sababu ya msingi ya kujiuzulu asijifiche kwenye kichaka cha Mapinduzi cup.
Gharama za uendeshaji ndio zinamkimbiza MO,hapo simba , yaan ndio kajitoa jumla hajanyoosha maelezo,

Huku nchi za dunia ya 3,hatuna financial fair play , ndio maana wenzetu wameiweka kumlinda hata muwekezaji

Pale simba Mo alitega ,simba iwe inafika angalau robo kwenye CL , hapo anapata karibu billion 1.5 , bado kila mech anajaza uwanja kama za kariakoo derby.hapo anakuwa na uhakika wa Million hadi 300 kwa mechi 1 za hatua za makundi ,Hivo anakuwa na uhakika wa kupiga angalau billion had 3 kwenye CL ,

Sasa Angalia kaishia hatua ya preminary kwenye CL , anabaki kugombania VPL ambapo bingwa anakula mil 80 .

Huku analipa mishahara na malupulupu kwa mwaka hadi billion 4

Hii ni hasara kubwa sana , hii ni biashara kichaa,lazima ukimbie tu
 
Mfanyabiashara Mohamed Dewji ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba akisema atabaki kuwa muwekezaji pekee.

Hiyo ni baada ya Simba kufungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar kwen

mooooooooo.png
 
MO DEWJI ambaye ni mwekezaji katika club ya mpira wa miguu, SIMBA Sc amejiuvua cheo hicho baada ya matokeo mabovu katika mchezo wa leo hii.

Simba SC aliingia dimbani na mtibwa SUGAR na kupokea kipgo cha 1-0


InShot_20200113_225708352.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
MO anatumia uwezo wake vibaya kuwanyanyasa wasio nacho.

Anajimwambafai eti kalipa 4B mishahara kwa mwaka.. ivi unataka kusema simba ni kubwa kuliko serikali ya zanzibar.

Serikali ya Muungano yenyewe kwa 4B inalipa miezi 4 hadi 5.


Nilipo soma tangazo la kujiondoa nikajiuliza , kulikua na umuhimu gaji wa kutaja fedha ulizo toa.


Ipo siku utavuna unacho panda kwa kuwaihia wananchi maskini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijakuelewa Tabutupu ! Taabu tupu ! Eti nini ? Nadhani unatania kuhusu mishahara inayolipa serikali ya Tanzania kwa mwezi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom