Mo Dewji: Simba inanipa hasara, ningenunua hata Ndege

Mo Dewji: Simba inanipa hasara, ningenunua hata Ndege

Huu ni ukweli.

Kuna mtu alikuwa ameajiriwa na Mo siku hizi amamuita "Mudi" kama njia ya mzunguko ya kumshusha hadhi yake. Lakini ukweli unabaki kuwa ukweli kwamba Mo anao uwezo wa kuiajiri familia yao yote na kuwalipa mshahara mpaka mwisho wa maisha yao!!
Kwa hiyo akina Mohamed wote wenye hela hawatakiwi kuitwa Mudi! Isipokuwa Mo! Halafu wale Mohamed wenzangu na mimi, ndiyo wanatakiwa kuitwa Mudi!

Unaweza kunifafanulia kidogo haya maelezo yako? Maana sijaona kosa kwa mtu anayeitwa Mohamed, kuitwa Mudi eti!!
 
Mudi kila siku analalamika Simba inamtia hasara ila bado yupo tu.! Tafakari chukua hatua
Hii kitu inafikirisha sana. Maana yake anataka kusema akiondoka, basi na simba itapotea kabisa kwenye ramani ya soka!

Na ili kuhakikisha haifi/kupotea, basi analazimika kuingia hasara, ili kuikoa!! Kweli akili za mbayuwayu, changanya na zako! Mwenzake kwa upande wa Yanga, hata humsikii akilialia!!
 
Kwa hiyo akina Mohamed wote wenye hela hawatakiwi kuitwa Mudi! Isipokuwa Mo! Halafu wale Mohamed wenzangu na mimi, ndiyo wanatakiwa kuitwa Mudi!

Unaweza kunifafanulia kidogo haya maelezo yako? Maana sijaona kosa kwa mtu anayeitwa Mohamed, kuitwa Mudi eti!!
Hapana. Yeye anajulikana siku zote anaitwa Mo. Muddy pia ni sahihi lakini si kwa jinsi ya kudhalilisha. Unajua ni kwa nini tuliacha kutumia neno "Zeruzeru" badala yake tukaanza kutumia "Albino" kwa ndugu zetu wenyewe ulemavu wa ngozi? Ni kwa sababu wenyewe walisema kuwa kuitwa zeruzeru ni kuwadhalilisha!!

Kuna mtu anaitwa William ni sawa na yule anayeitwa Billy. Lakini usimuite mtu Willliam wakati siku zote anajulikana kwa jina la Billy.
 
Kwa hili sikuungi mkono Mo. Kiongozi anapaswa kujua aongee nini wakati gani mahali gani mbele ya Nani. Maneno yako yanamaanisha uko Simba Kwa kujitolea na siyo Mwekezaji kama Katiba inavyotaka. Sisi tunajua 20b ndo inayokupa haki ya kuwa Mbia pale Simba na siyo mfadhili. Add ons unazotoa Kwa Simba hata kama si sehemu ya mkataba lakini hazipaswi kutangazwa Kwa Kila Mtu na kuonyesha kwamba bila wewe Simba si lolote tena. Umeoa mwanamke halafu Kila siku unamwambia bila wewe ningekuwa Tajiri maana hapa gharama za kukulisha na kukuvisha zingetosha kununua gari?
 
Hapana. Yeye anajulikana siku zote anaitwa Mo. Muddy pia ni sahihi lakini si kwa jinsi ya kudhalilisha. Unajua ni kwa nini tuliacha kutumia neno "Zeruzeru" badala yake tukaanza kutumia "Albino" kwa ndugu zetu wenyewe ulemavu wa ngozi? Ni kwa sababu wenyewe walisema kuwa kuitwa zeruzeru ni kuwadhalilisha!!

Kuna mtu anaitwa William ni sawa na yule anayeitwa Billy. Lakini usimuite mtu Willliam wakati siku zote anajulikana kwa jina la Billy.
Bado somo halijaingia kabisa kwenye ubongo! Yaani akina Mohamed wengine wakiitwa Mudi, ni sawa! Halafu akina Mohamedi wengine (wenye hela) wakiitwa Mudi, wanaona ni udhalilishaji! Na hivyo wanataka waitwe Mo! 🤔

Sawa kiongozi. Ngoja tu ibakie hivi hivi.
 
Back
Top Bottom